The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Baadhi ya vyama vya siasa visiwani Zanzibar vimesitisha mikutano yake ya kampeni kufuatia kifo cha mgombea ubunge wa Jimbo la Fuoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abass Ali Mwinyi, kilichotokea jana.
Miongoni mwa vyama vilivyositisha shughuli zake ni CCM pamoja na Chama cha ACT Wazalendo, ambavyo vimetangaza kuahirisha mikutano ya kampeni ili kupisha msiba huo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa ACT Wazalendo, Salum Bimani, chama hicho kimefanya uamuzi huo kwa kuzingatia utu, mshikamano na heshima ya kibinadamu.
Bimani amesema ACT Wazalendo kilikuwa na mkutano wa kampeni ya mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Othman Masoud, uliopangwa kufanyika Bubwini, wilaya ya Kaskazini Unguja, lakini kimesitisha kwa kuwa mazishi ya marehemu Abassi yamefanyika katika kijiji cha Mangapwani kilichoko jimboni humo.
"Tumesitisha shughuli za kisiasa ili kutoa nafasi kwa familia, ndugu, jamaa na wananchi wote kushiriki katika mazishi na kumzika marehemu kwa heshima stahiki," amesema Bimani.
Aidha, amesema ACT Wazalendo linaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wote katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.