Tetesi: Vyeti feki , Serikali imesalimu amri ? Waliondolewa bandari warejeshwa !

Hizo barua wanazopewa ni za nini , na zile za mwanzo ambazo hawakujibu zilikuwa za nini , na wakati ule wa mwanzo yale majina yaliyokuwa yanabandikwa ubao wa matangazo yalikuwa ya nini na nini walichokuwa wanaelezwa wahusika ?
 
Nami nimesikia wababe wa bandari wanarudi wote

Kweli nchi ina wenyewe
 
Hizo barua wanazopewa ni za nini , na zile za mwanzo ambazo hawakujibu zilikuwa za nini , na wakati ule wa mwanzo yale majina yaliyokuwa yanabandikwa ubao wa matangazo yalikuwa ya nini na nini walichokuwa wanaelezwa wahusika ?
Unajua pale Kuna mambo yafauatayo :
1. Kuna ambao waliwasilisha result slip za kidato cha nne (hawa wamepewa barua kujieleza kwa nini walifanya hivyo)
2.kuna ambao walioghushi vyeti vya kidato cha nne (hawa wameambiwa waje na cheti original kinachofanana na alichowasilisha kwenye jarada Lake la kazi),. Kundi hili haswa hawakusoma elimu ya sekondari au walipata sifuri matokeo ya kidato cha nne.
3. Hawa walibadili matokeo ya kwenye cheti cha form four kwa kughushi, yaani wenyewe wanaita kupendezesha cheti. Sasa hii unakuta mtu alipata div 3 au div 4. Kinachofanyika hapa ni kwamba anabadili zile alama za masomo. Unakuta ana div 2 au 1. Hapa cheti wakitizama kwenye mtandao wanakuta alama za zamani. Hawa pia wameambiwa walete vyeti original.

Hawa wote walipewa barua za kujieleza ndani ya siku saba, na chini kabisa watatakiwa wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu.

Kuna ambao waliwasilisha barua za kujieleza na kuna ambao hawakuwasilisha baada ya siku saba walizopewa kuisha. Sasa hao wamepewa barua wajieleze kwa nini ha wakujibu.
Swali hapa kama ulighushi cheti, je utapeleka cheti ulichoghushi ili wakushike vizuri au utakataa kujibu barua ili serikali ichukue hatua inazozifahamu yenyewe? Ndiyo maana humo bandarini kila mtu amekaa na alama za kujiuliza. Watu wanashinda kwenye nyumba za waganga. (received from my reliable source)
3.
 
Nimejikuta navunjika mbavu kwa kucheka ! Asante sana mkuu kwa kuongezea nyama .
 


Mkuu kichwani zimo kweli? Hii serikali imedhamilia kurudisha heshima Tanzania na haiwezi kurudi nyuma kwani kurudisha vihiyo na watu wasio na tija kwa taifa katika sehemu kama bandari ni kulirudisha taifa nyuma kimaendeleo. Hakuna nchi duniani inayoendeshwa na mambumbumbu, hii ilikuwa Tanzania katika awamu zilizopita lakini si kwa sasa. Mkuu, keep wishing, wewe kama unaona ajira imekupiga chenga uza matunda.
 
Source ya habari yako. Au ndo kama Facebook "Whats on your mind"
 
Kichwani zimo kiasi mkuu , zile za kuingilia Jf , tuendelee kutega sikio mjomba .
 
Uongo mtupu
 
Huo sio uongo huo unaitwa Umbea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…