beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Vyama vitatu vya siasa nchini Uingereza vimetangaza makubaliano ya kushirikiana ili kupata wanachama zaidi katika bunge ambao wanaunga mkono Uingereza kubakia katika Umoja wa Ulaya.
Vyama hivyo vitatu vya Liberal Democrats, Chama cha Walinzi wa Mazingira na chama cha Plaid Cymru cha jimbo la Wales vimekubaliana kushirikiana katika viti 60 kati ya viti 650 katika uchaguzi wa Disemba 12, ikimaanisha kuwa mgombea mmoja tu kutoka vyama hivyo vitatu atawania uongozi katika kila jimbo.
Kiongozi wa chama cha Liberal Democrat Jo Swinson ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa ana furaha kutangaza ushirikiano huo ili kupata wabunge wengi wanaounga mkono Uingereza kubakia katika Umoja wa Ulaya.
Nae kiongozi wa chama cha walinzi wa mazingira Jonathan Bartley amesema uamuzi wao wa kushirikiana unalenga kuhakikisha wana wawakilishi wengi katika bunge lijalo wanaotaka Uingereza ibakie katika Umoja wa Ulaya.
Hata hivyo chama cha wahafidhina chake Waziri Mkuu Boris Johnson kinautumia mpango wa "kufanikisha Brexit" kama kauli mbiu ya kampeni zake nacho chama cha Labour kimewaahidi wapiga kura kitafanya juhudi zote ili kura ya maoni kuhusu Brexit iitishwe upya.