Vyama vya upinzani vinawezaje kuepuka kuonekana vina sura ya kidini?

Vyama vya upinzani vinawezaje kuepuka kuonekana vina sura ya kidini?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Hili suala halisemwi lakini lipo. CUF kilikuwa cha kizuri na tishio cha upinzani. Shida yake kilionekana kama kina sura ya kiislamu. CDM kukawa vizuri sana lakini kikawa kama kina sura ya kikristo.

Imekuja ACT wazalendo lakini kinaonekana kama cha Zanzibar na Pwani kwa waislamu.

Chama kuwa na sura ya watu wote ni muhimu, si kupata madaraka tu bali zaidi ni kutawala kwa amani.

Vyama hivi vinawezaje kuepuka hili? CCM kimewezaje kuwa na sura ya watu wote?

Tujadili kwa kujenga.
 
Na yule Mwenyekiti wa CCM kuhudhuria mashindano ya Quran imekaa vipi?
 
Back
Top Bottom