Vyama vya upinzani hususani CHADEMA rekebisheni makosa mdogo mtafika mbali, Watanzania watawaunga mkono

Mfumo wa elimu wa nchi hii unahitaji maboresho makubwa. Inakuwa vigumu kuamini mtu mzima anaweza kuandika uzi mrefu namna hii huku akishindwa kueleza kiini cha tatizo.
Kama point huzioni basi jaribu kuangalia elimu yako .
 
Hao wote hawajulikana na umetaka wasukumu na wachaga ni mule mule tu ...Nakuambia ukweli ni sawa na CUF ambacho kilipotea hivyo hivyo, kilikuwa cha watu wa pwani ndio maana kilikufa kibudu.
 
Hao wote hawajulikana na umetaka wasukumu na wachaga ni mule mule tu ...Nakuambia ukweli ni sawa na CUF ambacho kilipotea hivyo hivyo, kilikuwa cha watu wa pwani ndio maana kilikufa kibudu.

..kwa hiyo pamoja na uongozi huo bado unasisitiza kwamba Chadema ni chama cha kaskazini, au cha Wachagga?

..chama chochote cha upinzani kinachoonekana kuwa na nguvu huwa vinapigwa vita kionekane ni chama cha kibaguzi.

..Cuf walipigwa vita kuwa ni Waislamu na magaidi. Ni nguvu za dola zikatumika dhidi yao. Kama utakumbuka viongozi wake walishtakiwa kwa UHAINI.

..UDP ya John Cheyo ilishambuliwa kuwa ni ya Wasukuma.

..Yaani Wasukuma walipokuwa UDP walikuwa wabaya. Alipokuja JPM na CCM Wasukuma wakawa watu wazuri.

..Siku CCM wakipata mgombea Mchagga usije ukashangaa jamii hiyo ikianza kupambwa kwa sifa kedekede.

..Hizo ni propaganda ambazo miaka 30+ tangu tuanze vyama vingi tunapaswa kuzipuuza.
 
Kwani maandamano yangeruhusiwa kama ilivyo kikatiba na polisi wakatoa ulinzi mbona wangejitokeza watu wengi? Si majuzi tu waliandana kwa wingi? umesahau?
 
Chadema inatakiwa iwekeze sana vijijini hasa vijiji vya kanda ya ziwa ikiwezekana ruzuku yote ipelekwe huko ,wapiga kura wapo vijijini mjini tupo wapiga porojo mitandaoni
 
Wala sijasoma riwaya yako bali nimeyasoma maoni ya watu kadhaa nikagundua ulichoandika ni upuuzi mtupu.
 
CCM haiwezi kuwa na mgombea urais mchaga. Never ever!
 
Chadema inatakiwa iwekeze sana vijijini hasa vijiji vya kanda ya ziwa ikiwezekana ruzuku yote ipelekwe huko ,wapiga kura wapo vijijini mjini tupo wapiga porojo mitandaoni

..inaelekea watu wa mijini sio wapiga kura waaminifu. Lakini jiji kama Dar lina kura nyingi kuliko kanda yoyote ile.

..kabla ya 2015 Chadema walikuwa wamewekeza sana ktk kanda ya ziwa. Kama sijakosea walikuwa na karibia 40% ya mitaa na vijiji ktk kanda ya ziwa.

..sasa inabidi wajijenge upya baada ya hujuma zilizoelekezwa kwao kati ya 2016 na 2020. Kwa ujumla ni kwamba demokrasia yetu imeyumba sana ktk miaka 5 na vyama vya upinzani vina wakati mgumu sana.
 
CCM haiwezi kuwa na mgombea urais mchaga. Never ever!
Huu pia ni ubaguzi m-baya kabisa! Ni kweli kuna makabila yasiyotakiwa kutoa rais wa nchi? Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?."

P
 
Huna hadhi ya kuishauri Chadema mkuu.
Ingekuwa una akili timamu,kwanza ungeanza kukemea utekaji,na mauwaji yanayofanywa na ccm kupitia Polisi wateuliwa.
Wananchi walishafikiwa zaidi ya unavyofikiri.
Acheni vyombo vya ulinzi na usalama vibaki na majukumu Yao.Then wanasiasa wawe na uwanja sawa afu tuone matokeo.

Kiufupi,kama umeshindwa kukemea yanayoendelea Nchini,basi wewe ni BOGASI TU.
Hauna faida,hata kama ww ni profesa inabidi nikuulize unabweka ukiwa wapi🤔.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…