Vyama vya upinzani hususani CHADEMA rekebisheni makosa mdogo mtafika mbali, Watanzania watawaunga mkono

Vyama vya upinzani hususani CHADEMA rekebisheni makosa mdogo mtafika mbali, Watanzania watawaunga mkono

Mfumo wa elimu wa nchi hii unahitaji maboresho makubwa. Inakuwa vigumu kuamini mtu mzima anaweza kuandika uzi mrefu namna hii huku akishindwa kueleza kiini cha tatizo.
Kama point huzioni basi jaribu kuangalia elimu yako .
 
Accumen Mo,

..natofautiana na wewe unaposema Chadema ni chama cha eneo fulani, ukilenga kanda ya kaskazini.

..hiyo ni hoja ambayo Ccm waliishabikia ili Chadema ichukiwe na Watanzania.

..ngoja nikupe mfano wa safu ya viongozi ambao Chadema ilipata kuwa nao halafu uniambie ni chama cha kina ya Kaskazini, au kwingine.

Mwenyekiti -- Mbowe -- Mchaga.

Makamu - Prof.Safari -- Msukuma.

Katibu Mkuu -- Mashinji -- Msukuma.

Naibu KM -- Mnyika -- Msukuma.

Mwenyekiti Bavicha -- Katambi -- Msukuma.

..Je, kutokana na safu hiyo ya viongozi ni sawasawa kudai Chadema ni chama cha kanda ya kaskazini?

..Lakini ukiacha safu hiyo ya viongozi, Chadema ina mfumo wa uongozi wa KIKANDA. Na kwa maoni yangu kuna kanda kama ya Nyasa ina nguvu na kura nyingi kuliko kanda ya Kaskazini.
Hao wote hawajulikana na umetaka wasukumu na wachaga ni mule mule tu ...Nakuambia ukweli ni sawa na CUF ambacho kilipotea hivyo hivyo, kilikuwa cha watu wa pwani ndio maana kilikufa kibudu.
 
Hao wote hawajulikana na umetaka wasukumu na wachaga ni mule mule tu ...Nakuambia ukweli ni sawa na CUF ambacho kilipotea hivyo hivyo, kilikuwa cha watu wa pwani ndio maana kilikufa kibudu.

..kwa hiyo pamoja na uongozi huo bado unasisitiza kwamba Chadema ni chama cha kaskazini, au cha Wachagga?

..chama chochote cha upinzani kinachoonekana kuwa na nguvu huwa vinapigwa vita kionekane ni chama cha kibaguzi.

..Cuf walipigwa vita kuwa ni Waislamu na magaidi. Ni nguvu za dola zikatumika dhidi yao. Kama utakumbuka viongozi wake walishtakiwa kwa UHAINI.

..UDP ya John Cheyo ilishambuliwa kuwa ni ya Wasukuma.

..Yaani Wasukuma walipokuwa UDP walikuwa wabaya. Alipokuja JPM na CCM Wasukuma wakawa watu wazuri.

..Siku CCM wakipata mgombea Mchagga usije ukashangaa jamii hiyo ikianza kupambwa kwa sifa kedekede.

..Hizo ni propaganda ambazo miaka 30+ tangu tuanze vyama vingi tunapaswa kuzipuuza.
 
Wasalaam ndugu zangu,

Kufuatia hali ya waandamaji na maoni ya baadhi ya watanzania kwenye mitandao ya kijamii, nimegundua CHADEMA hawana nguvu wala watu wengi kutoka na kukosa ushawishi. Chama cha CHADEMA kina misingi mizuri hasa ukiangalia sera zake za awali hata jina lake ni zuri (CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO), ni fupi ila limebeba dhamira kubwa.

Chama hiki kwa tathmini kadhaa kinaokena tatizo ni kwenye kuwafikia watanzania ili waweze kuelewa sera zake kuelekea kushika uongozi wa nchi. Je, kweli kitashawishi watu wapige kura kuwachagua ili kusika usukani wa kuongozi nchi? Baadhi ya mambo kadhaa ambayo yanawafanya CHADEMA Kufeli pakubwa ni kama ifuatavyo:-

Chama kinakuwa kama cha watu wenye asili fulani; ni mapema sana kama chama kimeshindwa kutanua wigo mkubwa ili kuweza kupata ushawishi kila kanda, kwa wakati mmoja ingekuwa ni rahisi kufanya maandamano nchi nzima na watu wengeitika.

