VVU na UKIMWI: Historia yeke, chanzo cha maambukizi, dalili, kinga na juhudi za kupambana na ugonjwa huu


Maswali yako unachanganya sana...

Swali la 1. Hakuna ukweli wowote juu ya defect kwenye watu wa makundi tajwa. Kinachozungumzwa ni ukosefu wa aina ya protein zinazoitwa CCRK5 kwenye seli za damu. Na hizi ziko kwenye seli nyeupe na wala sio seli nyekundu. Hivyo mtu mwenye group lolote la damu
Pili hakuna carrier katika maambukizi ya VVU. Watu wanaosemwa carrier huwa ni long term progresser ambao huchukua mpaka miaka 18 kuugua. Ni idadi ndogo. It's either unapata maambukizi au hupati hakuna carrier kwenye HIV

2. Hapana hawezi kwenda kuambukiza mtu mwingine
 
1.Mkuu inasemekana virus wanaishi ndani ya seli nyeupe tu? Ni kweli?
2.kama ni kweli vp kwenye mate,na fluid zingne ikoje?
3.mtu anayetumia ARV tunaiman anazuia virus wasizaliane na kama wako kwenye cell watabaki humo siyo? Na cell zina mda wake wakuishi ,je cell hiyo inavokufa na wao hufa na cell au ?
 
1.Ndani ya seli nyeupe za damu wanazaliana. Lakini wanaweza kuishi katika seli nyinginemfano kwenye ubongo ambao wanakuwa wamefubaa
2.Seli nyeupe za damu kazi yake ni ulinzi zinaweza kwenda sehemu yoyote ya mwili
3. Seli ikifa virusi huama na kuambukiza seli nyingine
 
Mteja /Mtu anapogundulika ni HIV+... Ni vipimo gani kwa sasa ambavyo huwa anatakiwa kufanya na kwa interval ipi kama vile kwa ajili ya Monitoring ya CD4, kucheki wingi wa virusi, athari za dawa kwa mgonjwa kwenye figo na ini..... Nawaza tuu...
Bila shaka unaujuzi ila unamuuliza kwa kumpima kama ni mjuzi kweli simple tu maswali yako ni yakitabibu kama si mtu mchukua dozi tafadhari
 
Sasa kama wanakaa kwenye damu kwa nini upime mate!.. huyo bwana is empty kana can
Mkuu ilinibidi nichimbe kidogo uko sawa kabisa.....

Kwenye post yangu no 99 nimeelezea maelezo niliopewa na Doctor mmoja wa CTC kumbe nae alikua chaka kidogo.....

Shukran mkuu leo nmepata jambo jipya na muhimu kwa ajili yangu na wale wanaonizunguka....!
 
Ni kweli ana uelewa na maswali ya HIV. Ni mtoa huduma za HIV. Ndio maana maswali yake yamebase kwenye guideline ya taifa.
Nimeyafatilia maswali yake yote ila anauliza si kwa kutaka kujua bali kutaka kupima uwezo wa mtu si mbaya utu uzima dawa mjibu kwa hekima kuu naamini atatoka berenge mwenyewe usikute wew ndio mkuu wake wakazi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Asante mkuu . Sasa kuhusu pep mtu akipewa husemekana inazuia replication ya virus ? (Kama nmekosea naomba unisahihishe)kwahiyo wanaweza kubaki kwa no. Walioingia wakabaki hiyo hiyo ? &
 
HIV-AIDS,ni ugonjwa ambao una mambo kama ya kishetani,fallacy nk. Iweje mbu asiambukize HIV? Ukiangalia dalili za awali za HIV utaona ni dalili pia za magonjwa mengine mengi tu yanapotaka kumuingia mtu(yeyote hata kama hana HIV),hivyo kuleta mkanganyiko. Kwamba unaweza kuwa na dalili alizozitaja mtaalam(Papa Mobimba) hapo lakini kumbe siyo HIV.
Kwamba vipimo vingi vya HIV siyo kama vya vimelea vingine kama malaria,bali ni kucheki anti bodies. Jambo hilo liliwahi kupingwa vikali na baadhi ya madaktari hasa wa huko nje(video za Youtube zipo), kwamba kama ni mambo ya antibodies au upungufu wa kinga,hata watu wanaougua maginjwa sugu yasiyoambukizwa,ama anti bodies au tuseme kinga hushuka na hivyo vipimo INAWEZEKANA vikaonyesha ni POSITIVE. Sasa kwa kweli kuhusu HIV kuna nadharia nyingi sana.
Yote kwa yote huo ugonjwa upo,lakini una mambo mengi sana yaliyojificha. Kwa mfano hadi sasa haijulikani huo ugonjwa kweli ni wa vimelea vya asili au kuna wauaji walipandikiza vimelea maabara( sawa na biological,Chemical Weapons& War)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…