KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Kiutawala, mitaa ,vijiji na vitongoji ni ngazi iliyo karibu zaidi na wananchi na uchaguzi wa Serikali za mitaa ,vijiji na vitongoji ndio kipimo Cha vyama vya siasa kujipima kukubalika kwao na wananchi walio wengi.
Hapo ni Kwa muundo wa Serikali ,mitaa ,vijiji na vitongoji ndio ngazi ya karibu sana wananchi lakini ukienda upande wa CCM na Kanisa Katoliki wana kipimo Cha chini zaidi.
Kwa muundo wa Kanisa Katoliki, jumuiya ndio ngazi ya chini kabisa na hii ipo karibu zaidi na wananchi kuliko vijiji, vitongoji na mitaa.
Kwa muundo wa CCM , kuna balozi wa nyumba kumi au shiba ambaye Kwa muundo wa Chama ni ngazi ya chini kabisa na ni ya chini zaidi na ya karibu zaidi na wananchi kuliko Ile ya jumuiya Kwa Kanisa Katoliki au mitaa Kwa Serikali.
Hapo tunaona ni jinsi gani uchaguzi wa Serikali unavyoweza kubadili matarajio ya Chama Chako kwenye Uchaguzi mkuu Kwa sababu ni kipimo Cha kukubalika Kwa Chama Chako Kwa wananchi walio wengi.
Vyama vinavyosusia uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji na vinataka kushiriki uchaguzi mkuu ni sawa na kujivika bomu la kujitoa muhanga wenyewe maana wanashiriki bila kujua wanakubalikaje.
Ushauri wangu Kwa vyama vya siasa vyenye tabia ya kususa uchaguzi wa Serikali za mitaa waache maana wanajiumiza wenyewe na athari za kususa uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2019 zilionekana uchaguzi mkuu wa 2020 ambapo tuliona matokeo mabaya Kwa vyama vya upinzani toka mfumo wa vyama vingi uanze.