Vurugu za Bungeni: Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!.

Vurugu za Bungeni: Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!.

Lissu bado ni mgonjwa aliponea kimuijiza kifo , kufuatia shambulio la wasiojulikana la risasi 38, na 16 kati ya hizo zikampata,

Watanzania wote wanajua, bara zima la Africa wanajua, dunia inajua.
Kufuatia shambulio hilo alipaswa kutibiwa na ofisi ya Bunge, lakini hili halikufanyika, he was denied deserving treatment, mshahara wake ukasitishwa, na baada ya kutangaza kuwa amepona na kutoa tarehe ya kutua nyumbani, ndipo ikaamuliwa atimuliwe ubunge.
I think this is not fair, it's like adding an insult to an injury, kutia chumvi kwenye kidonda.
Mtu wa aina hii, amepitia mitihani na majaribu makubwa sana, hivyo alistahili kuvumiiwa, kustahiliwa na kuendelea kusuportiwa na sio kutimuliwa kazi.
P
Kuna sababu nyingi zilizosababisha bunge kumtelekeza ikiwa pamoja na yeye kukataa kufuata taratibu, hata hivyo baada ya kupona alitakiwa arudi bungeni. Badal yake akaanza kuzurula nchi mbali mbali, hivyo bunge halina kosa hapo.
 
Nina kovu la risasi na la upasuaji siyapendi kabisa mwilini mwangu...
Makovu ya moyoni dawa yake naijua.......
yanatibika, pia kuna ointments za kuondoa makovu superficial kama birthmarks, au stretch marks.
P
 
Kuna sababu nyingi zilizosababisha bunge kumtelekeza ikiwa pamoja na yeye kukataa kufuata taratibu, hata hivyo baada ya kupona alitakiwa arudi bungeni. Badal yake akaanza kuzurula nchi mbali mbali, hivyo bunge halina kosa hapo.
Kisheria, kikanuni na kiutaratibu, Bunge liko very right, lakini kiukweli morality, kiutu na kiu binadamu, this is very wrong, it's just like adding an insult to an injury.
Kutia chumvi kwenye kidonda.
P
 
Kisheria, kikanuni na kiutaratibu, Bunge liko very right, lakini kiukweli morality, kiutu na kiu binadamu, this is very wrong, it's just like adding an insult to an injury.
Kutia chumvi kwenye kidonda.
P
Bro nakuheshimu sana ila naomba tukubaliane tukokukubaliana.
 
Naibu Spika yeye alipata matokeo mazuri first degree,mbali na kuwa na kauwezo ka kawaida,pi kutokana na ka utaratibu ka pale mlimani ka waalimu kuwa na mtandao wa mtu wamtakaye,kama wakikutaka,basi anayehitaji wewe ufaulu atawasiliana na wenzie,kila mmoja atakutwanga "A" au "B+", utapata chansi ya LLM, kwa gharama za chuo,then PhD

Dk Tulia alibebwa na Mzee Mwandosya(prof) alimtengenezea network nzuri,akapata maksi nzuri, na akamuunganisha na watu sahihi kwa wakati sahihi
 
Leo ni Tundu Lissu day, ilikuwa arejee, leo, japo hakurejea, tunamuadhimisha kwa kumtafakari kwa sababu


Leo siku ya tarehe 7/Sept. 2019 ni siku ya kumbukumbu ya miaka miwili toka Mh.Tundu Lisu aliposhambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Mpaka leo bado wasiojulikana hawa bado hawatajulikana na uchunguzi mkubwa, makini na mkali wa Jeshi letu adilifu la polisi, unaendelea kuwabaini wasiojulikana hawa, hivi sasa kuna mashuhuda wawili muhimu sana, wanasubiriwa wao tuu kuhojiwa ndipo taarifa rasmi ya polisi kuhusu maendeleo ya uchunguzi huu ndipo ilatolewa.


Tuvute subra.

Get well soon Mhe. Tundu Lissu and welcome back home.

