Vyombo vya Habari ifike wakati mseme sasa basi

Vyombo vya Habari ifike wakati mseme sasa basi

Ashasembeko

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
225
Reaction score
910
Ukandamizaji wa vyombo vya habari nchini haujaanza katika utawala wa Rais Magufuli. Nakumbuka kipindi cha Rais Kikwete, mnamo mwaka 2012, gazeti la Mwanahalisi lilifungiwa, na halijafunguliwa mpaka leo hii. Mwaka 2013, Magazeti mawili makubwa, Mwananchi na Mtanzania yalifungiwa kwa muda kwa siku 14 na lengine siku 90. Bado kuna waadishi kama Daudi Mwangosi waliouliwa kikatili na polisi.

Pamoja na yote yaliyofanywa huko nyuma, hakuna muda ambao vyombo vya habari vimekuwa na wakati mgumu kama miaka hii mitano ya utawala wa Rais Magufuli. Kuna waandishi kama Azory Gwanda waliopotea, kuna waandishi kama Bollen Ngeti waliotekwa, waandishi kama Erick Kabendera waliobambikiziwa kesi, waandishi kama Ansbert Ngurumo waliowindwa kama fisi mpaka ikabidi wakimbie nchi na wengine wengi waliokamatwa na polisi bila ufuatishwaji wa Sheria.

Tumeona pia vyombo vya habari kama Kwanza TV, Tanzania Daima, Mawio, Mseto na The Citizen (siku 7) yakifungiwa. Kibaya zaidi wakaleta mswada mkali "Media Services Act 2016" wa kudhibiti hivi vyombo. TCRA kutwa inawatoza faini na kuwatishia. Msemaji muu wa Serikali amekua Editor in chief wa vyombo vyote vya habari. Anawapigia wahariri na publishers kuwatishia kuchapisha habari ambao hawaipendi. Afu kinachosikitisha zaidi ni huyo msemaji ana PhD ya communications. Waziri husika nae ni mwanataaluma wa habari ila wapo mbele kuua hivi vyombo.

Tofauti ya vyombo vya habari enzi zilizopita na sasa ni kuwa, wakati wa Kikwete, pamoja na kuwa vilikua vinatishwa, vilikua vinajitahidi kusimamia taaluma. Mnakukumbuka jinsi IPP Media, ilikua inajibizana na serikali wazi wazi kutetea haki zake?

Sasa hizi najua hali imekua ngumu zaidi, ila kinachopaswa kwa waandishi na vyombo vya habari ni kuwa wamoja. Mkiona gazeti la mwezenu limefungiwa pazeni sauti. Mkiona habari mnayotaka kuchapisha inaendana na maadili yenu japo mnatishiwa na Dkt. Abass msichapishe, nyie chapisheni tu. Ndio watawafungia. Ila wakifungia vyombo vya habari vyote wanajiharibia wenywewe kwa wananchi na jumuiya ya kimataifa. Tuone kama wakibakisha TBC, Daily News na Uhuru na yale ya Musiba nani atafuatilia.

Inasikitisha sana kuona, vyombo vinatishiwa kuchapisha au kurusha mahojiano ya mgombea wa chama pinzani eti kisa hakijabalance stori. Magufuli akiwa anawatuhumu wapinzani wanatumiwa na mabeberu mbona hapo TCRA hawaulizi hivi vyombo kuhusu kubalance stori. Come on, let's be objective!!

Najua Vyombo vya Habari, mna familia na mnalinda kazi zenu, ila ifike wakati mseme sasa basi, maana mkiendelea kuchapisha habari zisizo na uzito au zenye upendeleo wananchi wataacha kununua habari zenu. Mmeona jinis mauzo ya gazeti la Mwananchi yanavyoshuka kila siku - maana kuna muda lilikua linatumika kisiasa, naona sa hizi kidogo wamejirekebisha. The Citizen ndio gazeti pekee ambalo kidogo, wanajaribu kustick kwa professional ethics. Sitoshangaa wakifungiwa very soon.

ITV sio super brand tena, maana ukitazama habari zao za saa mbili, ni habari za serikali tu, hata kukiwa na habari kubwa ya chama cha upinzani. This is unacceptable. Wataishia kususiwa kama TBC. Yaani, the only reason TBC inaendesha ni kodi zetu, la sivyo kingekua chombo binafsi kingeshakufa muda mrefu sanaaaa. ITV, Azam TV, Wananchi sio wajinga, wakipoteza imani kwenu mtakosa hata na hayo mapato mnayotaka.