Pia soma: Mwl. Nyerere alitaka vyama viwili imara vya siasa vishindane kama tunataka tufanikiwe

Msikifanye chama cha watu wa kaskazini pekee kwa kujaza viongozi wengi kutoka huko, jaribuni kutafuta watu kila kona ya nchi tena wawe kweny uongozi wa juu kwa sababu watu wengine wanafuata ushawishi wa watu wa kwao: je, mnajua kwa nn kwa sasa kule Mbeya kimeanza kushika hatamu? Ni kwa sababu wanaona watu wao kama kama Sugu na wengine wakiwa ndani ya chama hicho, kwa hiyo jaribuni kutanua wigo kusini, pwani, nyanda za juu zaidi.

Chama chenu kimegeuka sehemu ya kufanya vurugu; Mnaweza kufanya siasa safi bila kuathiri mambo mengine kama mlivyaonza mwanza ila sasa mnataka mambo ya vurugu. Hakuna mtu mstaarabu atakubali kujiunga na chama cha vurugu ila kuandamana ni haki yenu kikatiba hamna tatizo, jaribuni kuwajibika sio kubishana na polisi kila siku lumande kama mnavyojua serikali ilivyo. Hii ni nchi ina wasomi mambo ya vurugu sio mahali pake inaleta taswira mbaya kwa chama kwa ujumla: Mtu kama Lema ni vurugu tu badala ya kutoa sera safi ni kutisha watu! Mara anagombana na polisi!! Hii michezo achaneni nayo.

Kuweni na sera endelevu katika kujenga uhai wa chama sio kuibuka kwenye matukio kama vile mnatembelea kik ya watu fulani; Hiko ni chama bhana kiwe na hoja endelevu sio kujitokeza kwenye matukio tu.

Ongeleeni sana kuhusu sera zenu ili kuvutia wananchi na sio kusambaza chuki ili wananchi waichukie serikali iliyopo madarakani; mnaweza kuwa chama bora zaidi bila ya kusambaza chuki kwa wananchi kwa sababu wananchi ndio wanajua serikali inawajibika au laah, kwa nchi za kiafrika viongozi hawana wanalofanya kwa hiyo tumieni mda mwingine kushawishi watu kwa kutoa elimu nzuri. Suala la kusambaza chuki ni kuwapa mwanya washindani wenu kupata la kusema.

Baadhi ya mambo mnayoongea mtandaoni hamshawishi wananchi ila mnawakejeli wananchi kwa sababu mnatumia siasa rahisi ambayo haina logic kwa mtu mwenye akili; Tukiangalia maandamno ya jana basi utagundua hata wenye ushawishi wenu huko mitandaoni kama Twitter hawan hoja zaidi wanayoyaongea yanakejeli wananchi ya kujua: kwa mfano wanakuambia Mbowe ni tajiri halafu kaandamana wewe maskini hutaki, kwa kutumia akili kuandamana kwa Mbowe tajiri kuna logic gani?

Kama tajiri wale Top ten hapa bongo hakuna aliyeandamana. Wengine wanapost picha ya familia ya Mbowe sijui mkewe kasoma! Mara mtoo mtoto wa Mbowe kasoma sana anatokea familia ya kitajiri! sasa angalia hizo ni kejeli au ndio mnashawishi watu?

Acheni siasa rahisi kuweni na point endelevu ina maana maandamano yakipita hmtakuwa na hoja tena?
Kwani maandamano yangeruhusiwa kama ilivyo kikatiba na polisi wakatoa ulinzi mbona wangejitokeza watu wengi? Si majuzi tu waliandana kwa wingi? umesahau?
 
Chadema inatakiwa iwekeze sana vijijini hasa vijiji vya kanda ya ziwa ikiwezekana ruzuku yote ipelekwe huko ,wapiga kura wapo vijijini mjini tupo wapiga porojo mitandaoni
 
Wala sijasoma riwaya yako bali nimeyasoma maoni ya watu kadhaa nikagundua ulichoandika ni upuuzi mtupu.
 
..kwa hiyo pamoja na uongozi huo bado unasisitiza kwamba Chadema ni chama cha kaskazini, au cha Wachagga?

..chama chochote cha upinzani kinachoonekana kuwa na nguvu huwa vinapigwa vita kionekane ni chama cha kibaguzi.

