Vurugu za Bungeni: Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!.

Vurugu za Bungeni: Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!.

Mhe. Tundu Lissu ndiye aliyetangaza kuvuliwa uanachama Zitto kwa mijibu wa kanuni batili, inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT!.

Hapa nafanya tafakuri tuu!.

Pasco
 
Mhe. Tundu Lissu ndiye aliyetangaza kuvuliwa uanachama Zitto kwa mijibu wa kanuni batili, inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT!.

Hapa nafanya tafakuri tuu!.

Pasco
Ni kanuni ipi inayokwenda kinyume na katiba yako mbovu hiyo? Tazama kina Singh Seth wanavyotuchezea kuweka mapingamizi mahakamani tusiujadili wizi wao! CDM haijawazuia wanachama wake kudai haki zao za kichama mahakamani, lakini wakifanya hivyo kwa hila kama alivyofanya kipenzi chako, na huko mahakamani wakabwagwa chini, hakuna jingine ispokuwa kuachana nao. Hakuna nafasi ya uhuni CDM, fanyeni uhuni hukohuko kwenu.

Unaonaje katiba yako ya jmt ingeiba hivyo vipengele kwenye katiba yetu tukuka walau kupambana na wajingawajinga kama kina mtemi Andrea!
 
Mhe. Tundu Lissu ndiye aliyetangaza kuvuliwa uanachama Zitto kwa mijibu wa kanuni batili, inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT!.

Hapa nafanya tafakuri tuu!.

Pasco

nenda mahakamani kama hujalizika na uamzi sio kujaza mandishi humu kila sehemu ni wewe tu!
 
Hiyo ndo cdm ukienda mahakaman jipange kweli kweli ukishindwa umekwenda na maji. Mtu Unajua kwennda mahakamn ni kuvunja katiba ya chama alaf unaenda kibwege ----- lazima upate stahiki yako
 
Wanabodi,

Juzi katika kikao cha bunge, Spika wa Bunge, Mhe. Anne Maklnda, alimtaja Mbunge wa Singida, Mhe. Tundu kama ndie Mbunge anayeongoza kwa kuwa chanzo cha vurugu za bungeni, kwa kuongoza kwa utovu wa nidhamu, kuleta fujo na vurugu bungeni, hali ambayo sio tuu inahatarisha hali ya utulivu, amani na usalama wa bungeni, bali pia kumepelekea Spika kufuta baadhi ya ratiba za bunge ambazo zilikwisha ridhiwa na kuingizwa kwenye order paper ikiwemo kupokea hoja binafsi za wabunge, kwa kilichoelezwa kuepuka vurugu zaidi.

Jana kikao cha kamati ya Uongozi kimekaa kujadili hali hiyo na matokeo yake, tutayapata kesho asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo kwa PM!, ni hakika rungu la kiti, lazima litamshukia Mhe. Tundu Lissu!.

Swali la kwanza ambalo wengi mtapenda kujiuliza ni, ni jee ni kweli, Mhe. Tundu ni mtundu na ndie chanzo cha utovu wote wa nidhamu wa bunge hili la kumi kama anavyoelezwa na Madam Speaker?!, au huo utundu wa Mhe. Tundu, sio utundu bali ni uzingatiaji wa kanuni za Bunge, kufuatia Mhe. Spika, kuonyesha udhaifu mkubwa katika kuliendesha bunge kwa kutokuzingatia, sheria, taratibu na Kanuni?!.

Kwa vile mimi ni mmoja wa watu tunaomfahamu Mhe. Tundu, Tangu toka akiwa Shuleni, Ilboru (sio darasa moja, Nikiwa A-level, yeye alikuwa O-Level) naomba kuchukua fursa hii kumshauri na kumfariji Mhe. Spika, kwa kumuomba asiumize sana kichwa chake kuendelea kubishana na Mheshimiwa Tundu Lissu kuhusu kanuni za bunge, au kitu ambacho Lissu ana uhakika nacho, wala wasipoteze muda kumuadhibu kwa jambo ambalo liko wazi kabisa na udhaifu unajulikana tangu chanzo chake, ulipo na labda utaendelea kuwepo, hata akiadhibiwa vipi, kwa sababu Mhe. huyu ni mbishi hakuna mfano!, haswa pale anapokuwa na uhakika kuwa yuko right!.

