Uchaguzi 2020 Vyama vya siasa msiteue wabunge waliokaa miaka kumi au zaidi bungeni kugombea ubunge

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Hakuna sheria inayotamka ukomo wa mbunge. Rais tu ndio ana ukomo wa miaka kumi.

Kuingiza damu mpya ni muhimu kwa vyama vyenyewe vya siasa na nchi ili kuingiza mawazo mpya na msukumo mpya.

Naomba vyama vyote vya siasa ikiwemo CCM, mbunge yeyote aliyekaa bungeni miaka kumi au zaidi awe wa kuchaguliwa, kuteuliwa au viti maalumu, kateni jina lake

Mambo mengine sio lazima katiba iseme. Miaka kumi kwa mbunge inamtosha.

Watu wasigeuze ubunge kuwa ni uchifu.
 
Naunga mkono hoja ingawa watakataa kwa kuwa huko kuna pesa sana. Swali ni je, nani asiyependa pesa na marupurupu + kuitwa mheshimiwa hata Kama ukiongea utopolo?
 
Kabisa, hasa wabunge wa ccm. Wa upinzani ni vichwa, wao wanaweza kuendelea hata miaka 30. Toka nimekufahamu angalau leo umeongea cha maana.
Uwezo wa kujua cha maana umeutoa wapi!? Maana naona hata ulichoandika ni upuuzi tuu wenye double standard.
 
hata mapendekezo ya rasimu ya Jaji Warioba waliliona hili, ni kweli kbs hakuna sababu hata chembe ya kumfanya mbunge kuhudumu kwa vipindi zaidi ya viwili...watz wengine wapya wanapaswa kupewa nafasi kuonesha uwezo wao kuwatumikia wananchi.

natambua wabunge waliopo hawawezi kukubali kwa kujificha kwenye maneno hiyo ni demokrasia eti acha wananchi wenyewe waamue huku wakitumia rushwa na figisu waendelee kuwa wabunge wafaidi posho za bure na kiinua mgongo cha dhulumat!.
 
Hii itasaidie pia kupokezana kwa amani kwenye ubunge sababu anajua wazi miaka kumi ikifika kwa heri

Sasa hivi mbunge kuondoka Ni Kama Vita ya dunia kakaa miaka kumi au zaidi ya miaka kumi kumtoa Ni shughuli pevu hata chama kikiata jina ananuna anatangaza Vita na chama na viongozi wa chama Kama vile yeye alizaliwa kuwa mbunge

Lazima tuanzie mahali kila chama kivalie njuga Hilo kuwa umetumikia miaka kumi pisha Kama Kuna vyeo vingine kwenye chama au serikali wakitaka wampe lakini ubunge akatwe

Hili halitakiwi kucheka cheka
 
Demokrasia ifanye kazi tu, kwa kuwa hakuna ukomo wa ubunge haina shida
 
Naunga mkono hoja ingawa watakataa kwa kuwa huko kuna pesa sana. Swali ni je, nani asiyependa pesa na marupurupu + kuitwa mheshimiwa hata Kama ukiongea utopolo?
Keki hiyo pia inatakiwa kugawanywa .Kala miaka kumi na zaidi inamtosha apishe wengine wale pia.Pia Ni njia ya kupanua wigo wa maendeleo kwenye familia nyingi zaidi akiwa huyo huyo tu ndio mla hiyo keki familia zingine zitakufa kwa utapia mlo!!! Kupokezana muhimu pia
 
kwa tz hilo sio rahisi kutokea, ni ama wabunge waliopo ili usifanikiwe watakutoa uhai au watakuloga uwe chizi kbs!.
 
Naunga mkono hoja ndungai,mwakyembe,mdee,zitto,mkuchika,mama sita ,mkono,maghembe wapumnzike
 
Najua hofu yako ni wabunge kiboko ya maccm kina mh Mbowe, hata usemeje wabunge wakosoaji wa serikali yenu bado wapo sana
Hakuna sheria inayotamka ukomo wa mbunge. Rais tu ndio ana ukomo wa miaka kumi.

Kuingiza damu mpya ni muhimu kwa vyama vyenyewe vya siasa na nchi ili kuingiza mawazo mpya na msukumo mpya.

Naomba vyama vyote vya siasa ikiwemo CCM, mbunge yeyote aliyekaa bungeni miaka kumi au zaidi awe wa kuchaguliwa, kuteuliwa au viti maalumu, kateni jina lake

Mambo mengine sio lazima katiba iseme. Miaka kumi kwa mbunge inamtosha.

Watu wasigeuze ubunge kuwa ni uchifu.
 
Hii itasaidie pia kupokezana kwa amani kwenye ubunge sababu anajua wazi miaka kumi ikifika kwa heri

Sasa hivi mbunge kuondoka Ni Kama Vita ya dunia kakaa miaka kumi au zaidi ya miaka kumi kumtoa Ni shughuli pevu hata chama kikiata jina ananuna anatangaza Vita na chama na viongozi wa chama Kama vile yeye alizaliwa kuwa mbunge

Lazima tuanzie mahali kila chama kivalie njuga Hilo kuwa umetumikia miaka kumi pisha Kama Kuna vyeo vingine kwenye chama au serikali wakitaka wampe lakini ubunge akatwe

Hili halitakiwi kucheka cheka
Umenikumbusha vita ya wassira na bulaya
 
Wewe nani?

Nawewe ufukuzwe hapo lumumba na hiyo kazi yako ya kupika chai apewe mwenzako

Back
Top Bottom