Vyakula vya siku hizi havina harufu kabisa

Mbatata kwa roast ya nyama ilikuwa habari kubwa ,ila sikuhizi hamna kitu hata ndondo la nazii linakosa ladha siku hizi unatafuna karoto hamna kitu!mapapai embe dodo mastafeli mayai kuku shida tupu
 
Siku izi kila kitu kinakuzwa kwa kemikali mambo ya mbolea hayo ndio sababu kubwa ya kupungua kwa harufu ya vyakula. Nimechunguza hata kunde na maharage hayatoiwi harufu kabisa kama zamani.
 
Vyakula vingi vya dar havina ladha ila ukiwa mkoani vikapikwa fresh vina taste aisee. Pia sikuhizi kuna michakachuo ya misosi. Wali uwe mtamu upikwe na mkaa.
Haswaa
 
KUNA WATU WANAITWA MONSTER SANTO (MONSANTO) HAWA WATU WEKA MBALI NA WATOTO, HAWA NI MAJASIS WA MBEGU ZA MAUAJI KIPITIA MBEGU NA MAZAO, VYAKULA VYA GENETICALLY MODIFIED ORGANISM (GMO) WEKA MBALI NA WATOTO
 
KUNA WATU WANAITWA MONSTER SANTO (MONSANTO) HAWA WATU WEKA MBALI NA WATOTO, HAWA NI MAJASUS WA MBEGU ZA MAUAJI KIPITIA MBEGU NA MAZAO, VYAKULA VYA GENETICALLY MODIFIED ORGANISM (GMO) WEKA MBALI NA WATOTO.
 

Mkate Wa SUNKIST huo. Yani ukila mpaka unasikia raha. Sio kama ya huku Dar ukila leo na kesho, kesho kutwa huna hamu ushakinai!!!!
 
Zamani wali ukipikwa tunaoga mapema na kuimba siku hizi tumeuzoea ndio tofauti
 
Zamani wali ukipikwa tunaoga mapema tunaimba hatu sinzii siku hizi tumeuzoea
 
 
kweli mkuu zamani hata ugali wa dona ulikuwa unanukia sana tu siku hakuna kitu zimebaki dagaa za kukaanga tu
 
Pua zako zitakuwa zimekufa mkuu!

Wala sio pua ni kweli vyakula vimepoteza harufu pia na ladha hususan wali
HII INATOKANA NA MAPISHI YA SASA NI TAFAUT NA YA ZAMANI
Leo wali ukipikwa badala ya kufunikiwa ati unavalishwa mfuko wa nailoni kwa juu hapo ndio wanafunikia unaiva kwa mvuke wajoto la nailoni saa ngapi utanukia???
MAPISHI YA ENZI ZILE WALI UKIKARIBIA KUIVA UNAONA MOTO UNAPUNGUZWA NA KUFUNIKIWA MKAA JUU NA MKAA CHINI HAPO SASA UKIPAKUA UNAKUTA UKOKO WA JUU NA UKOKO WA CHINI HARUFU YAKE WAKATI UNAUPAKUA KTK SINIA HADI MTAA WA NNE[emoji3]
 
Sahivi hadi nazi hazinukii sijui ndo nazi za kichina zimekomaa miezi 6
 


Wacha uwongo teja wewe. Vyakula vyetu vina harufu murua tu sema wewe pua yako na mapafu yameungua kutokana na kutumia madawa ya kulevya.
 
Kweli kabisa vyakula siku hizi vimekosa ladha na harufu ya kutamanisha ukilinganisha na kipindi cha nyuma labda ni sababu ya maendeleo ya sayansi na teknologia kwenye kilimo vyakula vingi nowadays vinazalishwa kutumia kemikali nyingi hivyo kupelekea kupotezz uhalisia wake , mf rahisi kwangu ni Pilipili kwa wale wenzangu wapenda pilipili siku hizi pilipili mbuzi hazina harufu na ukali kama miaka ya nyuma huwezi amini unaweza mpa hata mtoto akaila bila wasi, hili la kemikali limeenda mbali mpk kwenye mifugo unategemea nn kuku anayefugwa kwa wiki 3 then analiwa akawa na harufu na ladha nzuri?
Sababu ya mwisho ni mazoea ya kula chakula fulani mara kwa mara inatufanya tukinai na tusiwe na attention nacho kikipikwa nakumbuka miaka ya 80's kitu Pilau ilikuwa si mchezo ikipikwa jua ni sikukuu au msiba, nyama ya ng'ombe ilipikwa wikiendi kuku anachinjwa mpk kuwe na mgeni hii ilipelekea kuongeza hamu ya hv vyakula siku hz pilau lapikwa muda wowote!
 
Mchele unaouzwa madukani huwa unakaa muda mrefu sana hivyo hupauka. ili kuutunza na kuhifadhi mngáo wake wafanyabiashara wanaupaka mafuta ya kula. mchele hata wa mwaka mmoja utauona kama mpya ila harufu ndo hutaisikia ngóoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…