Vyakula vya siku hizi havina harufu kabisa

Vyakula vya siku hizi havina harufu kabisa

Wakuu najua mko poa,
Yaani vyakula vya siku hizi havina harufu kabisa. Miaka ya nyuma kipikwe kitu cha wali hadi mtaa wa 7 utakisikia tu, lakini sasa hivi hata kipikwe hapo hutosikia harufu yake na hata mdomoni hauna ladha kivile.

Wajameni kulikoni harufu na ladha ya vyakula haipo siku hizi ????
mkuu mpishi wako hajitambui! tena sikuhizi ujuzi ndo umeongezeka iweje usisikie harufu?
 
Mbatata kwa roast ya nyama ilikuwa habari kubwa ,ila sikuhizi hamna kitu hata ndondo la nazii linakosa ladha siku hizi unatafuna karoto hamna kitu!mapapai embe dodo mastafeli mayai kuku shida tupu
Kote huko vijijini walimaji wanatumia mbolea za mchina unategemea nini?sasa hivi parachichi la mbeya dogo dogo km kitunguu wanaita ya kisasa.
 
Kote huko vijijini walimaji wanatumia mbolea za mchina unategemea nini?sasa hivi parachichi la mbeya dogo dogo km kitunguu wanaita ya kisasa.
Hataree mkuu! Zamani punga jipya likipikwa unasikilizia mtaa wa tatu hiyo harufu lakini siku ukiwa sebuleni ya jikoni huyajui!
 
Hata Michele wa siku hiz sio kama ule wa Kipindi kile. Yaani chumba cha kwanza wanapika wali lakn chumba cha pili hata kusikia harufu Hamna. Hii yote inatokana na ongezeko La madawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mjumbe moja alivyosema hapo juu. Technology imechangia unapikia rice cooker wakati ubwabwa wafa kupikiwa kwenye mka afu nakuweka mka juu.
Pia ndizi cku hizi zonapikwa pressure cooker. Unategemea nn. Hapohapo na mpishi anachangia unapika huku unachat
What do you expect?
 
Mbolea kutoka ulaya haikuwepo tulikula chakula cha asili Leo kila kitu Mbolea bila hiyo huvuni
 
Hapa ndio utajua umuhimu wa kuweka viungo kama vile mdalasini, uzile {bizari nzima}, pilipili manga {pilipili mtama}, hiliki na pilau masala kwenye chakula
 
Hapa ndio utajua umuhimu wa kuweka viungo kama vile mdalasini, uzile {bizari nzima}, pilipili manga {pilipili mtama}, hiliki na pilau masala kwenye chakula
Mku hata zamani hizo mambo zipo ila sikuhuzi majanga hadi tangawizi haiwashi siku hizi unakunywa tangawizi kama appke juice tu sasa hakuna ile ukimaliza kikombe na kijasho juu
 
Mku hata zamani hizo mambo zipo ila sikuhuzi majanga hadi tangawizi haiwashi siku hizi unakunywa tangawizi kama appke juice tu sasa hakuna ile ukimaliza kikombe na kijasho juu
Mabadiliko ni kitu cha kawaida, maana nakumbuka zamani nilikuwa nikijihisi homa nakunywa mwarobaini na ulikuwa mchungu balaa, lakini mwarobaini wa sahv umepooza kabisa.
 
Mku hata zamani hizo mambo zipo ila sikuhuzi majanga hadi tangawizi haiwashi siku hizi unakunywa tangawizi kama appke juice tu sasa hakuna ile ukimaliza kikombe na kijasho juu
Hahaha jmn tangawizi isowasha inapatikana wapi?
 
[emoji3] au wanatia maji mengi
No i mean unaenda kununua raw tangawizi una prepare mwenyewe kila kitu at the end unakunywa sparleta badala ya tangawizi ile ya kukutoa kijasho kwa ukali!
 
Back
Top Bottom