Mkuu Mpango, Ilboru ile ilikuwa ya vipanga wa kutoka kwenye umande na sio hii ya sasa ya spoon fed vipanga toka academy!.
Leat ni Chama cha Wanasheria wa Mazingira, wamefight sana ushenzi uliofanywa Loliondo, Yaeda Chini, sumu za Barick kule mto Tigiti na ushenzi mwingine wote tunaofanyiwa kwa jina au la hifadhi, au uwekezaji!.
Kuhusu sisi Watanzania, ni watu watulivu, watu wa upendo na mshikamano, hivyo viongozi wetu wanatutake for granted, hata wakifanya chochote, sisi ni yes man!, kuna wakati sikumbuki ni nchi gani, mkate ulipanda bei by 20%, maandanano nchi nzima, waziri mkuu wa nchi hiyo aling'olewa!. Sisi mtu anakufa mikononi mwa polisi picha zinasema kila kitu na wote wametulia tuu as if nothing happened. 1976 nikiwa mdogo bado, Mzee wangu aliwajibishwa kwa ile kesi ya mauji Mwanza, kuanzia Waziri wa mambo ya ndani na wa usalama, walijiuzulu, IGP, Boss wa TISS, walistaafishwa!, RPC, RSO, OCD, DSO walipandishwa kizimbani!. Leo tangu ile ya Maandamano Arusha, mtu kapigwa risasi stend, polisi wakatengeneza a make belive video kuwa wamewaua watu waliokuja kuvamia kituo cha polisi!, ya Mwangosi ndio usiseme, no one amewajibika as if nothing happened nasi tunawashangilia na 2015, tunawapa term nyingine tena!.
Tatizo sio viongozi wetu, tatizo ni sisi Watanzania, sisi ni mandondocha kabisa!, hatuchagui viongozi kwa sifa kwa sababu hata JK tulipomchagua kwa ile landslide tulimchagua kwa sifa zipi?. Spika Anne aliletwa ili kumkomoa Six awekwe bench ili kutoa fursa ya kumsafisha EL na dodoki litapita 2014!. Eti sifa kuu ni "gender!". Nimeshazisikia fununu kuwa kwa vile kuna mafahali wanapigana vikumbo kuigombania magogoni, kuna sketi nyingine inaandaliwa, ili kumleta a compromised candidate chama kisimegeke!. Ndani ya CCM, 2015 ni zamu ya Zanzibar, Shein is the man!, ila wanahofia wasiitoe magogoni kwa sadakawe kwenye upepo wa M4C!.
Amini nakuambia jinsi tulivyo mandondocha, hiyo 2015, hata tukiletewa sketi nyingine, tutaichagua tuu!, na ni CCM tena!.
Pasco.