econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Naomba nishauri ya kwamba vyombo vya Dola viwekeze kwenye mambo ya maana na sio kwenye mambo ya kijinga. Kwa muda mrefu vyombo vya Dola vimewekeza akili na vifaa kwenye kupambana na vyama pinzani. Kuteka, kuua na kunyanyasa wapinzani. Ila akili ya kupambana na maafa ni zero.
Tuliona kwenye tukio la ndege kule Bukoba, ajali ya meli kule ukerewe na Leo ajali ya jengo pale kariakoo. Utayari wa kushughulikia majanga ni mdogo Sana ukilinganisha na kushughulikia maandamano ya wapinzani au nguvu ya kumteka na kumuua Mzee Ally Kibao. Akili nyingi ya vyombo vyetu ipo kwa wapinzani na sio kazi yao sahihi. Ndio maana mpaka Kuna kesi ya utapeli ya milioni mia nne polisi hawaangaiki nayo lakini wambie wampoteze aliyechoma picha ya Rais wapo haraka Sana.
Nashauri kwa Dunia ya Sasa vyombo vyetu vya Dola vibadilike kabla havijabadilishwa na wakati. Viachane na akili za mwaka 1970, na Sasa vijikite kwenye technolojia ya maafa na mengineyo.
Ni ushauri tu.