Vyeti vya ndoa

Vyeti vya ndoa

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2015
Posts
18,611
Reaction score
27,615
Ndoa ni muungano wa mwanaume na mwanamke kuishi pamoja maisha yao yote,huku wakijenga familia watakayoipata.

Kwenye ndoa kuna raha na shida,wanandoa hawana budi kuvumiliana katika kipindi kigumu kwenye ndoa yao kipite.

Hoja ni kwamba kuna ulazima gani kwa wanandoa kupewa cheti cha ndoa wakati bado hawajafuzu kukabiliana na kuzishinda changamoto za ndoa?

Maana ndoa zimekuwa zikivunjika mapema, kwa nini wasipewe vyeti wakifikisha miaka 25 au 50?

Umru huo wa ndoa utakuwa umepitia mengi magumu na kuyashinda.
 
Nonsense! Cheti hakionyesha watu wamefuzu kuishi maisha ya ndoa. Cheti kinaonyesha watu wamefunga ndoa na wanaanza kuishi pamoja. Ni kama tiketi ya basi. Inaonyesha unaanza safari na siyo umekamilisha safari.

Au kwa sababu kinaitwa cheti ndiyo umekariri kila cheti huwa kinaonyesha action imekamilika? Cheti kinaweza kutolewa pale action inapoanza au inapomalizika.
 
Cheri cha ndoa kinachopewa sasa

Ni kuwa katika wapenzi wengi tulionao Mimi na mwenzangu tumeshinda

Ishu ya mitihani iliyoko ndani ya ndoa mbona hata darasani tukimaliza mitihani bado INA endelea uraiani.
 
Back
Top Bottom