DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 372
- 310
Wanabodi,
Inabidi tusome nyaraka za wakati katika kipindi ambacho wapinzani wanaishiwa nguvu. Labda kupungua kwa ushawishi wa vyama vya upinzani umesababishwa na chama tawala. Vile vile labda sera zao zimepitwa na wakati. Maoni mbali mbali kuhusu harakati za vyama vya upinzani yametolewa lakini takwimu muhimu ni kwamba chama kikuu cha upinzani (CHADEMA) kilipata mbunge mmoja tu wakuchaguliwa kwenye uchaguzi wa 2020.
Sidhani kama vyama vya upinzani vitafanya vizuri kwenye uchaguzi wa 2025 na kwasababu hiyo, nimeanza kujiandaa kisaikolojia kwa ajili ya serikali yenye wawakilishi wa chama kimoja tu. Hii ni ishara ya kuelekea kwenye udikteta lakini sio udikteta wote ni mbaya.
"Benevolent dictatorship" ni aina ya udikteta ambao viongozi hufanya maamuzi sahihi na yenye manufaa kwa wananchi bila kuminya haki na uhuru wa wananchi wao. Hii hupunguza sana urasimu na michezo ya kisiasa iliyopo kwenye demokrasia.
Serikali iliyopo madarakani itakuwa imejihakikishia ushindi kwenye kila chaguzi na mamlaka ya kufanya maamuzi yoyote bila kuwashirikisha wengi. Kwasababu hiyo, ni muhimu kwa mfumo huu kuhakikisha uwepo wa nidhamu, na umakini katika kuhakikisha kwamba serikali haikosei.