Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Tumekuwa tukipokea maoni toka kwa watu wengi juu ya matatizo ya kukosa usingizi, ingawa kuna
sababu nyingi zinazoweza kukufanya ukose usingizi kama magonjwa nk, ila mlo nao ni moja ya
sababu hizo.Na moja ya vyakula hivi ni vile vyenye mafuta (fat) mengi kama burger, chipsi nk.
Tafiti zinaonesha kuwa, vyakula hivi sio tu hukufanya uongezeke uzito bali pia huabiri mfumo wa kulala.
Tafiti zinaendelea kuwa, vyakula hivi vizito huamsha mfumo wa usagaji vyakula (digestion system)
na kuifanya ianze kufanya kazi, hii hukupelekea mwili wako kuwa hai na pia hukufanya mara nyingi
kujisikia kwenda haja hivyo kukukosesha
usingizi.
Hivyo basi epuka kula mlo wenye wanga mwingi wakati wa usiku au angalau kwa masaa mawili kabla ya kwenda kulala.DONDOO: Vyakula vya mafuta ni chanzo cha kukukosesha usingizi