Vyakula ambavyo haviruhusiwi kutumiwa na binadamu

Duh! Ila hiyo avatar na jina ni balaa. Avator ni jini, na hilo jina vipi mkuu
Kitongoji cha Pabaya, Kijiji cha Nyibhoko, Kata ya Kisaka, Tarafa ya Ngoreme, Wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara, Shit-hole. BadBoy anakula nguruwe hadi jini atatorokea Misri kutafuta hifadhi
 
Nje ya tiba pia ni nyama TAMU SANA.
 
Dini ni upuuzi tu!
Ndiyo dini hiyo hiyo inayo kataza kila kitu kizuri hata ‘kupiga ndogo’dini inakataza wkt ni tamu kweli kweli
Dini hizi tuzipuuze tu!
 
Hiyo imepitwa na wakati.... Ilikuwa agano la kale kabla ya Kristo!
 
Wasabato mna shida sana soma Mathayo 15:11 (11 Kitu kinachomtia mtu unajisi si kile kiingiacho kinywani, bali kile kitokacho kinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu unajisi.”)
 
BWANA MUNGU, alikuwa na sababu alipomwagiza Musa awaambie watu wale nini na nini wasile. Hakujisemea tu ili kujifurahisha. Yeye MUNGU, ndiye aliyemuumba mwanadamu, hivyo anajua mahitaji ya kimwili ya mwanadamu, anajua nini kinafaida kwenye mwili wa binadamu, na nini hakina faida.

Ni kama binadamu, anapotengeneza gari anakuwa anajua hilo gari linahitaji nini ili lifanyekazi vizuri. Lazima machine yoyote ile inapotengenezwa inaambatana na "manual instruction" yake. Vivyo hivyo BWANA MUNGU alimpa Musa maagizo ambayo ni kama "manual instruction" ya miili yetu.

Wanadamu kwa kiburi chao, wamekiuka hiyo "manual instruction" na kuanza kula chochote wanachojisikia kula, matokeo yake sasa hivi kuna magonjwa ambayo hayana hata tiba. Lengo la MUNGU lilikuwa ni kutulinda ili tusipate madhara kwa kula hivyo vyakula alivyovikataza, sababu alijua vina madhara kwa mlaji.
 
Kitu kinachomtia mtu unajisi si kile kiingiacho kinywani, bali kile kitokacho kinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu unajisi.”
Mathayo 15:11
 
Wasabato mna shida sana soma Mathayo 15:11 (11 Kitu kinachomtia mtu unajisi si kile kiingiacho kinywani, bali kile kitokacho kinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu unajisi.”)
Inaonekana ninyi hamkuelewa content ya maneno ya BWANA YESU. Ni kweli kabisa hakuna kitu utakachokula chini ya jua kikautia "moyo" wako unajisi. Kwa maneno mengine chakula hakiwezi kukufanya wewe ukahesabiwa dhambi. Ndiyo maana ukiendelea kusoma hapo utaona wanafunzi wa YESU wanamuuliza tena kuhusu hiyo kauli yake na Yeye anaifafanua zaidi. Soma MATHAYO 15:17-20.

YESU alisema chakula hakiwezi kukufanya ukawa na dhambi, lakini hakusema kuwa chakula fulani hakiwezi kukuletea madhara kiafya. Wakati ule BWANA MUNGU, alimpo mpatia MUSA, list ya nini kiliwe na nini kisiliwe, lengo lake lilikuwa ni kuwaepusha Waisraeli, na magonjwa ambayo wangepata baada ya kula vyakula hivyo. Waisraeli hawakuelewa maana yake, wao walifikiri ukila hivyo vyakula vilivyokatazwa na MUNGU unapata dhambi, kumbe siyo dhambi, ni madhara tu ya kimwili. Na kwasababu MUNGU anawapenda wanadamu, ambao ni watoto wake, hakutaka wale hivyo vyakula kisha wadhurike ndiyo maana alivikataza. Wao wakafikiri ukila unapata dhambi, ndiyo maana YESU alipokuja akalifafanua hilo swala kwa undani zaidi. Cha ajabu kuna watu mpaka leo, licha ya YESU kufafanua bado hawaelewi maana ya neno "najisi".

Ukweli ni kwamba hivyo vyakula vilivyokatazwa vina madhara makubwa kwenye mwili wa mwanadamu, lakini vikiliwa havina unajisi kwenye "roho" ya mlaji. Ndiyo maana YESU akasema kila kiingiacho mdomoni kinaenda tumboni kisha kinatoka na kwenda chooni. Waliomwelewa YESU, alimaanisha nini, kamwe hawawezi kula hivyo vyakula sababu ya kuitunza miili yao na roho zao pia. Ni kweli, unaweza ukala hivyo vyakula na usipate dhambi, hiyo ni sawa kabisa; lakini ukila, unaweza kupata madhara ya kimwili hasa kama hivyo vyakula havikuandaliwa vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…