P
 
Mayalla, wewe na Lissu mnalingana?
Ona aibu mdogo wangu.
No mimi na Lissu, hatulingani, japo tulikuwa shule moja Ilboru, mimi nikiwa A level, Lissu alikuwa O-level hivyo kwa Lissu mimi ni Kaka yake, na yeye ni mdogo wangu.
Lissu ni kichwa mbaya, mimi ni mtu wa kawaida.
Nimeisha mzungumza sana Lissu humu jf.
P
 
"Sisi na vilaza wengine tukaishia kwenye vile vyuo vya mashenzini!. "-pascal mayalla

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Pasco bhana hahahahahah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,

Juzi katika kikao cha bunge, Spika wa Bunge, Mhe. Anne Maklnda, alimtaja Mbunge wa Singida, Mhe. Tundu kama ndie Mbunge anayeongoza kuwa chanzo cha vurugu za bungeni, kwa kuongoza kwa utovu wa nidhamu, kuleta fujo na vurugu mbalimbali za bungeni, hali ambayo sio tuu inahatarisha hali ya usalama, utulivu na amani bungeni, bali pia kumevuruga hadi baadhi ya ratiba za Bunge kulikopelekea Spika kufuta ratiba za Bunge ambazo zilikwisha ridhiwa na kuingizwa kwenye Order Paper ikiwemo kupokea hoja binafsi za wabunge, kwa kilichoelezwa kuepuka vurugu zaidi!.

Jana kikao cha kamati ya Uongozi kimekaa kujadili hali ya usalama Bungeni na matokeo yake, tutayapata kesho asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo kwa PM!, ni hakika rungu la kiti, lazima litamshukia Mhe. Tundu Lissu!.

Swali la kwanza ambalo wengi mtapenda kujiuliza ni, ni jee ni kweli, Mhe. Tundu ni mtundu na ndie chanzo cha utovu wote wa nidhamu wa bunge hili la kumi kama anavyoelezwa na Madam Speaker?!, au huo utundu wa Mhe. Tundu, sio utundu bali ni kusimamia haki na uzingatiaji wa kanuni za uendeshaji wa Bunge kwa haki, kufuatia Madam Speaker kuonyesha udhaifu mkubwa katika kuliendesha Bunge kwa kutokuzingatia, sheria, taratibu na Kanuni?!.

Kwa vile mimi ni mmoja wa watu tunaomfahamu vizuri Mhe. Tundu, tangu zamani tukiwa shuleni, Ilboru (sio darasa moja, mimi nikiwa A-level, yeye alikuwa O-Level) naomba kuchukua fursa hii kumfariji Mhe. Spika, kwa kumshauri na kumuomba asiumize sana kichwa chake kuendelea kubishana na Mhe. Tundu Lissu kuhusu kanuni za Bunge, ni kujipotezea tuu muda wake bure kwa kubishana na Lissu kwa kitu ambacho Lissu ana uhakika nacho 100/100!. Nashauri wala Bunge wasipoteze muda na kujisumbua kumuadhibu kwa jambo ambalo liko wazi kabisa watu wote wenye macho tunduizi tunaona wazi ni wapi udhaifu wa uendeshaji wa Bunge letu ulipo, sababu za udhaifu huo zinajulikana tangu chanzo chake, ulipo sasa na labda utaendelea kuwepo, hivyo hata Lissu akiadhibiwa vipi, kwa sababu Mhe. huyu ni mbishi hakuna mfano!, haswa pale anapokuwa na uhakika kuwa yuko right!.

Nashauri Mhe. Spika, lazima ufike mahali, umkubali huyu jamaa kuwa lile jina lake la Tundu, sio jina tuu la kupewa, bali huyu bwana analiishi jina lake kwa kuwa ni mtundu kikweli pale anapogundua kuwa kanuni zinakiukwa na zinapopindishwa ili kutoa mteremko kwa upande fulani!.

