DOKEZO Vyeo vya Mamlaka viwe na ukomo wa umri mwisho uwe miaka 45

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,446
Reaction score
1,645
Habari Tanzania !

Pole kwa uchovu wa hapa na pale kwasababu ya kulitumikia Taifa letu hili la Tanzania.

Poleni sana wanasiasa na watu wengine wenye njaa za madaraka na Mamlaka kwa mtazamo wangu huu.

Nawaomba sana ikiwapendeza kwenye lile LIKATIBA letu tutakaloliboresha muweke ukomo wa uongozi hasa hizi nafasi za Kisiasa zenye Mamlaka mfano;
1. Rais
2. Mawaziri
3. Makatibu na Wakurugenzi Wote
4. Wakuu wa Mikoa na Wilaya
5. Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Umri wa kutumikia hivyo vyeo usizidi miaka 45. Hii tuikazie kweli kweli na tuamue kwa pamoja. Sio kila mtu awe kiongozi sawa.

Sababu ni hizi zifuatazo;
1. Tuwaze sasa kuwajengea watoto uwezo wa kuwa watumishi wa Umma mahili, majasiri na shupavu na wenye nguvu kuu.

2. Tuimarishe Elimu yetu kama tunavyofanya sasa na tuwekeze kwenye uzoefu hasa wa kiungozi kuanzia ngazi ya Shule za Msingi na Sekondari mpaka Vyuo.

3. Hawa vijana wanauwezo wa kwenda kasi na mabadiliko na maendeleo ya tehama duniani tofauti na viongozi waliopo sasa Sokoni.

Karibu
 
Mimi binafsi naona hoja yako haina mashiko..... binafsi naona mtu mwenye umri huo(45) bado ana nguvu zake na ana uwezo mkubwa wa kulitumikia taifa kwa weledi, uzoefu na maarifa kama ataamua kulitumikia taifa.....

Mimi binafsi naona tatizo kubwa la taifa letu sio umri wa kiongozi au muda wa kukaa madarakani bali uwajibishwaji wa kimfumo na kisheria pale ambapo kiongozi aliyepewa dhamana na umma anapofanya ubadhirifu........

Sote tunaona na kushuhudia vitendo vya ubadhirifu, ufisadi na wizi wa kutisha kwenye mali za umma kupitia ripoti za CAG na report zingine za kifedha lakini mpaka leo hatujaona wahusika ambao ni wakuu wa hizo idara wakiwajibishwa na wale wachache wanaotolewa kama mbuzi wa kafara kuuhadaa umma tunaona adhabu zao zilivyo za kuchekesha kama sio kusikitishwa ukilinganisha na uharibifu alioufanya!!!

Ukiacha na uzalendo na uadilifu lakini pia mwanadamu anatakiwa kudhibitiwa tena kwa ukali ili kuzuia dhamira mbaya zinazochipua kila siku kwenye nafsi yake.....
 
Unamjua Salim Ahmed Salim nchi ilimuamini akiwa mwenye umri wa miaka mingapi?
Mfano wake unajua; alilitendea nini Taifa letu Tanzania enzi hizo ambapo matunda yake yanaonekana leo na wewe ukiwa mnufaika namba moja.
 
Umri wa 45 si ndo mtu amekomaa Sasa rais awe na miaka 25 kweli?
Amekomaa na nini; tangu lini Urais una uzoefu ?
Kiongozi yoyote anakuwa na uwezo wa asilia au kujengwa tukiweka mazingira hayo ya kuwatambua.

(Hii itapunguza tamaa ya madaraka).
Maana kama atapenda kutumika kwenye eneo jingine nje na vyeo vyenye Mamlaka ataomba kazi za Umma akifikia umri miaka 45 si anaruhusiwa kwa Sheria za Utumishi wa Umma kuajiriwa.
 
Okay sawa. Binafsi nadhani umri una matter kwenye urais.
 
Okay sawa. Binafsi nadhani umri una matter kwenye urais.
Mfano mzuri unaoujua wewe kwa hii hii nchi yetu ni Rais yupi alifanya vizuri chini ya 45 ukimlinganisha na mwenye juu ya 45?

Kama kigezo ni ukomavu mbona tangu Uhuru Wazee walikuwepo au wazee wa sasa ni bora sana kuliko wale wakale ?

Mtazamo siku zote huzaa matokeo unayoyataka.
 
Unamjua Salim Ahmed Salim nchi ilimuamini akiwa mwenye umri wa miaka mingapi?
Mfano wake unajua; alilitendea nini Taifa letu Tanzania enzi hizo ambapo matunda yake yanaonekana leo na wewe ukiwa mnufaika namba moja.
Najaribu kulitafakari andiko lako lakini bado sijapata mantiki yake......

Kama ulikusudia umri wa mtu mimi nimeweka wazi kwenye masuala ya kiuongozi sidhani kama umri wa mtu unaweza kuwa kigezo kikubwa(labda awe Mzee Sana).....bali uwajibikaji ndio jambo la msingi
 
Sijakupinga na mimi. Ukumbuke huu utaratibu wa mambo ya Umri ni hao hao viongozi walikaa na wakaona busara kwao kupitia Mfumo huo. Ila kwa uhalisia haufanyi kazi 100%.

