Uchaguzi 2020 Vyama 8 vinavyoshiriki Uchaguzi vyamtaka Mbowe ajieleze kwa Msajili baada ya kuviita ni vyama bandia

Uchaguzi 2020 Vyama 8 vinavyoshiriki Uchaguzi vyamtaka Mbowe ajieleze kwa Msajili baada ya kuviita ni vyama bandia

Kuna haja kama sio sisi wenyewe mabeberu watusaidie kuwe na masharti magumu hivi vyama vipungue, walau tuwe na vyama 3 hadi 4 tu vya siasa.
 
Kuna haja kama sio sisi wenyewe mabeberu watusaidie kuwe na masharti magumu hivi vyama vipungue, walau tuwe na vyama 3 hadi 4 tu vya siasa.
Subiri October 28 chadema mkose wabunge na madiwani halafu uje na huo ushauri vyama vipi vibakie
 
Vyama 18 vimemtaka mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuomba msamaha kufuatia kauli aliyotoa hivi karibuni kuwa vyama vingine ni vyama bandia..
Freeman Mbowe asiwaombe msamaha hawa vyama 18. Bali na wao kwa umoja wao waidhalilishe CHADEMA kuwa ni kibaraka wa CCM.
 
Vyama 8 vimemtaka mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuomba msamaha kufuatia kauli aliyotoa hivi karibuni kuwa vyama vingine ni vyama bandia...
Hivi ni vyama vya kuidanganya dunia kuwa Tanzania inafuata siasa za vyama vingi ....vinalipwa kila kitu ...vyama vya uchaguzi ...ifike mahali chama kama hakina hata mtendaji wa mtaaa kishushwe usajili wake uwe wa muda
 
Vyama 8 vimemtaka mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuomba msamaha kufuatia kauli aliyotoa hivi karibuni kuwa vyama vingine ni vyama bandia...
Je, Mahera ataonywa lini?
 
Vyama pandikizi; uzuri wananchi wanajua kwa sura na kwa tabia.
 
Vyama 8 vimemtaka mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuomba msamaha kufuatia kauli aliyotoa hivi karibuni kuwa vyama vingine ni vyama bandia.

Vyama hivyo vimesema Mbowe amevidhalilisha na amevunja sheria na huku vyama hivi vimesajiliwa kama kilivyosajiliwa CHADEMA.

Wamekitaka CHADEMA wajitoe kwenye uchaguzi kwani wamekata pumzi na watabaki vyama 14 vyenye wagombea machachari akiwemo Mwanamama Queen.

My take: Hivi kweli hivi vyama vidogo vina strategies yoyote katika kukuza vyama vyao au ni wasindikizaji wa siasa hapa Tanzania hasa kwenye uchaguzi?
Usilolijua tu hata Chadema nacho kilikua chama kidogo Sana,back on 2000-2005,
Vyama vilivyowahi kuavikubwa na kusumbua Ni Kama NCCR,TLP,CUF na Kisha Sasa Ni CHADEMA huku ACT ikianza kuonekana kuchukua hatamu ya Chadema soon after October 28.

So wanahaki ya kumuonya,na hata nchi zingine vyama vidogo viliwahi kuja kukua na kua vyama vikubwa.

Mbowe anatoa picha ya umimi,ubinafsi na ubaguzi unaotajwa Sana ndani ya hiki chama Cha kusaka rudhuku kwa udi na uvumba
 
If they feel aggrieved, let them file a suit against Mbowe. Wao wanajua kwamba ni vibaraka wa CCM ila hawataki mtu aseme hilo jambo.
Alichokisema Mh.Mbowe IS A DEEP PAINFUL TRUTH kwa fraudulent political parties ambayo ni matawi ya ccm.
 
Vyama 8 vimemtaka mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuomba msamaha kufuatia kauli aliyotoa hivi karibuni kuwa vyama vingine ni vyama bandia.

Vyama hivyo vimesema Mbowe amevidhalilisha na amevunja sheria na huku vyama hivi vimesajiliwa kama kilivyosajiliwa CHADEMA.

Wamekitaka CHADEMA wajitoe kwenye uchaguzi kwani wamekata pumzi na watabaki vyama 14 vyenye wagombea machachari akiwemo Mwanamama Queen.

