Vyama vya Upinzani, kubalini kwamba sio udikteta wote ni mbaya

CDM wala haipo tena. Haina ushawishi popote zaidi ya Kilimanjaro na Arusha kidogo. Chama cha wahuni nani anataka?
Arusha ipi mkuu.Ilishazikwa muda mrefu.Kiongozi wa maana wa mwisho alikuwa ni Ally Bananga.
Hakuna uongozi wa Chadema Arusha.Lema nae kawa mkimbizi.
 
Machafuko gani tena?

Kwani mungu wenu si alishawasaidia kumuondoa dhalimu wenu bila kumwaga damu? Sasa machafuko tena kwani dhalimu bado yupo?

Hiiii bangosha..
 
Kilichopo ni kwamba CCM siyo chama Cha siasa Sasa hivi, CCM wakirudi kuwa chama cha siasa na kikategemea sanduku la kura, basi kesho tu asubuhi hawapo. Hiki chama kipo kwa nguvu ya TISS na Polisi, Hawa ndo sanduku lao la kura. CCM wakisema tunataka serikali za mitaa nchi nzima, TISS na Polisi wanatekeleza. CCM wakisema tunataka bunge la kijani tu, TISS na Polisi wanatekeleza bunge linakuwa la Chama kimoja. CCM siyo chama Cha siasa.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Uchaguazi ukiitishwa next week, wengi tutaamia upinzani ili kwenda kuona kuna nini huku. Porojo za ccm kujisifia kila siku bila kuruhusu kuhojiwa zimetukifu.
 
Tulikuaga na demokrasia ya chama kimoja na wala nchi yetu haikua na utawala wa kidikteta.
Kuvishinda vyama vya upinzani hadi kutoka kapa kwenye uchaguzi pia sio udikteta. Kwenye nchi yenye kila sifa ya umoja watu wanaweza amua kua na imani na chama kimoja peke yake. Tusisahau wakati wa ukoloni watanganyika waliipa tanu kura kwa wabunge wote ila kiti kimoja tu. Wakoloni wasingeweza kuiba kura kwa niaba ya tanu.
 
Kwa sasa, asilimia 99 ya nafasi za uongozi kuanzia serikali za mitaa zime chukuliwa na chama cha mapinduzi. Wananchi wana ruhusiwa kupiga kura lakini hilo tu halitoshi katika kushiriki kwenye uongozi wa nchi. Lazima kuna maamuzi mengi yanayofanywa na serikali bila ya kuwa na ridhaa ya wananchi. Serikali kama taasisi ina mamlaka ya kufanya kitu chochote bila kuwashirikisha wawakilishi kutoka vyama vya upinzani. Udikteta tayari upo, sio lazima uone watu wengi wame beba bunduki barabarani
 
Tunaelewa ila Udikteta ni Mbaya sama Au kwakuwa hujakutana Na Mkono wake live?

Nimeongezeka kg 7 tokea Magufuli amefariki , alale alipo huko
 
Technically unakubali kwamba Tanzania kulikuwa na Udikteta. Sasa ulishasema udikteta unamaanisha autocratic leadership, sidhani kama ukisema autocratic leadership utakuwa unamaanisha kuwa ndio mfumo mzuri .

Labda ujiuzlize ni sawa .tu aseme upo ujambazi mzuri na mbaya, au mauaji mazuri na mabaya, first place ulishasema mauaji tayari sio kitu kozuri halafu unakuja na borrow mind kusema yapo mauaji mazuri.

Vijana wa siku hizi kadiri siku zinavyoenda ndio mnapoteza uwezo wa kufikiria vizuri . No wonder we need only robots maana hamna tofauti.
 
Nitatumia neno "Systemic dictatorship" kuelezea hali iliyopo sasa hivi. Kutokana na "Mass psychology", viongozi wanaweza kuwafanya wananchi kufikiria kwamba nchi hii ni ya kidemokrasia wakati hali hiyo sio sahihi. Hali halisi ni kwamba mifumo iliyopo inaisaidia sana chama tawala kubaki madarakani na kuongoza bila ya kuwa na mpinzani. Hili lisipotumiwa vizuri linaweza kuzua jambo baya lakini hali hii ikisimamiwa kwa uangalifu kama ilivyo sasa hivi basi tutaendelea kuishi kwa amani na utulivu hata kama hatu shirikishwi sana kwenye shughuli za maendeleo.
 
And you find it plausible right?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…