Kati ya mambo ambayo Rais Magufuli amefeli kabisa ni kwenye kulinda misingi ya utawala wa sheria, haki za binadamu, uhuru wa maoni na demokrasia.
Mambo haya ambayo ndiyo msingi mkubwa wa ubunifu na maendeleo, Rais Magufuli amayafanya vibaya kuliko Rais yeyote tuliyewahi kumpata.
Leo hii nchi kama China, nchi yenye eneo kubwa na idadi kubwa ya watu kuliko nchi yoyote, inayategemea mataifa madogo kama Netherlands, Singapore, Hong Kong, kuwekeza kwenye uchumi wake.
Kwenye ugunduzi wa teknolojia, mataifa kama Israel, Sweden, Finland na Norway, yanaiacha China kwa mbali. China imebakia kuwa nchi ya copy and paste. Sababu kubwa ya China kuwa hivyo - wataalam wa Sayansi ya Binadamu wanatuambia ni kutokana na mfumo uliowalea Wachina. Mfumo wa kunyimwa uhuru wa kufikiri, uhuru wa maoni, na demokrasia ya kuchagua mtu anachotaka. Na huyu wa kwetu anapenda sana atufanye tuwe Taifa la manunda. Taifa la watu wasio na uhuru wa kufikiri, kutoa maoni yao, kukosoa, kukataa, au kuwa na demokrasia ya kuchagua watu wanachokitaka.
Waandishi wa habari, wananchi wa kawaida na wenye nafasi mbalimbali ni lazima tulikatae hili. Lazima Taifa liwe na watu walio huru kuhoji, kufikiri, kujaribu na kuamua. Taifa ambalo Mwalimu aliwahi kusema, lenye vijana jeuri.
Kuwa Rais, Waziri, Mkurugenzi n.k. siyo chochote katika uwezo wa akili. Taifa lina mamilioni ya watu. Ndani ya kundi hilo kuna super intelligent people pia. Na watu hao siyo Marais, siyo mawaziri, wakurugenzi au wakuu wa mikoa. Watu hawa ni lazima wawe huru katika kuhoji na kufanya mambo yao ili tuweze kusonga mbele.
Sent using
Jamii Forums mobile app