Msimame pamoja, mtetee taaluma yenu. Kama serikali inataka kucontrol vyombo ifanye hivo kwa TBC sio kwenye vyombo private. Wanawasaidia kulipa mishahara?

Ifike wakati na nyie mseme sasa basi!!
 
Magufuli alisema vyombo vya habari havipo huru kiasi hicho.Yana mwisho lakini.
 
Nakumbuka gazeti la majira, lilivuma sana ya miaka ta tisini.
N
Baadae lilitiwa mfukoni na serikali.
Wanunuzi wakapungua hadi likajifia.
Vyombo vyetu vya habari kwa kutiwa mfukoni na serikali vinajichimbia kaburi.
 
Nakumbuka gazeti la majira, lilivuma sana ya miaka ta tisini.
N
Baadae lilitiwa mfukoni na serikali.
Wanunuzi wakapungua hadi likajifia.
Vyombo vyetu vya habari kwa kutiwa mfukoni na serikali vinajichimbia kaburi.
Kweli kabisa. Wananchi watachoka wakiona lila siku habari tu za upendeleo. Ataeomoa taalumu yaoo ni wao wenyewe.
 
Watanzania tunasumbuliwa sana na ubinafsi.Kila mtu mpaka yamkute ndio ajue kun tatizo huku wengine wanajitia upofu na kujipendekeza ili tu wapewe uteuzi.Hata hivyo,wakati unakuja kila mtu atakjikuta ni mhanga na hapo ndio wote tutaungana na kusema sasa basi.
 
Jiwe ana ka-ujinga kabaya sana na haka ndiko katamwangusha vibaya, mpaka sasa hivi vyombo vya nje kama BBC, DW na CNN wanalalamika sana kuhusu kufungiwa kutoa habari za Tz. Kuna makubwa yanakuja.
 
Kutokurusha habari za Chadema ndio kusema kwao kwamba sasa basi
 
Kulikuwa na mwandishi mmoja , matata anaitwa Charles Charles na gazeti la Heko, sijui anaandikia gazeti gani siku hizi.
===
Vyombo vya habari vifuate sheria. Ndiyo maana yule Mwandishi nadhani ndiye Mhariri wa Gazeti la Jamhuri alilazimika kwenda kusoma sheriz bpale mlimani. Lengo lake aepuke usumbufu wa kisheria kwenye kazi yake. Aliwahi kusema hajawai kujutia uamuzi wake huo.

Hata, Mkuu Paskali alifanya uamuzi huo...ingawa baadaye alikuja kujikwaa kwa Bunge. Pia sidhani kama naye anajutia uamuzi wake huo.
 
Millard Ayo juzi alicheza nao vizuri sana.. Alikava matukio yote live..

Lissu akichukua form na uviccm wakiwa kwenye uchaguzi.

Wakamkosa.

Ila sidhani kama ataachwa tu zeti eksitenti..
 
Kulikuwa na mwandishi mmoja , matata anaitwa Charles Charles na gazeti la Heko, sijui anaandikia gazeti gani siku hizi.
===
Vyombo vya habari vifuate sheria. Ndiyo maana yule Mwandishi nadhani ndiye Mhariri wa Gazeti la Jamhuri alilazimika kwenda kusoma sheriz bpale mlimani. Lengo lake aepuke usumbufu wa kisheria kwenye kazi yake. Aliwahi kusema hajawai kujutia uamuzi wake huo.

Hata, Mkuu Paskali alifanya uamuzi huo...ingawa baadaye alikuja kujikwaa kwa Bunge. Pia sidhani kama naye anajutia uamuzi wake huo.
Tatizo linakuja pale mamlaka kama TCRA, zinaoverride sheria za nchi, Mfano ni jinsi kwanza TV, ilivyofungiwa kwa kurepost tahadhari ya ubalozi wa marekani kuhusu hali ya COVID-19 nchini. Kisheria, Kwanza TV haijafanya kosa lolote, ila TCRA, ikatafsiri sheria inavyojua wao na ikakifungia hiko chombo. Japo Kwanza TV wamesema wataenda mahakamani tunajua ni mlolongo mrefu sana, mpaka waje wapate haki yao.
 
Back
Top Bottom