MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Nianze na kuvisikitikia vyombo vya habari hasa baadhi ya TV stations kubwa kubwa hapa nchini na baadhi ya magazeti. Mnafanya ubaguzi kwa kuonesha live coverage kwa matukio ya CCM pekee. Endeleeni na ubaguzi huu iko siku mtasema ukweli.
Tundu Lissu anazunguka mikoani kutafuta wadhamini na matukio yake anahudhuria na maelfu ya watu ambao wanasimamisha hata kazi zao kwa masaa, hizi ni habari na matukio yanayoaswa kusomwa kwenye taarifa zenu na kuandikwa pia kwenye magazeti.
Eti mnatishwa, kwanini anayewatisha msimwambie aende mahakamani au aliwafungia mkamshtaki ili haki itendeke?
Kama tukio la Lissu kutafuta wadhamini ni haramu si mngeshaona amepelekwa mahakamani?
Endeleeni kulinda ugali wenu kwa kuogopa kuwapa watanzania ukweli. Andikeni habari zenu kwa kuchagua lakini hamtafanikiwa.
Sijajua udhaifu wenu kwenye sheria ya nchi uko sehemu gani? Hivi hamna wanasheria wa kusimamia vyombo vyenu mnasubiri kutishwa tu?
Siasa hazitabiriki, huyu mnayeogopa kumuonyesha siku akiwa Rais wenu mtafanyaje?