My take: Hivi kweli hivi vyama vidogo vina strategies yoyote katika kukuza vyama vyao au ni wasindikizaji wa siasa hapa Tanzania hasa kwenye uchaguzi?
Waende Mahakamani
 
Umeandika 18 heading.
Then 8 ndio wametoa onyo kwa niaba ya 14.

ndio nini hii?
 
wanataka wao wewe ndio chama pekee ila wakianzisha wengine bandia.Kwa hio Ada tadea sio watu.
 
Muungano wa vyama vinane vya siasa vinavyoshiri Uchaguzi Mkuu, vimemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, amuite Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ajieleze kwa madai kuwa ameviita vyama hivyo ni bandia.

Makatibu wakuu wa vyama hivyo, wametoa msimamo huo wakati wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Vyama vilivyokutana na kutoa tamko hilo ni ADC, NRA, DP, UMD, SAU, UPDP, Demokrasia Makini na AFP.

Makatibu hao walisema Mbowe alisema vyama hivyo ni bandia, kwa kuwa kupitia Tume ya Maadili ya Uchaguzi vilipitisha azimio la kusitisha kampeni za mgombea urais kupitia Chadema, Tundu Lissu baada ya kukiuka kanuni na taratibu.

Kiongozi wa Muungano huo ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Democratic (DP), Abdul Mluya alisema kauli hiyo ni sawa na udhalilishaji kwa vyama hivyo, vilivyoundwa kwa mujibu wa sheria na taratibu.

"Mbowe ametukosea sana adabu sisi kama viongozi wa vyama hivi lakini pia wanachama wetu, kwa kauli yake kuwa vyama vyetu ni bandia, kauli yake hiyo haivumiliki na zaidi imelenga kutuchafua mbele ya wanachama wetu na taifa kwa ujumla" alisema Mluya.

Alisema kauli hiyo na nyingine kuwa vyama hivyo vinatumika kisiasa wakati huu wa Uchaguzi Mkuu ni sawa na matusi kwa vyama hivyo. Alisema vyama hivyo vinahoji Mbowe anapata wapi kiburi cha 'kuwatukana' hadharani.

Mluya alidai kuwa Mbowe na viongozi wengine wa Chadema, wanaonekana kukosa hoja za msingi hasa wakati huu wa harakati za Uchaguzi Mkuu.

Aliomba watanzania wanasubiri kuona Msajili wa Vyama vya Siasa, anatoa adhabu kali kwa Mbowe na Chadema ili iwe fundisho kwa wenye tabia kama hiyo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima (AFP), Rashid Rai alisema umefika wakati kwa watanzania kuipima Chadema na viongozi wake, hasa kutokana na kauli za mara kwa mara zinazoashiria uchokozi wa kisiasa.

Alidai kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa chama hicho, kutoa kauli za uchochezi na kuvunja umoja. Aliwataka wananchi wakiepuke ili taifa lisipoteze amani.

Rai alisema Chadema wameona uchaguzi umekuwa mgumu kwao; na ndiyo maana wameanza kuleta chokochoko kuuharibu, kama ambavyo wamekuwa wakionekana wakinadi sera majukwaani

"Ukiangalia tabia zao, mienendo yao utaona kabisa kuwa wamepoteza dira, hivi vyama ni halali kisheria na mahali pote ambapo wao wapo hivi vyama, pia vipo na vyote vinafanya kazi kisheria. Iweje watuite kuwa sisi ni vyama bandia" alihoji.

Rai alisema vyama hivyo, vinafanya kazi kwa utaratibu wao na si kufuata yale ambayo Chadema wanayataka. Aliitaka Chadema kutambua kuwa vyama vya siasa ni mali ya wananchi na ndiyo wanaohusika kuchagua.
 
Chama kimeanzishwa zaidi ya miaka 10 nyuma hakijawahi hata kupata diwani halafu useme hicho ni chama cha siasa.
Tusioneane aibu ktk kusema ukweli. Ni mfano wa vyama mfu.
Chama kama ADC kina nguvu kuliko Chadema Zanzibar uchaguzi uliopita kilitoa waziri wa serika Zanzibar Hamad Rashid Mohammed wakati chadema hakikuambulia hata mbunge wala mwakilishi wa baraza LA wawakilishi Zanzibar

Chama kama NRA in cha waislamu wengi wa siasa Kali sio cha mchezo mchezo

UMD kina wanyamwezi kibao na kilikuwa chama chenye nguvu mno kabla ya Chadema kikashuka safari ambayo hata Chadema safari hii kinaelekea huko huko
 
Back
Top Bottom