Vurugu za Bungeni: Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!.

Hivi katika hao wote waliosoma "spesho" skulz kuna hata mmoja aliyevumbua chochote?

Na kwa chochote namaanisha kitu au kanuni yoyote ile katika jambo lolote lile?

Yes, kanuni ya kumpelekesha Makinda na Ndugai hadi wanapoteza mwelekeo kabisa na kuahirisha kikao cha bunge, siku mbili mfululizo! Seminal, 100% Tanzanian!
 
Nahisi kizungu zungu hapa, mwaka 1961 palikuwepo na mfumo wa elimu wa form one? khaaaaa! Nisaidieni muliokula chumvi nyingi mkuu Mag3

Kwahiyo unataka kutuambia kwamba miaka hiyo ya mkoloni hakukuwa na shule za sekondari siyo?? yani wewe hata hujiulizi mwalimu Nyerere pamoja na wasomi wengine wa enzi za ukoloni waliwezaje kufika vyuo vikuu kama hakukuwa na Sekondari??
 
Kwahiyo unataka kutuambia kwamba miaka hiyo ya mkoloni hakukuwa na shule za sekondari siyo?? yani wewe hata hujiulizi mwalimu Nyerere pamoja na wasomi wengine wa enzi za ukoloni waliwezaje kufika vyuo vikuu kama hakukuwa na Sekondari??

mkuu Mwita Maranya, naomba unifafanulie tu ndugu yangu nijue mfumo mzima wa elimu enzi hizo kabla ya uhuru/enzi za ukoloni kuanzia primary hadi chuo kikuu kusomea diploma/degree ! Najua wasomi walikuwepo na wataendelea kuwepo we nitoe tu kizungu zungu mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Unatumia vigezo gani kufikia hilo hitimisho?

Naomba unisaidie ili nikuelewe vizuri!

Dark City hauamini kama karne hii bado watu wanahongwa tshirt,kanga,sh 5000,na kula pilau na soda wanacheza kwamba hakuna kama fulani simply amehongwa vitu ambavyo baada ya muda mfupi havitumiki tena lakini amempa mtu ulaji wa miaka 5,bado sana na inatakiwa kazi ya ziada Watanzania wengi ni short sighted hawaangalii keshp kitatokea nini wao wanaangalia saa hivi wana nini,poor TANZANIAN
 

Mkuu PASCO naomba kunukuu baadhi ya maneno katika thread yako ambayo naona ndiyo chanzo cha matatizo yote haya:
  1. Spika ndiye dhaifu
  2. Spika kujiendeshea bunge anavyotaka
  3. Bunge lina "Spika wa majaribio ya jinsia"
  4. Taratibu na kanuni, zinakiukwa, na kupindishwa
 
Je Makinda naye ni Kinda bado katika uendeshaji wa shughuli za Bunge ?

siyo yeye tu ni makinda na makinda yake ya ccm bado ni makinda katika upeo wao hata wa kutambua kuwa watanzania siku hizi wamekuwa waelewa na wanajua nani mkweli na nani longolongo.
hoja zilizoletwa bungeni na ccm na upinzani ukizipima tu huhitaji elimu ya chuo kikuu kutambua ipi muhimu kwa maslahi ya taifa.
 
Tundu mbele ya Kinda nani zaidi? hakika kauli ya Jk inajidhihirisha waziwazi.
 
Mkuu Pasco,kwa hiyo kwa sasa mama Anna pale bungeni analea dogo TUNDU na dogo JANJA?
 


Ng'wanamapalala

Du, Watanzania gani tena hao pot? Madame Speaker ndiyo Watanzania?
 
Dhulma ya madame speaker na naibu wake ndiyo chanzo kikubwa cha vurugu bungeni, Leo hadi Shibuda amewaonya kwa jinsi walivyo chemsha! I wish wampe adhabu ili waonje ladha ghadhabu hasira za watanzania...
 
Ng'wanamapalala

Du, Watanzania gani tena hao pot? Madame Speaker ndiyo Watanzania?

Mkuu,
Nilichofanya hapa ni kuwa na balanced opinion. Tukubali kuwa pale mjadala unapohamia katika jamii basi lazima kutakuwepo na contradicting remarks.

Ninafikiri hata wewe unafahamu kama kuna watu ambao mtazamo wao utakuwa upande wa Mh. Makinda na huku wengine wakiwa upande wa Mh. Lissu.

Nashindwa kuelewa kwa nini unaona kama sikumtendea haki Mh. Lissu wakati hata mtendaji mkuu wa chama (Dr. Slaa)aligusia kwenye press conference na kusema yeye anapingana na mbinu iliyotumika kukabiliana na machafuko bungeni ambapo bunge liliahirishwa badala ya kuwa susppended kwa muda tu mpaka pale hali ya amani itakapo rejea ili kikao kiendelee.

Anyway, hili ni wazo langu tu na tukubali kutokubaliana.
 
I didn't ask you, did I?