Nimebahatika kusoma na Mhe. Lissu shule moja kule Ilboru, (sio darasa moja) miaka hiyo enzi za mkuu mmoja wa shule aitwae Mwalimu Mushi, kwa jina la utani, Bino!. Huyu Bino alikuwa ni Mwalimu Mkuu bingwa wa nidhamu, ila kwa Tundu Lissu, alinyanyua mikono juu na kisha kuishusha chini, baada ya kuthibitika kuwa japo Tundu alikuwa "toto tundu", ila pia ndie aliyekuwa kipanga wa darasa lake!, kwani pepa alikuwa akizifumua, utadhani mtihani katunga yeye!.

Tundu Lissu alijiunga shule ya vipaji ya Ilboru akitokea Singida, wakati huo shuleni akiitwa Antipasi Tundu, na alikuwa ni mtoto mtundu kweli!. Wakati huo, O-Level ya Ilboru ilichukua wanafunz vichwa tupu wenyeji wa Arusha, Singida na Shinyanga!. Sisi Wasukuma tukiitwa "Wasukusu", wenyeji wakiitwa "wamenye" huku jamaa wa Singida wakijiita watu wa "Singapore", A-Level wakichukua vipanga wenye Div 1 kali, enzo hizo uji ukiitwa "sumu", na nje kulikuwa na kaduka kwa "Akwii".

Utundu wa Tundu Lissu ulkikuwa ni kwenye mishe mishe tuu hizi za zile, haijulikani alikuwa akisoma muda gani, ila pepa zikija, anafumua ile mbaya kama mitihani katunga yeye!, hivyo huyu jamaa ni very bright and na very intelligent.

Moja ya maeneo ambayo Tundu Lissu alikuwa ni mtundu au tusema ni mbishi, ni kwenye school debate!. Tundu Lissu alikuwa Bingwa wa school debate, akishakuwa na uhakika yuko right and on the right side and on the right track, ni mbishi hakuna mfano!.

Hata mimi nami sikuwa malaika, nilikuwa na matatizo yangu tangu shule, yale matatizo ya kawaida ya Wasukuma wa Chapa Ng'ombe, unapokutana bidhaa adimu za vibinti vya vyeupe vya Kiarusha pale Mlimani Ilboru, ukijumlisha na lile baridi kali la Ilboru , tena wakati huo, "bwawa bado halijaingia luba!'...

Tundu Lissu aliondoka Ilboru na Div. 1 ? kali ya point 7!, akaenda Galanos huko nako akafumua Div. 1 ya point 3!, na hatimaye kujiunga UDSM alikofumua upper 2nd Class (inasemekana alipata 1st class wakambania). Sisi na vilaza wengine tukaishia kwenye vile vyuo vya mashenzini!.

Tulipoteana kwa kipindi cha takriban miaka 10!, tulikuja kukutana tena jijini Atlanta, nchini Marekani, yeye akiwa na yake nami nikiwa na yangu, ndipo akanieleza sasa yuko LEAT, na huko aliichachafya serikali vivyo hivyo kama anavyo mchachafya Madame Spika, kwa kumsulubu bila huruma!.

Pamoja na utundu wote huu wa Mhe. Tundu Lissu, kiukweli kabisa this guy is dam good upstairs tangu academically akiwa shule na kwa kujenga hoja akiwa wakili na hadi sasa mule Bungeni.

