Accumen Mo
JF-Expert Member
- May 15, 2022
- 18,036
- 39,882
Wasalaam ndugu zangu,
Kufuatia hali ya waandamaji na maoni ya baadhi ya watanzania kwenye mitandao ya kijamii, nimegundua CHADEMA hawana nguvu wala watu wengi kutoka na kukosa ushawishi. Chama cha CHADEMA kina misingi mizuri hasa ukiangalia sera zake za awali hata jina lake ni zuri (CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO), ni fupi ila limebeba dhamira kubwa.
Chama hiki kwa tathmini kadhaa kinaokena tatizo ni kwenye kuwafikia watanzania ili waweze kuelewa sera zake kuelekea kushika uongozi wa nchi. Je, kweli kitashawishi watu wapige kura kuwachagua ili kusika usukani wa kuongozi nchi? Baadhi ya mambo kadhaa ambayo yanawafanya CHADEMA Kufeli pakubwa ni kama ifuatavyo:-
Chama kinakuwa kama cha watu wenye asili fulani; ni mapema sana kama chama kimeshindwa kutanua wigo mkubwa ili kuweza kupata ushawishi kila kanda, kwa wakati mmoja ingekuwa ni rahisi kufanya maandamano nchi nzima na watu wengeitika.
Pia soma: Mwl. Nyerere alitaka vyama viwili imara vya siasa vishindane kama tunataka tufanikiwe
Msikifanye chama cha watu wa kaskazini pekee kwa kujaza viongozi wengi kutoka huko, jaribuni kutafuta watu kila kona ya nchi tena wawe kweny uongozi wa juu kwa sababu watu wengine wanafuata ushawishi wa watu wa kwao: je, mnajua kwa nn kwa sasa kule Mbeya kimeanza kushika hatamu? Ni kwa sababu wanaona watu wao kama kama Sugu na wengine wakiwa ndani ya chama hicho, kwa hiyo jaribuni kutanua wigo kusini, pwani, nyanda za juu zaidi.
Chama chenu kimegeuka sehemu ya kufanya vurugu; Mnaweza kufanya siasa safi bila kuathiri mambo mengine kama mlivyaonza mwanza ila sasa mnataka mambo ya vurugu. Hakuna mtu mstaarabu atakubali kujiunga na chama cha vurugu ila kuandamana ni haki yenu kikatiba hamna tatizo, jaribuni kuwajibika sio kubishana na polisi kila siku lumande kama mnavyojua serikali ilivyo. Hii ni nchi ina wasomi mambo ya vurugu sio mahali pake inaleta taswira mbaya kwa chama kwa ujumla: Mtu kama Lema ni vurugu tu badala ya kutoa sera safi ni kutisha watu! Mara anagombana na polisi!! Hii michezo achaneni nayo.
Kuweni na sera endelevu katika kujenga uhai wa chama sio kuibuka kwenye matukio kama vile mnatembelea kik ya watu fulani; Hiko ni chama bhana kiwe na hoja endelevu sio kujitokeza kwenye matukio tu.
Ongeleeni sana kuhusu sera zenu ili kuvutia wananchi na sio kusambaza chuki ili wananchi waichukie serikali iliyopo madarakani; mnaweza kuwa chama bora zaidi bila ya kusambaza chuki kwa wananchi kwa sababu wananchi ndio wanajua serikali inawajibika au laah, kwa nchi za kiafrika viongozi hawana wanalofanya kwa hiyo tumieni mda mwingine kushawishi watu kwa kutoa elimu nzuri. Suala la kusambaza chuki ni kuwapa mwanya washindani wenu kupata la kusema.
Baadhi ya mambo mnayoongea mtandaoni hamshawishi wananchi ila mnawakejeli wananchi kwa sababu mnatumia siasa rahisi ambayo haina logic kwa mtu mwenye akili; Tukiangalia maandamno ya jana basi utagundua hata wenye ushawishi wenu huko mitandaoni kama Twitter hawan hoja zaidi wanayoyaongea yanakejeli wananchi ya kujua: kwa mfano wanakuambia Mbowe ni tajiri halafu kaandamana wewe maskini hutaki, kwa kutumia akili kuandamana kwa Mbowe tajiri kuna logic gani?
Kama tajiri wale Top ten hapa bongo hakuna aliyeandamana. Wengine wanapost picha ya familia ya Mbowe sijui mkewe kasoma! Mara mtoo mtoto wa Mbowe kasoma sana anatokea familia ya kitajiri! sasa angalia hizo ni kejeli au ndio mnashawishi watu?
Acheni siasa rahisi kuweni na point endelevu ina maana maandamano yakipita hmtakuwa na hoja tena?