Huo ungwana wenu mbona huwa hamzingatii wakati mnawachinja na kuwala albino, ni taifa gani dunia yote zaidi ya Tanzania linalofahamika kwa mauaji ya hao maskini walemavu wa ngozi, tatizo huwa mna unafiki mkubwa sana. Kuna baadhi yetu tunawafahamu nyie jinsi mlivyo hadi ndani.
Kitu ambacho huwa nafurahishwa na mleta mada, yeye hudhihirisha Utanzania halisi uliojificha wa roho zenu nyeusi bila unafiki. Mara nyingi unakuta Watanzania mna hulka ya kuamkuana na kuitana wakuu lakini ndani ya roho zenu mna majungu na machungu kupitiliza. Ni kawaida Mtanzania kukuchangamkia kwa salamu nyingi na vijimaneno, lakini ukiondoka tu, anaanza kuporomosha majungu dhidi yako.
Hivyo muache kupoteza muda eti mnamrekebisha mleta mada, yeye alishafanya maamuzi ya kutoishi kinafiki kama mlivyo, huwa anadhihirisha chuki zake zote na kuziweka wazi bila kumunya maneno wala kuremba.