Nashauri Mhe. Spika, lazima ufike mahali, umkubali huyu jamaa kuwa lile jina lake la Tundu, sio jina tuu, huyu bwana analiishi jina lake kwa kuwa ni mtundu kikweli pale anapogundua kuwa kanuni zinapopindishwa ili kutoa mteremko kwa upande fulani!.

Nimebahatika kusoma na Mhe. Lissu shule kule Ilboru, (sio darasa moja) miaka hiyo enzi za Mkuu mmoja aitwae Bino!. Huyu Bino alikuwa ni mwalimu mkuu bingwa wa nidhamu, ila kwa Tundu, alinyanyua mikono juu na kwisha kuishusha juu baada ya kuthibitika kuwa japo Tundu alikuwa "toto tundu", ila pia ndie aliyekuwa kipanga wa darasa lake!, kwani pepa alikuwa akizifumua, utadhani mtihani katunga yeye!.

Tundu Lissu alijiunga shule ya vipanga ya Ilboru akitokea Singida, wakati huo akiitwa Antipasi Tundu, na alikuwa ni mtoto mtundu kweli!. Wakati huo, Ilboru ilichukua wanafunzi wenyeji wa Arusha, Singida na Shinyanga!. Sisi Wasukuma tukiitwa "Wasukusu", wenyeji wakiitwa "wamenye" huku jamaa wa Singida wakijiita watu wa "Singapore", uji ukiitwa "sumu", na nje kulikuwa na duka la kwa "Akwii".

Utundu wa Tundu Lissu ulkikuwa ni kwenye mishe mishe tuu hizi za zile, haijulikani alikuwa akisoma saa ngapi, ila pepa zikija, anafumua ile mbaya!. Moja ya maeneo ambayo jamaa alikuwa ni ni mtundu au tusema ni mbishi, ni kwenye school debate!. Jamaa akishakuwa na uhakika yuko on the right track, ni mbishi hakuna mfano!. Hata nami nilikuwa na matatizo yangu tangu shule, yale matatizo ya kawaida ya Chapa Ng'ombe, unapokutana na vibinti vya Vyeupe vya Kiarusha pale Mlimani Ilboru, ukijumlisha na lilke baridi la kule, tena wakati huo, "bwawa halijaingia luba!'...

Tundu lissu aliondoka na wani kali, akaenda Galanos hatimaye UDSM. Sisi vilaza wengine tukaishia vile vyuo vya mashenzini!. Tulipoteana kwa kipindi cha miaka 10!, tulikuja kukutana tena mjini Atlanta, yeye akiwa na yeke nami na yangu, ndipo akanieleza yuko LEAT, na huko aliichachafya serikali vivyo hivyo kama anavyo mchachafya Madame Spika, kwa kumsubu bila huruma!.

Pamoja na utundu wote huu wa Mhe. Tundu Lissu, wakati tukisubiria kusikia ni adhabu gani itamfika hapo kesho, kuna maswali matatu tujiulize!.
  1. Jee ni kweli Mhe. Tundu Lissu ni mtundu kihivyo na ndio anayeongoza kwa utovu wa nidhamu hadi kustahili adhabu kali?.
  2. Au ni Spika ndiye dhaifu hadi kushindwa kumdhibiti Tundu Lissu na utundu wake?.
  3. Baada ya kuthibitisha, Mhe. Tundu Lissu alikuwa ni mtundu toka shuleni, jee nani wa kubadilika kati ya Mhe Tundu Lissu na wabunge wa upinzani, wakae kimya wakati sheria, taratibu na kanuni, zikikiukwa, na kupindishwa?, hivyo kumpatia fursa Mhe. Spika kujiendeshea bunge anavyotaka, ili kudumisha utii, na nidhamu, bunge liwe la amani?.
  4. Hivyo Mhe Spika kuwathibitishia Watanzania kuwa hata yeye ambaye ni Spika wa majaribio ya "jinsia" "ameweza" kuliendesha bunge vizuri tuu, ambalo ni mhimili mmoja wa dola, hivyo jee, 2015, tukamilishe majaribio ya "jinsia" kwa mihimili miwili iliyobakia?, ili nchi yetu iwe ni nchi ya usawa halisi wa kijinsia?.

Wasalaam

Paskali
(Skulu Meti wa Toto T).
Baada ya toto tundu Tundu Lissu kuchaguliwa rais wa TLS, sasa ni zamu ya Rais wetu Magufuli na waziri wake Mwakyembe kuusikilizia muziki wake!. Kichaa kapewa rungu na kibali cha kuua nzi! . Ataponda mtu kichwa kwa excuse ya kuua nzi.

