Wanabodi,
Juzi katika kikao cha bunge, Spika wa Bunge, Mhe. Anne Maklnda, alimtaja Mbunge wa Singida, Mhe. Tundu kama ndie Mbunge anayeongoza kwa kuwa chanzo cha vurugu za bungeni, kwa kuongoza kwa utovu wa nidhamu, kuleta fujo na vurugu bungeni, hali ambayo sio tuu inahatarisha hali ya utulivu, amani na usalama wa bungeni, bali pia kumepelekea Spika kufuta baadhi ya ratiba za bunge ambazo zilikwisha ridhiwa na kuingizwa kwenye order paper ikiwemo kupokea hoja binafsi za wabunge, kwa kilichoelezwa kuepuka vurugu zaidi.
Jana kika cha kamati ya Uongozi kimekaa kujadili hali hiyo na matokeo yake, tutayapata kesho asubuhi baada ya kipindi cha maswali ya papo kwa papo na maswali na majibu! ni hakika rungu la kiti, lazima litamshukia Mhe. Tundu Lissu!.
Swali la kwanza la kwanza ambalo wengi mtapenda kujiuliza ni, ni jee ni kweli, Mhe. Tundu ni mtundu na ndie chanza cha utovu wote wa nidhamu wa bunge hili la kumi?, kama anavyoelezwa na Madam Speaker?, au huo utundu wa Mhe. Tundu, sio utundu bali uzingatiaji wa kanuni za Bunge, kufuatia Mhe. Spika, kuonyesha udhaifu mkubwa katika kuliendesha bunge kwa kutokuzingatia, sheria, taratibu na Kanuni?.
Kwa vile mimi ni mmoja wa watu tunaomfahamu Mhe. Tundu, Tangu akiwa Shuleni, naomba kuchukua fursa hii kumfariji Mhe. Spika, kwa kumuomba asiumize sana kichwa chake kuendelea kubishana na Mheshimiwa Tundu Lissu kuhusu kanuni za bunge, wala wasipoteze muda kumuadhibu kwa jambo ambalo liko wazi kabisa na udhaifu unajulikana tangu chanzo chake, ulipo na labda utaendelea kuwepo, hata akiadhibiwa vipi, kwa sababu Mhe. huyu ni mbishi hakuna mfano!, haswa pale anapokuwa na uhakika kuwa yuko right!.
Nashauri Mhe. Spika, lazima ufike mahali, umkubali huyu jamaa kuwa lile jina lake la Tundu, sio jina tuu, huyu bwana analiishi jina lake kwa kuwa ni mtundu kweli pale kanuni zinapopindishwa ili kutoa mteremko kwa upande fulani!.
Nimebahatika kusoma na Mhe. Lissu shule moja kule Ilboru, (sio darasa moja) miaka hiyo enzi za Mkuu mmoja aitwae Bino!. Huyu Bino alikuwa ni mwalimu mkuu bingwa wa nidhamu, ila kwa Tundu, alinyanyua mikono juu na kwisha kuishusha juu baada ya kuthibitika kuwa japo Tundu alikuwa "toto tundu", ila pia ndie aliyekuwa kipanga wa darasa lake!, kwani pepa alikuwa akizifumua, utadhani mtihani katunga yeye!.
Tundu Lissu alijiunga shule ya vipanga ya Ilboru akitokea Galanos, wakati huo akiitwa Antipasi Tundu, na alikuwa ni mtoto mtundu kweli!. Wakati huo sisi Wasukuma tukiitwa "Wasukusu", wenyeji wakiitwa "wamenye" huku jamaa wa Singida wakijiita watu wa "Singapore", uji ukiitwa "sumu", na nje kulikuwa na duka la kwa "Akwii".
Utundu wa Tundu Lissu ulkikuwa ni kwenye mishe mishe tuu hizi za zile, haijulikani alikuwa akisoma saa ngapi, ila pepa zikija, anafumua ile mbaya!. Moja ya maeneo ambayo jamaa alikuwa ni ni mtundu au tusema ni mbishi, ni kwenye school debate!. Jamaa akishakuwa na uhakika yuko on the right track, ni mbishi hakuna mfano!. Hata nami nilikuwa na matatizo yangu tangu shule, yale matatizo ya kawaida ya Chapa Ng'ombe, unapokutana na vibinti vya Vyeupe vya Kiarusha pale Mlimani Ilboru, ukijumlisha na lilke baridi la kule, tena wakati huo, "bwawa halijaingia luba!'...
Tundu lissu kama livyoingia Ilboru, vivyo hivyo ndivyo alivyoondoka na wani kali, akaenda UDSM na sisi vilaza wengine tuykaishia vile vyuo vya mashenzini!. Tulipoteana kwa kipindi cha miaka 10!, tulikuja kukutana tena mjini Atlanta, yeye akiwa na yeke nami na yangu, ndipo akanieleza yuko LEAT, na huko aliichachafya serikali vivyo hivyo kama anavyo mchachafya Madame Spika, kwa kumsubu bila huruma!.
Pamoja na utundu wote huu wa Mhe. Tundu Lissu, wakati tukisubiria kusikia ni adhabu gani itamfika hapo kesho, kuna maswali matatu tujiulize!.
- Jee ni kweli Mhe. Tundu Lissu ni mtundu kihivyo na ndio anayeongoza kwa utovu wa nidhamu hadi kustahili adhabu kali?.
- Au ni Spika ndiye dhaifu hadi kushindwa kumdhibiti Tundu Lissu na utundu wake?.
- Baada ya kuthibitisha, Mhe. Tundu Lissu alikuwa ni mtundu toka shuleni, jee nani wa kubadilika kati ya Mhe Tundu Lissu na wabunge wa upinzani, wakae kimya wakati sheria, taratibu na kanuni, zikikiukwa, na kupindishwa?, hivyo kumpatia fursa Mhe. Spika kujiendeshea bunge anavyotaka, ili kudumisha utii, na nidhamu, bunge liwe la amani?.
- Hivyo Mhe Spika kuwathibitishia Watanzania kuwa hata yeye ambaye ni Spika wa majaribio ya "jinsia" "ameweza" kuliendesha bunge vizuri tuu, ambalo ni mhimili mmoja wa dola, hivyo jee, 2015, tukamilishe majaribio ya "jinsia" kwa mihimili miwili iliyobakia?, ili nchi yetu iwe ni nchi ya usawa halisi wa kijinsia?.
Wasalaam
Pasco.
(Skulu Meti wa Toto T).