Hii ni taarifa niliyomegewa na msamalia mwema , kwamba baada ya matenki ya fikra ya serikali kutumia darubini kuangalia maeneo mengine ya utumishi yanayoitwa nyeti , wakashauri mchezo uishie hapohapo.
Sasa ili kuua soo ikabidi wote walioondolewa Bandarini warejeshwe kazini , tena bila masharti yoyote , wakiwemo hata wale waliobainika kutokujua kusoma wala kuandika .
Wito wangu kwa serikali , tuwe makini tunapoamua kutangaza mambo kama haya ambayo huunguza NYUMBA na MASHAMBA .
Nakulilia Tanzania .