Hivyo wakati tukisubiria kusikia ni adhabu gani itamfika Lissu hapo kesho, kuna maswali matatu tujiulize!.
  1. Jee ni kweli Mhe. Tundu Lissu ni mtundu kihivyo na ndie mbunge anayeongoza kwa utovu wa nidhamu hadi kustahili adhabu kali?.
  2. Au ni Spika ndiye Spika dhaifu hadi kushindwa kulisimamia Bunge kwa kanuni, kuliendesha Bunge kwa haki hivyo Tundu Lissu akisisitiza kufuatwa kwa kanuni, anaonekana kama analeta vurugu?.
  3. Baada ya kuthibitisha, Mhe. Tundu Lissu alikuwa ni mtundu toka shuleni, jee nani wa kubadilika kati ya Mhe Tundu Lissu na wabunge wa upinzani, yaani wakae kimya wakati sheria, taratibu na kanuni za Bunge, zikikiukwa, na kupindishwa?, hivyo kumpatia fursa Mhe. Spika kujiendeshea Bunge kwa kuliburuza atakavyo, ili tuu kudumisha utii, na nidhamu ili Bunge liwe la amani?, au wakuu wa Bunge ndio wabadilike baada ya kugundua limeingia wabunge makini wanaojua sheria na kanuni, hivyo huwezi kuwaburuza kibwege barge, hivyo mabadiliko na waliendeshe Bunge kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni kwa kutoa haki na usawa kwa wote, kwa vyama vyote, hivyo kupatikana kwa amani ya kweli ya kudumu.
  4. Hivyo Mhe Madam Spika kuwathibitishia Watanzania kuwa hata yeye, japo ni Spika wa majaribio ya "jinsia" "ameweza" kuliendesha Bunge vizuri tuu, ambalo ni mhimili mmoja wa dola, hivyo 2015, tunaweza kuendelea na majaribio ya "jinsia" kwa mihimili miwili iliyobakia?, ili nchi yetu iwe ni nchi ya usawa halisi wa kijinsia?.
Wasalaam

Paskali
(Skulu Meti wa Toto T).
Wanabodi, mimi nilidhani Lissu hatarejea
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, "Kwa Mliomsikia Tundu Lissu Kwenye Hard Talk, Jee Unadhani Atarejea Nchini?. Mimi kwa upande wangu, I seriously doubt kama atarejea, na ikitokea kweli akarejea, then Tundu Lissu atakuwa ni shujaa mwenye uthubutu na ushujaa mkubwa kuliko hata ushujaa wa Nelson Mandela!.

Nimesema hivyo kwa sababu nimemsiliza kwa makini Tundu Lissu, him being a Lawyer, kwa yale aliyoyasema, kwa tuhuma alizoshusha bila ushahidi, I seriously doubt if Tundu Lissu will ever return home during this era, na ikitokea kweli akarejea, then Tundu Lissu atakuwa ni shujaa kuliko Nelson Mandela.
Hongera zake.

Paskali
Final Update
Tundu Lissu leo amerejea nyumbani Tanzania, hivyo naomba kuthibitisha humu kuwa Tundu Lissu ni Jasiri na Shujaa Kuliko Nelson Mandela.

Hivyo sasa, kufuatia kurejea huku, ule ushauri wangu nilioutoa kwake kabla hajashambuliwa, sasa utekelezwe.

Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Shujaa Kamanda Tundu Lissu, karibu nyumbani.
Mungu ni mwema amekutendea muujiza, hivyo endelea kutimiza ndoto yako, Mungu aliyekuponya ni Mungu mwenye uwezo, anaweza kabisa kulifanya "Jiwe Walilolikataa Waashi, Likafanywa Jiwe Kuu la Pembeni"

I wish him all the best.
Paskali
 
Mkuu Mpango, Ilboru ile ilikuwa ya vipanga wa kutoka kwenye umande na sio hii ya sasa ya spoon fed vipanga toka academy!.

Leat ni Chama cha Wanasheria wa Mazingira, wamefight sana ushenzi uliofanywa Loliondo, Yaeda Chini, sumu za Barick kule mto Tigiti na ushenzi mwingine wote tunaofanyiwa kwa jina au la hifadhi, au uwekezaji!.

Kuhusu sisi Watanzania, ni watu watulivu, watu wa upendo na mshikamano, hivyo viongozi wetu wanatutake for granted, hata wakifanya chochote, sisi ni yes man!, kuna wakati sikumbuki ni nchi gani, mkate ulipanda bei by 20%, maandanano nchi nzima, waziri mkuu wa nchi hiyo aling'olewa!. Sisi mtu anakufa mikononi mwa polisi picha zinasema kila kitu na wote wametulia tuu as if nothing happened. 1976 nikiwa mdogo bado, Mzee wangu aliwajibishwa kwa ile kesi ya mauji Mwanza, kuanzia Waziri wa mambo ya ndani na wa usalama, walijiuzulu, IGP, Boss wa TISS, walistaafishwa!, RPC, RSO, OCD, DSO walipandishwa kizimbani!. Leo tangu ile ya Maandamano Arusha, mtu kapigwa risasi stend, polisi wakatengeneza a make belive video kuwa wamewaua watu waliokuja kuvamia kituo cha polisi!, ya Mwangosi ndio usiseme, no one amewajibika as if nothing happened nasi tunawashangilia na 2015, tunawapa term nyingine tena!.

