Vyeti vya shule na ndoa vinatofautiana majina, naomba ushauri jinsi ya kuvipeleka kwa HR

Karemboo

Member
Joined
Dec 17, 2023
Posts
32
Reaction score
44
Dr JF nmembers naomba kusaidiwa mimi vyeti vyangu vya kuzaliwa na shule majina yake ni ya kiislam “Mwanaidi Juma Katani” lakini ndoa yangu ni ya kikristo na majina ya vyeti vya ubatizo na ndoa ni “Janeth Juma Katani”. Sasa nimeshaajiriwa serikalini na nataka nipeleke vyeti vya ndoa kwa afisa utumishi, sasa naambatanisha nini ili kusiwe na mkanganyiko. Asante
 
Hapana nimezaliwa, nimesoma mpk namaliza shule majina yangu ni MWANAIDI JUMA KATANGA lakini nimeolewa kikristo ndo nikabatizwa na kupewa jina la janeth so cheti changu cha ndoa kikaandikwa JANETH JUMA KATANGA…. Sasa nataka kuupdate marital status kwa HR
 
Affidavit of names ndiyo pa kuanzia.
Waone mawakili au Mahakimu
 
Soma post uelewe usiniite vitu vya ajabu, hayo majina yametofautiana kwenye cheti cha ndoa tu baada ya kuolewa na mkristto. Vyeti vyangu vya kuzaliwa na taaluma vyote majina yanafanana ambayo ni ya kiislam
 
Mkuu si wewe...
Umejibiwa hapo juu na mdau, fanyia kazi..
 
1.Andika barua ya maelezo (cover letter)
Katika barua hii, eleza kwa ufupi kwamba una majina tofauti kwenye vyeti vya dini na vyeti vya umma (kama cheti cha kuzaliwa na ubatizo), lakini wote ni wewe.
Toa mfano:
“Ninathibitisha kuwa vyeti vyangu vya kuzaliwa (Mwanaidi Juma Katani) na cheti cha ubatizo/ndoa (Janeth Juma Katani) vyote vinahusu mimi, hivyo majina tofauti ni kutokana na tofauti ya dini.”
Hii husaidia afisa wa utumishi kuelewa tofauti bila kuibua mashaka.

2. Ambatanisha nyaraka zinazothibitisha utambulisho wako
Cheti cha kuzaliwa – Mwanaidi Juma Katani
Cheti cha ubatizo/ndoa – Janeth Juma Katani
Namba ya kitambulisho au pasipoti – Hii itathibitisha kuwa vyote ni wewe.
Kitambulisho cha Taifa au Passport – hakikisha jina linalooneshwa kwenye kitambulisho ni sawa na lile uliloajiriwa.

3. Ikiwezekana, toa affidavit / uthibitisho wa kisheria
Unaweza kwenda kwa notiari au tarafa/mtaa ili kutengeneza barua ya uthibitisho wa majina.
Hii barua itasema wazi kuwa:
“Mwanaidi Juma Katani na Janeth Juma Katani ni mtu mmoja, hivyo vyeti vyote vinahusiana na [wewe].”

4. Kuambatanisha na cheti cha ndoa
Wakati unapopeleka cheti cha ndoa serikalini, weka pamoja:
Cheti cha ndoa
Kitambulisho cha Taifa / Passport
Cheti cha kuzaliwa
Affidavit (ikiwa imefanyika)
Barua ya maelezo kwa afisa wa utumishi
Hii itapunguza mkanganyiko wowote.

Afisa wa utumishi atakuwa na nyaraka zote zinazothibitisha ni wewe, na majina tofauti hayataunda shida.

Ahsante
 
Nenda kaape mahakamani au kwa mwanasheria.
Peleka vyeti na hati ya kiapo.
Mahakamani unalipia stamp duty gharama ndogo kama pesa ya vocha ya muda wa maongezi kwenye simu.
 
1.Andika barua ya maelezo (cover letter)
Katika barua hii, eleza kwa ufupi kwamba una majina tofauti kwenye vyeti vya dini na vyeti vya umma (kama cheti cha kuzaliwa na ubatizo), lakini wote ni wewe.
Toa mfano:
“Ninathibitisha kuwa vyeti vyangu vya kuzaliwa (Mwanaidi Juma Katani) na cheti cha ubatizo/ndoa (Janeth Juma Katani) vyote vinahusu mimi, hivyo majina tofauti ni kutokana na tofauti ya dini.”
Hii husaidia afisa wa utumishi kuelewa tofauti bila kuibua mashaka.

2. Ambatanisha nyaraka zinazothibitisha utambulisho wako
Cheti cha kuzaliwa – Mwanaidi Juma Katani
Cheti cha ubatizo/ndoa – Janeth Juma Katani
Namba ya kitambulisho au pasipoti – Hii itathibitisha kuwa vyote ni wewe.
Kitambulisho cha Taifa au Passport – hakikisha jina linalooneshwa kwenye kitambulisho ni sawa na lile uliloajiriwa.

3. Ikiwezekana, toa affidavit / uthibitisho wa kisheria
Unaweza kwenda kwa notiari au tarafa/mtaa ili kutengeneza barua ya uthibitisho wa majina.
Hii barua itasema wazi kuwa:
“Mwanaidi Juma Katani na Janeth Juma Katani ni mtu mmoja, hivyo vyeti vyote vinahusiana na [wewe].”

