Haya ni matamanio ya kila mwanaccm kuwa CHADEMA ipoteze nguvu, ila CHADEMA wakifanya movement hata moja na kujaza watu, utaona CCM inaanza tena kujishikisha na vyombo vya dola
Iko hivi, CCM sio chama cha kizazi hiki, na haitakaa tena ivute hisia za watu hasa vijana wa kizazi hiki. CCM haina uwezo tena wa kushinda uchaguzi wowote kihalali, na haitakaa iwe tena na uwezo huo.
Ni kweli kuwa inaweza kuendelea kukaa madarakani, ila sio kwa ushawishi tena wa kisiasa, bali ni mashirikiano yao ya kihalifu na vyombo vya dola. Mfano mrahisi ni sasa, CCM iko zaidi ya 97% kwenye sehemu zote za uwakilishi, lakini isiyo na mvuto kabisa, huku wananchi wakipuuza box la kura.
Matokeo haya ya wananchi kulipuuza box la kura ni ishara ya wazi ya kuichoka CCM, na hii itapelekea machafuko huko mbeleni ili kuitoa CCM madarakani. Tuombe machafuko hayo yasiwe makubwa, maana yataliharibu Taifa letu.