Unaposisitiza kuwa tatizo si dhana bali ni mifumo, naomba ufafanue Mkuu,,,
ni mifumo ipi mahsusi unayoiona haipo au ni dhaifu kwenye uongozi wa umma?
Mifumo hiyo ingewekwa wapi na ingeendeshwaje ili kumzuia kiongozi yeyote, mzuri au mbaya kukiuka uwajibikaji?
Unaposema nchi zilizofanikiwa zilianza na mifumo, unaweza kutaja mfano wa mfumo mmoja uliowekwa kwanza kabla ya mabadiliko ya watu au fikra?
Na ikiwa dhana nzuri lazima ikutane na mfumo unaomdhibiti, je, ni nani anayeunda na kulinda mfumo huo kama si watu wale wale unaosema tusitegemee dhana zao?
Mwisho, je, tunapambana na tatizo la watu au tunakubali kuwa bila mfumo thabiti, hata watu wenye nia njema huishia kushindwa?
Kwanza ningependa kudadavua ni maana ya dhana kwa ujumla wake......
DHANA
Kwa tafsiri fupi ni namna ambavyo mtu unamjengea taswira ya muendelezo kwenye fikra zake kwa namna ambavyo unavyomuona au unavyomjua.....taswira hiyo inaweza kuwa nzuri au mbaya kulingana na mtazamo wa mtu anayemtazama huyo kwa utashi wake kulingana na unavyomuona au kumjua......
Dhana kwenye uongozi inakujaje!??
Msingi wa mtoa post amependekeza ya kuwa uongozi wa umma ukomo wake uwe mwisho miaka 45.....amejenga hoja yake kwenye dhana ya kwamba mtu umri huo atakuwa ameshazeeka na mwenye umri chini ya huo atakuwa bado angali ana nguvu za kuwatumikia watu wake.....na mimi nikaikataa hoja yake kwa kusema uongozi unasimamiwa na mifumo imara inayoleta uwajibikaji kwa kiongozi dhidi ya hao anaowaongoza!!!
Sasa mfumo nini
Kwa tafsiri yangu kulingana mjadala uliopo mezani....mfumo ni utaratibu uliowekwa na mtu, watu au kikundi cha watu kwa ajili ya kusimamia na kuongoza jambo fulani kwa kipindi fulani.......
Mfano
Kutungwe sheria ya kuwa kiongozi wowote wa umma akibainika kuhujumu, ubadhirifu na wizi wa mali yoyote ya umma basi hukumu yake iwe ni kifo!!....hiyo adhabu ni kubwa sana na yenye kuogofya......na itakuwa tishio kwa wale wote waliokuwa wakiutaka uongozi kwa nia ovu lakini si tishio kwa mwenye kuutaka uongozi kwa nia njema!!!
Kwa hiyo sheria itahakakisha utumiaji mzuri wa fedha zinazoelekezwa kwenye miradi ya kimaendeleo na wananchi kunufaika!!
Kwa maana hiyo hapo tunaachana na dhana ya kuwa mtu wa umri fulani, au mtu wa aina fulani, hawezi kuwa hivi au kufanya hivi bali tumeweka ulinzi wa kiutaratibu.....
Sio wote ni wacha Mungu kwa utashi wao kuna wengine ni wacha Mungu kwa kuogopa adhabu za Mungu baada ya kutenda uovu na kukiuka taratibu wake......watu hawahofii adhabu za Mungu bali wale WAOVU!!!
Na muktadha huo hata mataifa yaliyoendelea yana mfumo au utaratibu mzuri wa kuwasimamia, kuwawajibisha na kuwaadhibu viongozi wao wakiteleza kwenye uongozi wao bila kuweka dhana ya wema au ubaya wa mtu!!
Juzi hapa rais wa zamani wa ufaransa alihukumiwa kifungo jela kwa makosa aliyoyafanya kipindi cha utawala wake..... wakati hapa kwenye rais ana kinga ya kutoshitakiwa na mahakama yoyote kwenye ardhi hii kwa lolote atakalotenda akiwa madarakani!!!
Mpaka hapo nadhani utakuwa umeshapata taswira ya DHANA, MIFUMO na UONGOZI.....
Nawasilisha!!