Tatizo sio viongozi wetu, tatizo ni sisi Watanzania, sisi ni mandondocha kabisa!, hatuchagui viongozi kwa sifa kwa sababu hata JK tulipomchagua kwa ile landslide tulimchagua kwa sifa zipi?. Spika Anne aliletwa ili kumkomoa Six awekwe bench ili kutoa fursa ya kumsafisha EL na dodoki litapita 2014!. Eti sifa kuu ni "gender!". Nimeshazisikia fununu kuwa kwa vile kuna mafahali wanapigana vikumbo kuigombania magogoni, kuna sketi nyingine inaandaliwa, ili kumleta a compromised candidate chama kisimegeke!. Ndani ya CCM, 2015 ni zamu ya Zanzibar, Shein is the man!, ila wanahofia wasiitoe magogoni kwa sadakawe kwenye upepo wa M4C!.

Amini nakuambia jinsi tulivyo mandondocha, hiyo 2015, hata tukiletewa sketi nyingine, tutaichagua tuu!, na ni CCM tena!.

Pasco.

Hivi huyu Pascal Mayalla wa enzi hizo yuko wapi siku hizi..?

Au "bwawa ndiyo hivyo tena, lilishaingia luba" bhageshi...???
 
Wanabodi,

Kwa vile mimi ni mmoja wa watu tunaomfahamu vizuri Mhe. Tundu, tangu zamani tukiwa shuleni, Ilboru (sio darasa moja, mimi nikiwa A-level, yeye alikuwa O-Level) naomba kuchukua fursa hii kumfariji Mhe. Spika, kwa kumshauri na kumuomba asiumize sana kichwa chake kuendelea kubishana na Mhe. Tundu Lissu kuhusu kanuni za Bunge, ni kujipotezea tuu muda wake bure kwa kubishana na Lissu kwa kitu ambacho Lissu ana uhakika nacho 100/100!. Nashauri wala Bunge wasipoteze muda na kujisumbua kumuadhibu kwa jambo ambalo liko wazi kabisa watu wote wenye macho tunduizi tunaona wazi ni wapi udhaifu wa uendeshaji wa Bunge letu ulipo, sababu za udhaifu huo zinajulikana tangu chanzo chake, ulipo sasa na labda utaendelea kuwepo, hivyo hata Lissu akiadhibiwa vipi, kwa sababu Mhe. huyu ni mbishi hakuna mfano!, haswa pale anapokuwa na uhakika kuwa yuko right!.

Nashauri Mhe. Spika, lazima ufike mahali, umkubali huyu jamaa hivyo hivyo jinsi alivyo na lile jina lake la Tundu, sio jina tuu la kupewa, bali huyu bwana analiishi jina lake kwa kuwa ni mtundu kweli!, na haswa pale anapogundua kuwa katiba, sheria, taratibu na kanuni zinakiukwa na zinapopindishwa ili kufavour na kutoa mteremko kwa upande fulani mule Bungeni.

Wasalaam

Paskali
(Skulu Meti wa Toto T).
Dear School mate Tundu Lissu, najua umepitia makubwa. Welcome back home. Nakuomba sana upunguze kidogo kuliishi jina lako, usimsumbue huyu Mama kama ulivyomsumbuaga yule Madam, Mwenyekiti wako Mbowe tayari ameisha onyesha uungwana na ustaarabu mkubwa, wa hali ya juu@, please do the same!, tufanye siasa za kiungwana na kistaarabu. Kubebwa bebeka, ukipedwa pendeka, ukishikwa shikamana, ukiaminiwa jiaminishe!.
Yaliyopita si ndwele, samehe, tugange yajayo tusonge mbele!.
Welcome back home.
Your school mate
Pasco
 
Back
Top Bottom