Mleta mada.
Kwanza hongera kwa kuleta uzi huu humu ndani pia Mkuu pole sana kwa kuwa kuna watu wanabeza kile ulicholeta pamoja na Dr Sebi.
Niwe mkweli kuwa huyu jamaa sikumjua kabla, niliwahi kumsikia mwaka jana 2019 ila nikamsoma kidogo kisha nikamuacha.
Tukija upande wa cancer naona watu wanazungumza tu ila ndio ugonjwa unaoongoza kuwa mkali kwa kumaliza watu Tanzania, kama haishiki nafasi ya kwanza basi ya pili.
Wapumbavu wanapinga hoja ya vyakula ila wamtafute oncologist(Daktari Bingwa wa Kansa) yeyote yule aulizwe njia ya kuepuka kansa ni ipi? Majibu ya mwanzoni yatakuwa ni haya ...
1. Kula matunda mara kwa mara
2. Kula mboga za majani
Ninachoweza kusema na kuamini ni kuwa Mungu ametupa matibabu hapa hapa chini ya ardhi, mwanadamu ameumbwa kwa udongo, nadhani hata matibabu yake yanatoka hapo kwa sehemu kubwa.
Hii kansa ni moja ya biashara kubwa saana kulimwenguni, japo huwezi kuifananisha na AIDS.
Kuhusu cancer tu wanakataa baadhi ya facts, ukija kuwaletea biashara ya HIV si watakuona kichaa.
Uhalisia wa mambo tunayofahamu ni tofauti na uhalisia.
Sent using
Jamii Forums mobile app