Vurugu za Bungeni: Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!.

Amsumbue kivipi ?...hakuna kitu kama hicho.
 
Amsumbue kivipi ?...hakuna kitu kama hicho.
Sio vibaya kumkumbusha maana kuna watu hawanaga shukrani, hata umtendee mema vipi, kwa vile alitendwa basi ni kuvurumisha makombora mwanzo mwisho!. Mwenzake Mbowe keshaonyesha ustaarabu, bado Lissu, ndio tunamsubiria Leo.
P
 
Nimeyasikiliza mahojiano haya, namshauri haya ambayo Tundu Lissu anazungumza kwenye media kuhusu shambulio lake, na waliohusika ambao anawataja kwa majina, aende akawaripoti polisi ili uchunguzi wa kijinai ufanyike, asiporipoti aitwe athibitishe kauli zake za uhusika wa huyo mtu, akishindwa kuthibitisha, anastahili adhabu kali!.
Huwezi kumsingizia tuhuma nzito hivi mtu aliyelala usingizi wa milele na hawezi kujibu!.
P
 
Duh
 
 
Ulichambua historia vizuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kuthibitisha TL ni Simba Dume!. Wanabodi,
Leo nimelikumbuka bandiko hili kuhusu TL kukosesha mtu usingizi baada ya kuiangalia clip hii
View: https://youtu.be/UXFoyKtbEEA?si=l6IxoAUVEFFWXWSP
Usikute TL anamkosesha mtu usingizi!, halafu itokee TL ndie asimame nae 2025!, na alivyo hana break... si kuna mtu ataogeshwa .... kila uchao?.
Hapa ni ninauliza tuu!.

Ndio maana nimeshauri, kama mgombea wa urais wa chama kubwa 2025 ni mwanamke, then vyama vyote viweke wagombea urais wanawake wapambane na sio jitu dume zima lipambane ma majike!.

Hivyo nikapendekeza Iwapo Watanzania wataamua 2025 twende na Mwanamke, mnaonaje tukiwashauri CHADEMA wasimamishe Mwanamke? Maana Mwanaume kushindwa na Mwanamke ni aibu!

Na endapo wapinzani watakuwa hawana kabisa mwanamke ambaye ni match na mgombea wa chama kubwa hivyo ni lazima kumsimamisha mwanaume, then mgombea wa upinzani asiwe TL ili kumstahi mgombea mwanamke, maana jinsi TL asivyo na breki, hachelewi kumuogesha na mvua ya ... TL saizi yake alikuwa JPM na sio huyu Maza Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

hivyo nimeshauri mgombea wa upinzani awe Kama CCM Itamsimamisha Rais Samia 2025, Mnaonaje Freeman Mbowe Awe Mgombea wa Upinzani? Atapiga Ndege 3 kwa Jiwe Moja, Atavuna Wabunge Wengi ila... sababu ya kupendekeza FM ni kufuatia kukubali maridhiano na CCM kugawana nusu mkate, TL anayabeza maridhiano Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

Hili mnalionaje?.

P
 
Ccm haitegemei matokeo ya hesabu za kura kushinda, hilo hata wewe unalifahamu.
 
Kufuatia Tundu Lissu kugombea uenyekiti wa Chadema, nimelikumbuka bandiko hili ili kuwasaidia wasio mjua Tundu Lissu, wamjue.

Chadema kwa hapa ilipo, japo kinaitwa ni chama cha upinzani, ni upinzani jina tuu sio upinzani nia, kwa sasa Chadema ni kiji saccos fulani hivi cha kupigia tuu fedha za ruzuku, lakini hakina mpango wowote wa kushika dola kwasababu kiongozi wake wa sasa hana ubavu wa kuiingiza Chadema ikulu.

Kama kuna wana Chadema, wana nia ya dhati, Chadema, kiwe ni chama cha upinzani kweli, chenye nia ya kushika dola, then ni lazima wafanye mabadiliko ya uongozi, wamchague mtu mwenye uwezo wa kuiingiza Chadema Ikulu.

CCM imeota mizizi iliyojichimbia chini sana na kukomaa kwa miaka mingi, hivyo kuing'oa pale ikulu, kunahitaji mtu mgumu, sio laini laini, mwenye msuli wa kiukweli kweli, na sura ya ndimu, zile risasi 16, zimempitisha Lissu kwenye bonde la uvuli wa mauti na kumpika kwenye tanuru la moto, hivyo zimemfanya Lissu kuwa ni chuma cha pua!.

Chuma cha type hii ndio kinaweza kuingoa CCM ikulu.

Nasema nendeni na Lissu japo Lissu sio mkamilifu, hakuna mkamilifu, Lissu tatizo lake kubwa ni ropo ropo!, japo huo u ropo ropo wake ni a liability kwa wastaarabu na waungwana, huo uropo ropo wake ndio the biggest asset ya kuifurusha CCM Ikulu!, Japo Lowassa Alikuwa a Liability CCM, Akawa Asset Chadema. Lissu is a Very Bad Liability, but is The Only Asset Chadema Has Kuwangiza Ikulu!. Je... ?

Hivyo wana Chadema kama mnataka kugeuka chama cha siasa na kwenda ikulu, Lissu is the man to bank with, ila kama mnataka kuendelea na saccos yenu ya kupiga fedha za ruzuku, then endelezeni the status quo.

P
 
Una hoja aisee....japo wewe ni kada wa Ccm
 
Paskali katika ubora wake
 
Tuungane kumu wish Tundu Lissu all the best kesho.
YEYE atatenda!
Sema Amen!.

Ushindi wa Tundu Lissu kesho ni muhimu ili October, YEYE aonyeshe uwezo wake kwa kulifanya lile jiwe lililokataliwa na waashi, YEYE atalifanya kuwa jiwe kuu la pembeni!.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…