Katika vitu namshukuru sana mama yangu na mshua, japo mshua alikua miyeyusho kwenye mambo mengine, ni masuala mazima ya afya. Sijawahi kuwasikia hawa wazee wakilalamika kabisa magonjwa mpaka uzee wao kwa kufuata hizi taratibu
Nakumbuka mwaka 2001 ndipo formula mpya home za ulaji zilichukua ukurasa. Japo, sifuati exactly kama wao kutokana pia na changamoto za kimaisha lakini angalau nina mambo mengi aidha naacha au nauhuisha mwili wangu kwa kufuata kanuni hizo.
Kuna mzee pia anaitwa Fredrick Macha - huyu ni mtanzania anaishi London. Ana mambo mengi sana yenye kufundisha kwa masuala mazima ya afya na mazoezi. Ni vile tu watz tubapenda kufuatilia upuuzi na mambo yenye kupumbaza fikra. Youtube channel yake anaweka mambo ya maana sana na yenye kufaa lakini hakuna watazamaji. Na ninachompenda si mchoyo na haoni tabu kutoa muda wake kuelekeza jambo kama ukiweza kumuandikia. Mimi huwasiliana sana kwa WhatsApp na nikapata kumuuliza chungu nzima ya maswali.