Unajua tukiweka ukomo wa miaka 45. Unajua mambo mengi hii nchi yatabadilika na yatakuwa tofauti kuanzia; Jamii, Siasa, Uchumi, Sheria, Tehama nk

Huwezi kuona uzuri wa hili wazo endapo ukiwa unatamaa. Ila ukiishinda tamaa ndani yake kuna uzuri sana.
 
fact
 
Mtoa mada umezingua kwenye umri huu ndio mtu kakomaa tayar kwa maisha na majukumu,hekima mingi busara mingi halafu unataka asishike hizo nafasi?
 
Huo ndo umri wa mtu kushika mamlaka. Anakuwa amejifunza, amekomaa na hana mihemuko tena.

Nadhani ungeseme kuanzia 45 ningekuelewa.
 
Labda niseme tu kitu kimoja tukisimama kwenye ubinadamu na mapungufu yake hakuna umri sahihi utakaopendekezwa na kufanya kazi kwa 100%......hao walioweka huo utaratibu huo wa umri ni jitihada zao wakidhania ya kuwa inaweza kufanya kazi......

Zipo taasisi kadhaa zilizokuwa chini ya vijana walio chini ya miaka 45 lakini tumeona matokeo yake......

Hatupaswi kuishi maisha ya dhana wakati tunaweza kuweka mfumo utakaowafanya watendaji wawajibike kwa wananchi iwe kwa mapenzi yake au kwa kuogopa kitakacho tokea baada ya kwenda kinyume na alichokubali......

Sote tunaona mataifa kadhaa yaliyopiga hatua kimaendeleo mifumo yao ya uwajibikaji kwa watumiaji, viongozi na watawala wanaokwenda kinyume na sheria kali.....na sote tunaona nidhamu iliyopo kwenye uwajibikaji na utekelezaji....bila kuangalia umri wa mtu!!!!
 
Vyeo hivyo vinahitaji watu wanaoielewa jamii na taifa, wanaofahamika, waliotumia ujuzi wao kwenye fani mbalimbali, wasio na mihemko na wenye uwezo wa kufundisha wengine.
Mtu ambaye hajawahi kujenga, kununua gari au kumiliki mali nyingine kwa jasho lake akiwa kiongozi kwa ngazi hizo ni hatari sana kwa taifa.
Hizo ni nafasi za kutumikia wananchi zaidi. Vivyo hivyo ubunge.
Mbunge asiyejua bei ya sukari (watoto wa viongozi na wafanyabiashara wakubwa) siyo wawakilishi wazuri wa wananchi walio wengi, hasa kwenye nchi masikini kama Tanzania.
 
Hoja yako sio sahihi. Nakupa mfano unaoendana na umri.
1. Zamani ndoa zilifanyika kwenye umri mdogo; mfano mzuri ni wazazi wako si ndio. Na hizi ndoa zilidumu. Sasa hawa hawakuwa na hekima kama kizazi cha sasa wenye uzoefu wa mapenzi na umri mkibwa ila takwimu zinawaumbua kuwa kuna idadi kubwa ya mahusiano na ndoa nyingi kila siku kuvunjika (Je, hawa wa sasa wamepungukiwa nini).

Hiyo ndio jamii niliyokuwa naisemea kuwa itabadilika endapo tukiweka umri wa miaka 45.

Hatuwezi kuwa na viongozi wanaowaza kujilimbikizia mali kila siku. Hii hapana.
 
Tutaondoa kashfa kwa viongozi wa kitaifa kuwasakama kuwa watoto wao wanavuna mali za nchi yetu na kuzitapanya. Kwa huo umri lazima huyo kiongozi watoto wake wawe chini ya miaka 15 endapo akiwahi kupata kizazi sawa.
 
Tutaondoa kashfa kwa viongozi wa kitaifa kuwasakama kuwa watoto wao wanavuna mali za nchi yetu na kuzitapanya. Kwa huo umri lazima huyo kiongozi watoto wake wawe chini ya miaka 15 endapo akiwahi kupata kizazi sawa.
Bado unarudi pale pale kwenye DHANA....hali ya kuwa hili jambo halihitaji dhana bali linataka mifumo....kiungozi wa umma anatakiwa kubanwa kiuwajibikaji kimfumo na sio kwa kumjengea DHANA ya kuwa kwa hali hii au kwa mazingira haya atafanya vizuri......

Nchi zote zilizoamua kuyatafuta maendeleo kwenye jamii zao zilianza na kuimarisha mifumo kwa viongozi wao na sio kuwajengea DHANA... inatakiwa dhana yake nzuri ikutane na mfumo unaomdhibiti ili kuimarisha uwajibikaji
 
Kuongoza njia lazima uijue na kuipita, kwa ufanisi ni Bora kivitendo zaidi badala ya ndoto.
Rubani mzuri ni yule aliyerusha ndege tofauti tofauti na mara nyingi bila changamoto kubwa na nyingi.
Vijana waende sambamba na wazee kupata uzoefu.
Ni muhimu kujenga jamii kuanzia chini mpaka juu. Kuwaza kundi moja la umri au daraja kwenye jamii ni uthibitisho wa ubinafsi wa kiwango cha juu.
Social mobility ni muhimu sana kwa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…