4. Kuambatanisha na cheti cha ndoa
Wakati unapopeleka cheti cha ndoa serikalini, weka pamoja:
Cheti cha ndoa
Kitambulisho cha Taifa / Passport
Cheti cha kuzaliwa
Affidavit (ikiwa imefanyika)
Barua ya maelezo kwa afisa wa utumishi
Hii itapunguza mkanganyiko wowote.

Afisa wa utumishi atakuwa na nyaraka zote zinazothibitisha ni wewe, na majina tofauti hayataunda shida.

Ahsante
Karemboo kubadilisha jina ni jambo la kawaida na njia zipo nyingi za uthibitisha kama alivyoelekeza huyu mchangiaji. BTW ngoja nitoe ushauri: Pamoja na kubatizwa, ungeweza kubaki na jina lako tu. Mimi huwa naamini hakuna jina la kikristo wala kiislam. Kuna jamaa yangu ni mkisto yeye na mke wake lakini baadhi ya watoto wao wamepewa majina ya ''kiislam''.
 
Sasa nimeshaajiriwa serikalini na nataka nipeleke vyeti vya ndoa kwa afisa utumishi, sasa naambatanisha nini ili kusiwe na mkanganyiko. Asante
Wewe ni Mwalimu au ni kada ipi? Maana huu mchakato maelekezo yapo kipindi kilekile wakati unasaka ajira kunakua na maelekezo unapewa nini cha kufanya ikiwa majina yako hayafanani au yana walakini ni aidha ukaape Mahakamani au kwa Mwanasheria na upewe cheti cha kiapo aidha affidavit au deedpoll ndio ukishapewa hivyo vyeti unapeleka huko unapotaka kupeleka,

deedpoll ni pale unapokua na jina lenye changamoto sasa unataka kutumia jina fulani officially na kulikana jina fulani mfano hapo umesema jina lako ni Mwanaidi na pia jina lako lingine ni Janeth sasa ukichukua deedpoll unachagua jina moja lingine unalikana mfano unasema sasa mimi ni Janeth au kule kazini umeajiriwa km Janeth basi chukua jina la Janeth ndio liwe jina lako jina la Mwanaidi unalikana kwamba mimi silitumii tena jina hili na kuanzia leo hii halitokua tena jina langu ninalolitumia kisheria unapiga sahihi yako unagongwa muhuri wa Mwanasheria au Hakimu na yeye anagonga sahihi yake juu ya muhuri wake anakupa document yako unalipia unaondoka inakua imeisha hio,

tukija kwenye affidavit unayakubari majina yote Janeth na Mwajuma kwamba haya ni majina yangu kwa hio unaapa kwamba haya majina yote ni ya kwangu na yatambulike kisheria.

Kwa kesi yako wewe inabidi ukachukue Deedpoll, Mahakamani au kwa Mwanasheria uape sign hio document then umemaliza.

Case closed.
 
Hivi ukiolewa ni lazima ubadilishe majina? Usipobadilisha inakuwaje?

Nje ya mada..
 
Umehama dini kutoka ukristu kwenda Uislamu lazima Uslimu na ukitoka Uislamu kwenda Ukristu lazima Ubatizwe na katika michakato hio hapo kunakua na mlolongo wa kukubadirisha kuanzia jina na mengineyo yaan unapigwa msasa safi kuanzia jina lako km uliitwa Joyce jina linabadirishwa unaitwa Mwazani au Sikujua
 
Soma post uelewe usiniite vitu vya ajabu, hayo majina yametofautiana kwenye cheti cha ndoa tu baada ya kuolewa na mkristto. Vyeti vyangu vya kuzaliwa na taaluma vyote majina yanafanana ambayo ni ya kiislam
Kachukue Deedpoll achana na Affidavit, au muelezee hakimu hapo Mahakamani au Mwanasheria atakupa cheti sahihi cha wewe kujaza, ni simple sana why panicking?
 
Karemboo kubadilisha jina ni jambo la kawaida na njia zipo nyingi za uthibitisha kama alivyoelekeza huyu mchangiaji. BTW ngoja nitoe ushauri: Pamoja na kubatizwa, ungeweza kubaki na jina lako tu. Mimi huwa naamini hakuna jina la kikristo wala kiislam. Kuna jamaa yangu ni mkisto yeye na mke wake lakini baadhi ya watoto wao wamepewa majina ya ''kiislam''.
HAwawezi kukuelewa kirahisi
 
Hapana nimezaliwa, nimesoma mpk namaliza shule majina yangu ni MWANAIDI JUMA KATANGA lakini nimeolewa kikristo ndo nikabatizwa na kupewa jina la janeth so cheti changu cha ndoa kikaandikwa JANETH JUMA KATANGA…. Sasa nataka kuupdate marital status kwa HR
Nenda kwanza kwa wakili aliyesajiliwa au hakimu ukaape kuwa hayo majina ya kiislamu na hayo ya ubatizo wa kikristo ni majina yako.Ukipata hiyo affidavit,nanda kwa msajlii wa hati hapo mkoani ulipo upeleke hiyo affidavit iki uyasajiki hayo majina yote,na utalioia kiasi cha pesa,utapewa hati na risiti.Sasa kwa afisa utumishi peleka affidavit uliyopata kwa wakili au hakimu,cheti cha usajili wa majina na risiti ulivyovipata kutoka kwa msajili wa hati na utakuwa umekamilisha kila kinachotakiwa na utayatumia hayo majina yote kisheria
 
Back
Top Bottom