Vyombo vya habari na wananchi wapuuza bajeti ya 2023/2024 iliyopitishwa leo 26/06/2023; kwanini haijadiliki?

Vyombo vya habari na wananchi wapuuza bajeti ya 2023/2024 iliyopitishwa leo 26/06/2023; kwanini haijadiliki?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Hii bajeti ya kwanza kupitishwa bungeni na jamii nzima kukaa kimya bila kuiweka kwenye agenda ya siku

Miaka yote tumezoea siku kama ya leo kunakua na mijadala mizito ya kada mbalimbali lakini mwaka huu hali imekuwa tofauti. Hali hii siyo nzuri kwa mustakabali wa kesho wa nchi yetu. Yawezekana bajeti ni nzuri ila wananchi wamekata tamaa kutokana na aina ya mijadala iliyopo bungeni; yawezekana bajeti siyo nzuri na watu pia wamekwazika kwa namna hizi bajeti zinavyowasilishwa.

Tusikae kimya kwa kuamini kwamba mambo yanakwenda; tutafute uungwaji mkono wa jamii katika vitu sensitive kama hivi....tujiulize kwanini nchi inyamaze siku kama ya leo?

Waziri Mwigulu amejibu mambo mengi leo bungeni lakini watu wamepuuza. Hata vyombo vya habari vilivyokuwa bungeni havijayaweka hayo kwenye headlines....tuamke tusidhani mambo yanakwenda. Lazima tutafute nini kimefanya bajeti ikose attention ya umma...


Community engagement imeshuka sana na kupuuza kumeongezeka...tulizoea watu kuhoji kupanda kwa mishara hakuna, watu kuhoji unafuu wa kodi napo kimya....kuna nini?
 
Samia mwenyewe hajaifwatilia... anaongea kwa hasira na hofu kuu... DP World ni zimwi kali. Linaondoka na mtu.
 
Bandari nimuhimu kuliko hiyo Bajeti ya mchongo.
 
Tunapitia report ya TLS iliyochambua uhovyo wa mkataba wa bandari.
 
Back
Top Bottom