Vyombo vya Habari Tanzania ubunifu ni zero kabisa

Vyombo vya Habari Tanzania ubunifu ni zero kabisa

666 chata

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
1,700
Reaction score
3,921
Watangazaji wote wanaongea kwa mfanano mmoja, ni ajabu sana, unakuta reporter wa TBC hana tofauti na reporter wa ITV, house style moja. Sauti moja yaani kama ndo wanajifunza kutangaza.

Watangazaji wanatangaza kwa kunata nata sana its like slow motion, sentesi moja ina tamkwa kwa sekunde 17 yaan kusema tu "tutaenda mjini" wao wanasema "tu--ta----- enda mjini lakini hapaa".

Sasa wale wa vipindi vya michezo ndio zero zero kabisa!! Jamaa wanatangaza hadi habari za juzi, alaf wanaongea kwa dk 2 dk 28 matangazo na hizo dk mbili dk moja wanarudia kusisitiza juu ya matangazo ambayo tayari yameshatangazwa.

Vipindi vya muziki ni hopless kabisa kabisa, wote wanaongea style moja lugha moja.

Imagine mpaka leo kuna vituo vya TV et bado wameweka ka nembo ka mti christmas kama moja ya logo za pembeni pale.

Sasa iv kila redio ina promote kamali, so sad.

Sisi wateja wenu tumewachoka, na mie nnae yazungumza haya kwa mwaka natazama tv na kusikiliza redio kwa siku chache chini ya 9 ktk siku 365 za mwaka ila nimekereka hivi, je hao wanaosikiliza kila siku sasa? Zama zinakwenda mbio, badilikeni kuweni wabunifu.

Haya ni mawazo na maoni positive ya mdau anaetamani upya ktk tasnia hii adhimu na mahiri kweli kweli ktk kila nchi.
 
Hivi nyie mnapata wapi mda kusikiliza hivyo vyombo vya habari kama TBC ITV mara chanel10 nk
 
Kamali hizo ni biashara man wana earn pesa za kuendesha kituo sometimes endapo wana wadhamini wachache walionunua airtime... Ila ubunifu wa vipindi kiukweli radio nyingi chenga sana, wengi wanaforce wafanane na ile MAWINGU....
 
😀 😀 😀 😀 Redio zetu hizi huwa nazisikiliza kwenye mwendo kasi tu. Watangazaji wengi katika kipindi kimoja alafu wote kichwani 0
 
Halafu unakuta mtu kama Zembwela anadadavua jambo huku akishawishi wasikilizaji waamini kile anachokiamini yeye
Tatizo tulipogeuza utangazaji ni kipaji siyo taaluma hapo hapo tukaribu kabisa ila kwakua tasnia ya habari wameamua wao tasnia yao iwe hivyo acha liende
 
Boss mbona uraumu mapadri wa katoriki ile tone yao ipoje au mashekhe wetu zile tone zao
sasa pale kwenye TV, ni kituo cha sala cha RC, mpaka unaanza kufananisha. Kule RC ni utaratibu wa ibada kwa misingi yao ya kiimani. Tuwe wakweli ubunifu wa waandishi wetu wa TV uko chini sana
 
Wanapenda kuigana. Mimi naona wa itv wana ubunifu sana hasa wa habari. Kila mkoa mtangazaji ana unique character yake ya utangazaji.

Kuna wakati kila mtangazaji wa viredio uchwara alikua anataka atangaze kama millard ayo
 
Back
Top Bottom