Uko kwenye mjadala jamvini. Watu wsnajadili mambo mazito. katikati unauliza idadi ya wajukuu. just say what does it have to do with the discussion. stop trivializing serious deliberations.
 
Uko kwenye mjadala jamvini. Watu wsnajadili mambo mazito. katikati unauliza idadi ya wajukuu. just say what does it have to do with the discussion. stop trivializing serious deliberations.

You can't tell me what to do.
 
Makinda anaidhurumu nafsi yake na naamini inamsuta kwa kutetea mafisadi wakubwa, anapindisha sheria wazwaz hata mtoto wa shule ya msingi ataligundua hilo bila kuambiwa, LISSU ni jembe sana na anajua analofanya na hua yupo makini sana , wakimpa adhabu itawatokea puani, kwanza sakata hilo naamini lishawamaliza jijini dar es salaam sasa wakiendelea kurikoroga ndo wanajimaliza kabisaa, all in all lets wait nguvu ya umma inaelekea kushinda 2015 utakua mwanzo wa siasa mpya za tanzania!!
 
Unatumia vigezo gani kufikia hilo hitimisho?

Naomba unisaidie ili nikuelewe vizuri!
Mkuu Dark City,
nimeripoti chaguzi 4, hivyo ya 2015 itakuwa ni uchaguzi wa tano kuuripoti. CCM siku zote inashinda sio kwa sababu inapendwa sana, bali kwa mazoea tuu!, nimeisha andika makala zangu mbalimbali kwa nini 2015 ni CCM tena. Chadema itavuna wabunge wengi zaidi huku bara, CUF itapoteza baadhi ya majimbo. Mshindi wa jumla wa urais ataendela kuwa CCM!.

Chadema inayo nafasi ya kushinda kama itakubali "to do things right", kwa sasa kupitia M4C, Chadema, inafanya kazi nzuri, yaani "is doing the right thing!". Ili chapa kipya kiweze kuking'oa "chama kubwa", "chama kongwe", na kuingia Ikulu, "doing the right thing" peke yake hakutoshi!, it got to do "things right", kitu ambacho sikioni Chadema kufanya!, as a result watu wataendeleza mazoea!.

Zile umati za watu kwenye maandamano au kwenye mikutano, sio kura!, nimeisha waambia Chadema humu kwa nini hawatashinda urais 2015 na nini cha kufanya, lakini nimeishia kutukanwa tuu "wee gamba!", mimi nasisitiza kuendelea kusema ukweli no matter what. Let them call me what they may, ila ikifika 2015 mtayaono na baada ya hapo tutaanza kuelewana vizuri!.

Siasa ni kama barabara ndefu, mbovu na ya kona kona, milima, mabonde, mashimo na makorongo!, vyama ni kama magari, wanachama ndio abiria, na viongozi wa vyama ndio madereva!. Kuelekea 2015 ndio safari yenyewe. Kwa huku bara, mchuano ni kati ya CCM, (gari kongwe, injini kongwe chovu, lakini dereva mzoefu, aliyeisha izoea hiyo barabara, miaka nenda, miaka rudi, hivyo anajua aendesheje, wapi apunguze mwendo na wapi aende kasi, wapi kuna korongo wapi kuna bonde, wapi kuna konakali na wapi kuna mlima, etc,etc!) na Chadema (gari mpya na injini bomba ina nguvu kupita gari kongwe na inakwenda mbio kuliko ule mkweche ila ina dereva mpya ambaye hajui njia!, kazi ya dereva mpya ni kutimua mbio, na kuendesha kwa kasi ili awahi kufika!, kutokana na kutojua njia, japo anakwenda kasi zaidi, kwa kuipita gari kongwe kwa mbali, mara kibao hujikuta anapotea njia, hivyo kulazimika kurudi nyuma na kuendelea na safari!.

Kwenye hii scenario, huyu dereva mpya anayo nafasi ya kushinda, sio kwa kitimua mi mbio, bali endapo atakubali au kuwasikiliza baadhi ya abiria wake wazoefu ambao wameishaipita njio hiyo mara nyingi ndani ya ule mkweche, au kutusikiliza sisi watazamaji wa mchuono huo ambao sio abiria wa gari yoyote, ila tuko homo njiani kwa muda mrefu, tunapoona dereva mpya anakosea, huwa tunampungia ishara kuwa huko siko!, au kumpa ishara ya hatari ya mbele, lakini hasikilizi!. Yeye ni mwendo kasi wa mbio tuu huku akishangiliwa na umati wa abiria wake, kuwa aendeleze "mwendo mdundo!.

Safari ya kuelekea 2015 ndio hii inaendelea, sasa hivi tuko half way!, bado hakuna dalili za dereva mpya kujifunza, hebu tusubiri, nasikia kutafanyika zoezi la kubadilishana madereva baadae mwaka huu, hebu na tusubirie timu mpya tuone, hata ikirudi timu ile ile kama itaendelkeza uendeshaji ule ule, basi ni hakika bila mashaka yote, mshindi ataendelea kuwa yule yule, dereva bingwa mwenye ule mkweche!.

Pasco.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…