Hongera Tundu Lisu kuwa rais wa TLS! .

Paskali
 
Baada ya toto tundu Tundu Lissu kuchaguliwa rais wa TLS, sasa ni zamu ya Rais wetu Magufuli na waziri wake Mwakyembe kuusikilizia muziki wake!. Kichaa kapewa rungu na kibali cha kuua nzi! . Ataponda mtu kichwa kwa excuse ya kuua nzi.

Hongera Tundu Lisu kuwa rais wa TLS! .

Paskali
Nimecheka kama mazuri
 
Mkuu Mpango, Ilboru ile ilikuwa ya vipanga wa kutoka kwenye umande na sio hii ya sasa ya spoon fed vipanga toka academy!.

Leat ni Chama cha Wanasheria wa Mazingira, wamefight sana ushenzi uliofanywa Loliondo, Yaeda Chini, sumu za Barick kule mto Tigiti na ushenzi mwingine wote tunaofanyiwa kwa jina au la hifadhi, au uwekezaji!.

Kuhusu sisi Watanzania, ni watu watulivu, watu wa upendo na mshikamano, hivyo viongozi wetu wanatutake for granted, hata wakifanya chochote, sisi ni yes man!, kuna wakati sikumbuki ni nchi gani, mkate ulipanda bei by 20%, maandanano nchi nzima, waziri mkuu wa nchi hiyo aling'olewa!. Sisi mtu anakufa mikononi mwa polisi picha zinasema kila kitu na wote wametulia tuu as if nothing happened. 1976 nikiwa mdogo bado, Mzee wangu aliwajibishwa kwa ile kesi ya mauji Mwanza, kuanzia Waziri wa mambo ya ndani na wa usalama, walijiuzulu, IGP, Boss wa TISS, walistaafishwa!, RPC, RSO, OCD, DSO walipandishwa kizimbani!. Leo tangu ile ya Maandamano Arusha, mtu kapigwa risasi stend, polisi wakatengeneza a make belive video kuwa wamewaua watu waliokuja kuvamia kituo cha polisi!, ya Mwangosi ndio usiseme, no one amewajibika as if nothing happened nasi tunawashangilia na 2015, tunawapa term nyingine tena!.

Tatizo sio viongozi wetu, tatizo ni sisi Watanzania, sisi ni mandondocha kabisa!, hatuchagui viongozi kwa sifa kwa sababu hata JK tulipomchagua kwa ile landslide tulimchagua kwa sifa zipi?. Spika Anne aliletwa ili kumkomoa Six awekwe bench ili kutoa fursa ya kumsafisha EL na dodoki litapita 2014!. Eti sifa kuu ni "gender!". Nimeshazisikia fununu kuwa kwa vile kuna mafahali wanapigana vikumbo kuigombania magogoni, kuna sketi nyingine inaandaliwa, ili kumleta a compromised candidate chama kisimegeke!. Ndani ya CCM, 2015 ni zamu ya Zanzibar, Shein is the man!, ila wanahofia wasiitoe magogoni kwa sadakawe kwenye upepo wa M4C!.

Amini nakuambia jinsi tulivyo mandondocha, hiyo 2015, hata tukiletewa sketi nyingine, tutaichagua tuu!, na ni CCM tena!.

Pasco.
.....
......Pasco siyo Pasikali hapo kwenye LEAT umenikumbusha mbali
 
Baada ya toto tundu Tundu Lissu kuchaguliwa rais wa TLS, sasa ni zamu ya Rais wetu Magufuli na waziri wake Mwakyembe kuusikilizia muziki wake!. Kichaa kapewa rungu na kibali cha kuua nzi! . Ataponda mtu kichwa kwa excuse ya kuua nzi.

Hongera Tundu Lisu kuwa rais wa TLS! .

Paskali
Mkuu umeamua kuji quote mwenyewe?
 
Pascal Mayalla ukiangalia thread zako zote ulikuwa unampobda lisu lakini Mr Lissu sasa. Ni Raid unanza kujipendekeza pesa ulizopewa kusafisha njia ya KOLOMIJE umeshindwa.

Mayalla kwetu no Njaa.


Swissme
 
Mhe. Tundu Lissu ndiye aliyetangaza kuvuliwa uanachama Zitto kwa mijibu wa kanuni batili, inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT!.

Hapa nafanya tafakuri tuu!.

Pasco
Pascal anapokua mtoto
29a1be2228db2ee17ca072bf177e778b.jpg
 
Back
Top Bottom