VVU na UKIMWI: Historia yeke, chanzo cha maambukizi, dalili, kinga na juhudi za kupambana na ugonjwa huu

VVU na UKIMWI: Historia yeke, chanzo cha maambukizi, dalili, kinga na juhudi za kupambana na ugonjwa huu

Mimi nadhani ifike mahali tuache kupokea vitu vingi hasa jamii ya chanjo na chakula kutoka Kwa wazungu mana sio wote wanaotupenda Leo ukimwi kesho utasikia wameleta dawa wanaume tusizaliane.

Kesho kutwa watakuja na lingine Ila kwakuwa tumezoea kupewa hatutaweza kuacha misaada ya Ajabu na hovyo eti mzungu anatuletea biscuit na peremende kama walivyofanya kule Zanzibar ambapo watoto wakila wanazimia na hivi vitu madhara yake tutakuja kuyaona baadae Sana Kwa ujinga na uzembe wa wizara ya afya
 
Kiwango cha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kitaifa kimeshuka kutoka asilimia 7 mwaka 2003/04 hadi kufikia asilimia 4.7 mwaka 2016/17 huku maambukizi kwa wanaume ikiwa ni asilimia 3.4 na wanawake ni asilimia 6.3.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mpango wa taifa wa kudhibiti Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI), ya mwaka 2018/19 kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI jijini Dodoma.

Amesema kiwango hicho cha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kimeonekana kushuka kufuatia utafiti wa hali ya maambukizi nchini na kudai kuwa Wizara kupitia NACP inatekeleza mpango mkakati wa nne wa VVU na UKIMWI ambao unalenga kutekeleza malengo ya dunia ya 90 tatu (90 90 90).

“Mpango huu wa mkakati wa nne wa VVU na UKIMWI utatekeleza mpango wenye mwelekeo wa kupambana na ugonjwa wa Upungufu wa Kinga Mwilini yaani UKIMWI na unapaswa kufikiwa ifikapo mwaka 2020, “ ameongeza Dkt. Chaula.

Amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi Juni, 2019 Serikali kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi imetekeleza hatua mbalimbali kwa lengo la kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030.

Dkt. Chaula amesema hatua hizo ni pamoja na huduma za ushauri nasaha na upimaji, huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU na huduma za upimaji wa wingi wa VVU mwilini.

“Huduma zingine ni za tohara ya kitabibu kwa wanaume, huduma za kondomu, huduma za VVU na UKIMWI kwa makundi maalum na huduma za Habari, Elimu na mawasiliano ya kubadili tabia,” amefafanua Dkt. Chaula.

Chanzo: Dar24
 
bila shaka baadhi ya waathirika wamekufa ndio maana imeshuka
 
Mkuu bora serikali ingeongeza kiwango cha maambukizi ili Watanzania waogope kuliko kushusha.Sasa hivi ukiwa hauzungumzwi kama ugonjwa hatari ila binafsi naamini maambukizi ni makubwa sana kuna watu ukiuzungumzia ukimwi wanachukia
 
Maambuki yamepungua kwasababu tumegoma kwenda kupima. Hasa wanaume ndo mana hata kitakwimu hapo asilimia ya maambukizi kwa wanaume ipo chini.
 
Zile za kukataa kwenda kujiandikisha kupiga kura zilitokana na zile za kukataa kwenda kupima, ndio maana maambukizi yamepungua kwa sababu hatuendi kupima, na kupima kila mara ni ishara kuna kitu mtu anakitafuta.
Mtu hana gari, hana nyumba, hana mifwedha ya nini kupima!!!
 
miss zomboko,


Hawa watafiti wanatuchanganya, wakiona fedha imekwisha wansema hali ni mbaya kiwango cha maambukizi kipo juu, fedha ikipatikana wanasema kiwango kimeshuka na hapo hawaendi kwenye tafiti
 
Wakiishiwa pesa watafanya pinduapindua watasema maambukizi ni 7.4
 
Ivi kwani Huwa inachukua mda gani minimum and maximum mtu aliye pata ukimwi kuona dalili za ugonjwa huo?...
 
Back
Top Bottom