Duh! Ila hiyo avatar na jina ni balaa. Avator ni jini, na hilo jina vipi mkuuAaaaaamen!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh! Ila hiyo avatar na jina ni balaa. Avator ni jini, na hilo jina vipi mkuuAaaaaamen!
Kitongoji cha Pabaya, Kijiji cha Nyibhoko, Kata ya Kisaka, Tarafa ya Ngoreme, Wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara, Shit-hole. BadBoy anakula nguruwe hadi jini atatorokea Misri kutafuta hifadhiDuh! Ila hiyo avatar na jina ni balaa. Avator ni jini, na hilo jina vipi mkuu
Nje ya tiba pia ni nyama TAMU SANA.Nguruwe analiwa kama dawa.ukikutana na MTU yeyote mwenye majini mwambie ale kitimoto yatafunga virago yenyewe.Wachaga wanakula sana kitimoto ndio maana hufanikiwa kibiashara biashara zao hazilogeki hata wafungue maeneo ya wafuga mjini.Majini ukisoma Biblia yalikuwa kwa mgerasi yesu akayaamuru yawaingie nguruwe kwa kuwa alijua nguruwe ni kiboko cha majini na wanajua namna ya kuyashughulikia.Nguruwe wakabeba Yale majini wakaenda kuyamwaga baharini.Kula kitimoto kama unataka uogopwe na majini ni tiba
Nzige ndio kumbi kumbi au?
Mtuachie sisi tukionyeshe kazi.kitimoto nae haram!
---------------------------------------------![]()
Hii ni spesho kwa Wateule wa Bwana, wasiofungwa na dhamira na sheria bali wakidodondozwa unono na Neema zitokazo kwa Mungu.
Haswaaa !!!.Kwahyo kisayansi kuna madhara ukiwala!?...Hilo ni agano la kale lilishatenguliwa sasa hivi hata kunguni ukiweza we kula tu!..kikutokacho ndio najisi!
Wasabato mna shida sana soma Mathayo 15:11 (11 Kitu kinachomtia mtu unajisi si kile kiingiacho kinywani, bali kile kitokacho kinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu unajisi.”)Wapendwa tupitie sehemu ya maandiko kuhusu vyakula visivyofaa kutumiwa na mwanadamu!
Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia. Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia,
,**Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi.
1.Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu ya kupasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala.
2.Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato;
*Ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
*Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.
*Katika hao wote walio ndani ya maji mtakula hawa; kila aliye na mapezi na magamba, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, mtakula hao.Na hao wote wasio na mapezi na magamba, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, hao ni machukizo kwenu, watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu.Kila asiye na mapezi wala magamba aliye ndani ya maji ni machukizo kwenu.
*Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu, na mwewe, na kozi kwa aina zake, na kila kunguru kwa aina zake;
*Na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake, na bundi, na mnandi, na bundi mkubwa, na mumbi, na mwari, na mderi, na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo.
*Pamoja na hayo, hivi vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne ni halali kula, hao walio na miguu mirefu, ya kurukia juu ya nchi; katika hao mna ruhusa kuwala; nzige kwa aina zake, na nzige kuu kwa aina zake, na panzi kwa aina zake, na parare kwa aina zake.
*Lakini vyote vitambaavyo vyenye mabawa, vilivyo na miguu minne, ni machukizo kwenu.
* Kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, naye hana kwato mbili, wala hacheui, huyo ni najisi kwenu; kila agusaye wanyama hao atakuwa ni najisi.
*Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni.
*Tena katika vitu vile vitambaavyo, vitambaavyo juu ya nchi, hivi ni najisi kwenu; kicheche, na panya, na mjombakaka, kwa aina zao na guruguru na kenge, na mjusi na goromoe, na lumbwi.
Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; awaye yote atakayewagusa, wakiisha kufa, atakuwa ni najisi hata jioni.
(Mambo ya Walawi 11:01-31)
Karibuni kwa michsngo au maoni
Kitu kinachomtia mtu unajisi si kile kiingiacho kinywani, bali kile kitokacho kinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu unajisi.” Mathayo 15:11
BWANA MUNGU, alikuwa na sababu alipomwagiza Musa awaambie watu wale nini na nini wasile. Hakujisemea tu ili kujifurahisha. Yeye MUNGU, ndiye aliyemuumba mwanadamu, hivyo anajua mahitaji ya kimwili ya mwanadamu, anajua nini kinafaida kwenye mwili wa binadamu, na nini hakina faida.Unaweza ukanipa uhusiano wowote wa kimantiki (logical corelation) kati ya 'mnyama kutocheua' na mnyama kuwa 'najisi'? Either ki-imani, kisayansi au hata kwa logical thinking tu..;
Kwamba iliandikwa kwenye vitabu haimaanishi tusijiulize maswali au kuhoji..
Inaonekana ninyi hamkuelewa content ya maneno ya BWANA YESU. Ni kweli kabisa hakuna kitu utakachokula chini ya jua kikautia "moyo" wako unajisi. Kwa maneno mengine chakula hakiwezi kukufanya wewe ukahesabiwa dhambi. Ndiyo maana ukiendelea kusoma hapo utaona wanafunzi wa YESU wanamuuliza tena kuhusu hiyo kauli yake na Yeye anaifafanua zaidi. Soma MATHAYO 15:17-20.Wasabato mna shida sana soma Mathayo 15:11 (11 Kitu kinachomtia mtu unajisi si kile kiingiacho kinywani, bali kile kitokacho kinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu unajisi.”)
Halelujaah halelujaaah bwana ametamarak8.![]()
Hii ni spesho kwa Wateule wa Bwana, wasiofungwa na dhamira na sheria bali wakidodondozwa unono na Neema zitokazo kwa Mungu.