..Cuf walipigwa vita kuwa ni Waislamu na magaidi. Ni nguvu za dola zikatumika dhidi yao. Kama utakumbuka viongozi wake walishtakiwa kwa UHAINI.

..UDP ya John Cheyo ilishambuliwa kuwa ni ya Wasukuma.

..Yaani Wasukuma walipokuwa UDP walikuwa wabaya. Alipokuja JPM na CCM Wasukuma wakawa watu wazuri.

..Siku CCM wakipata mgombea Mchagga usije ukashangaa jamii hiyo ikianza kupambwa kwa sifa kedekede.

..Hizo ni propaganda ambazo miaka 30+ tangu tuanze vyama vingi tunapaswa kuzipuuza.
CCM haiwezi kuwa na mgombea urais mchaga. Never ever!
 
Chadema inatakiwa iwekeze sana vijijini hasa vijiji vya kanda ya ziwa ikiwezekana ruzuku yote ipelekwe huko ,wapiga kura wapo vijijini mjini tupo wapiga porojo mitandaoni

..inaelekea watu wa mijini sio wapiga kura waaminifu. Lakini jiji kama Dar lina kura nyingi kuliko kanda yoyote ile.

..kabla ya 2015 Chadema walikuwa wamewekeza sana ktk kanda ya ziwa. Kama sijakosea walikuwa na karibia 40% ya mitaa na vijiji ktk kanda ya ziwa.

..sasa inabidi wajijenge upya baada ya hujuma zilizoelekezwa kwao kati ya 2016 na 2020. Kwa ujumla ni kwamba demokrasia yetu imeyumba sana ktk miaka 5 na vyama vya upinzani vina wakati mgumu sana.
 
CCM haiwezi kuwa na mgombea urais mchaga. Never ever!
Huu pia ni ubaguzi m-baya kabisa! Ni kweli kuna makabila yasiyotakiwa kutoa rais wa nchi? Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?."
Wanabodi,
Jee Watanzania hawana makabila yao?, Lazima tukubali tukatae, Tanzania tuna makabila makubwa, dominant tribes ambayo yana dominates. na makabila madogo, non dominate tribes. Kati ya haya dominant tribes lazima tukubali kuna baadhi yake wana ukabila wa kutisha!, kuna baadhi yake wana nyodo za ajabu!, kwani iliwahi kutamkwa au kuandikwa popote kuwa watu wamakabila fulani sio hawafai kuchukua urais wa nchi hii, bali hawawezi kupewa kwa sababu matokeo tunayajua!, hivi tuu walivyo na hizo nafasi kubwa kubwa walizo nazo sasa tayari ni miungu watu, wakiukwaa urais si ndio wataota pembe kabisa?!.

Ni general unwritten public opinion kuwa rais wa nchi hii asitokee kwenye hizi dorminant tribes!. Kuna wagombea fulani walinyimwa kura maeneo fulani kwa kuitwa wakuja!. Kuna mikoa fulani mgombea ambaye sio mzawa huitwa "kyasaka" na wanakuambia kabila letu kamwe haliwezi kumchagua "kyasaka"!. Jee huu soi ukabila?. Huu ukabila ni dhana tuu ya ukabila au ndio ukweli wenyewe kuwa kuna ukabila wa kichini chini kwenye siasa kwenye baadhi ya maeneo?.

Tushukuru marais wa Tanzania, wote wametoka katika makabila madogo non dormant tribes, siku akiingia rais kutoka haya makabila makubwa, na ikatokea anatokea kwenye hizi dominant tribes na akiwa ni mkabila, kutazuka ukabila wa ajabu, hadi mtashuhudia watu wakihutubia umma kwa lugha za kabila zao ndipo watu humu mtanielewa nilikuwa nazungumzia nini!.
Pasco

P
 
Huna hadhi ya kuishauri Chadema mkuu.
Ingekuwa una akili timamu,kwanza ungeanza kukemea utekaji,na mauwaji yanayofanywa na ccm kupitia Polisi wateuliwa.
Wananchi walishafikiwa zaidi ya unavyofikiri.
Acheni vyombo vya ulinzi na usalama vibaki na majukumu Yao.Then wanasiasa wawe na uwanja sawa afu tuone matokeo.

Kiufupi,kama umeshindwa kukemea yanayoendelea Nchini,basi wewe ni BOGASI TU.
Hauna faida,hata kama ww ni profesa inabidi nikuulize unabweka ukiwa wapi🤔.
 
Back
Top Bottom