Jamani eh, kwani hatuwezi kuzungumzia mambo mengine +ve? Siyo fresh kila kukicha kuzumgumzia masuala ya Wakristo/Waislaam as if kuna ushindani wa aina fulani vile, kati ya dini hizi mbili!!
Wengi wetu tume bahatika kumesoma shule za Sekondary za Serikali, tulikuwa mchanganyiko wa karibu dini zote, religious sect was not an issue per se, masuala ya dini yalikuwa yamepangiwa kipindi maalumu kwenye time table, tuna attend once per week kila mwanafunzi anakwenda kwenye sect yake basi.
Hivi Watanzania wenzangu tumeingiliwa nini??? Inakuwaje matukio ya kawaida ya shuleni yanajengewa hisia za KIDINI hata kama kuna malalamiko ya kweli yanayo hitaji ufumbuzi wa kawaida tu, unakuta yanakuzwa out of proportion kwa kujaribu kumtafuta MCHAWI!! i.e mtu wa kulahumu.
Mbona atuzungumzii wapagani!!! Kwani wao siyo RAIA wa nchi hii??