Vyombo vya Habari ifike wakati mseme sasa basi

Millard Ayo juzi alicheza nao vizuri sana.. Alikava matukio yote live..

Lissu akichukua form na uviccm wakiwa kwenye uchaguzi.

Wakamkosa.

Ila sidhani kama ataachwa tu zeti eksitenti..
Kusema ukweli, kuna vyombo ambavyo vinajitahidi na vinajitoa ufahamu. Kuna gazeti la The Citizen, we soma habari zake, unaona kabisa wako objective, japo nina uhakika watafungiwa very soon. Pia kuna hizi online channels kama Millard, Dar Mpya, Jenerali Online na Mwanahalisi.
 

Tena nadhani walisomea namna ya kuandika kwenye sheria kandamizi.
 
Kiburi hiki cha mkuu wa kaya ni njia ya haraka ya kumjiangusha yeye mwenyewe.Naona yeye kila lililo mbele yake analikabili kwa nyundo.
 
Taarifa ya habari ya Azamu ni mkutano wa UWT; Leo wameshindwa ukumbini...

Habari za Lissu na CDM hawagusi... kwa sasa wameungana na ITV kuwa TBC 2 and 3 respectively.
 
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]
 
Kati ya mambo ambayo Rais Magufuli amefeli kabisa ni kwenye kulinda misingi ya utawala wa sheria, haki za binadamu, uhuru wa maoni na demokrasia.

Mambo haya ambayo ndiyo msingi mkubwa wa ubunifu na maendeleo, Rais Magufuli amayafanya vibaya kuliko Rais yeyote tuliyewahi kumpata.

Leo hii nchi kama China, nchi yenye eneo kubwa na idadi kubwa ya watu kuliko nchi yoyote, inayategemea mataifa madogo kama Netherlands, Singapore, Hong Kong, kuwekeza kwenye uchumi wake.

Kwenye ugunduzi wa teknolojia, mataifa kama Israel, Sweden, Finland na Norway, yanaiacha China kwa mbali. China imebakia kuwa nchi ya copy and paste. Sababu kubwa ya China kuwa hivyo - wataalam wa Sayansi ya Binadamu wanatuambia ni kutokana na mfumo uliowalea Wachina. Mfumo wa kunyimwa uhuru wa kufikiri, uhuru wa maoni, na demokrasia ya kuchagua mtu anachotaka. Na huyu wa kwetu anapenda sana atufanye tuwe Taifa la manunda. Taifa la watu wasio na uhuru wa kufikiri, kutoa maoni yao, kukosoa, kukataa, au kuwa na demokrasia ya kuchagua watu wanachokitaka.

Waandishi wa habari, wananchi wa kawaida na wenye nafasi mbalimbali ni lazima tulikatae hili. Lazima Taifa liwe na watu walio huru kuhoji, kufikiri, kujaribu na kuamua. Taifa ambalo Mwalimu aliwahi kusema, lenye vijana jeuri.

Kuwa Rais, Waziri, Mkurugenzi n.k. siyo chochote katika uwezo wa akili. Taifa lina mamilioni ya watu. Ndani ya kundi hilo kuna super intelligent people pia. Na watu hao siyo Marais, siyo mawaziri, wakurugenzi au wakuu wa mikoa. Watu hawa ni lazima wawe huru katika kuhoji na kufanya mambo yao ili tuweze kusonga mbele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumefikia mahali pabaya kabisa ktk tasnia ya habari Tz kuliko kipindi kingine chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…