Hata mfanano wa vipindi TV zote Tz karibu zinaelekeana. Ikifika saa 2 wote taarifa ya habari. Na habari zenyewe ni wote ni zile zile. Mfano ukifungulia ITV saa 2. 20 labda ndio wanamtangaza jambazi kukamatwa na polisi,ukaamua ubadirishe Chanel uende labda UTV utashangaa unakutana na hiyo na picha ni zile zile.
Na bahati mbaya wote wanatangaza habari zile za kawaida,nyepesi ambazo wananchi mitaani wameshazizoea wanakutana nazo kila siku. Hakuna TV yenye habari za uchumguzi (kama ilivyokuwa TBC ya Tido Mhando,mihabari ilikuwa ya uchumguzi ilikuwa huwezi kukosa taarifa ya habari.
Na hawa waliokuja kukamata matangazo ya TV Tz,hawa Azam ndio kabisa hawana ubunifu kabisa. Wamefocus kukamua watu tu hela ndefu lakini zinapotea tu hamna kitu cha maana. Sijui Tido kazeeka ama wamempiga pin.
Hata matamthilia yao yanaboa sana tofauti na zamani tulivyokuwa tunaangalia ITV tu yale matamthilia kama CAMILA,ACAPULCOBAY,zilikuwa zinasisimua hasa. Sio hizi za Azam,utafikiri hadithi za shigongo kufa na kufufuka. Za watoto na wanawake tu.
Zinaboa sana. Nataka niweke DStv nione