Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
MALISA GJ
Baada ya Lissu kunusurika risasi 37 na waliompiga, ama kutojulikna , na baadaye kupokwa ubunge wake, na pia kunyimwa matibabu na mafao yake, na watu ambao wana majina ya watakatifu , "Yoana Nduguwai" na "Yohana Alcohol Padlock" huku wakimtakia kifo, Mungu kamtende miujiza kaibuka mzima na majereaha mwilini.
Wauaji hao ambao hawajulikani "Mungu anawajua" wapo tu wanavuta pumzi huku roho zikiwauma kutokumuua Lissu.
Vyombo vya Habari vya ndani haviripoti habari zake, ITV hawakuweka habari za Lissu alipowasili SINGIDA na kupokelewa na umati wa watu zaidi elfu ishirini.
Nimekuwa nikisoma kwenye vitabu na sasa nashuhudia kwa macho. Uhuru wa habari unakanyagwa na watu hawathubutu kukemea kwa sababu ya HOFU. Vyombo vya habari vilivyoalikwa kuripoti tukio la Lissu kuchukua fomu havijatokea kwa sababu ya HOFU.
Azam wakavuka kiunzi cha HOFU na kwenda kuripoti. Lakini ghafla wakakatisha matangazo na kufuta post zote zinazohusu Lissu kuchukua fomu. Nimeshangaa sana.
Kuna watu wanashangilia kuona uhuru wa habari ukiminywa ili wafurahishe mamlaka. Na wengine wanaogopa kukemea ili nao wasiingie kwenye makucha ya mamlaka. Tukifika hapa hakuna aliye salama.
Jana @advocate_jebra alieleza kisa cha Simba na Kondoo. Simba alifungiwa kwenye kizimba kwa siku kadhaa. Akawa anatafuta msaada wa kufunguliwa kwa nje. Kondoo akapita. Simba akamwambia nifungulie naahidi sitakula. Kondoo akamwambia Simba apa, akaapa. Kondoo akamfungulia.
Alipotoka akamrarua kondoo na kutaka kumla maana alikua na njaa ya siku kadhaa alizofungiwa kwenye kizimba. Wanyama wengine wakapita wakakuta Simba na Kondoo wakizozana. Kondoo akajielezea, Simba nae akajielezea. Simba akakiri ni kweli aliahidi hatamla kondoo lakini ana njaa ya siku 3 afanyeje?
Wanyama wote kwa sababu ya HOFU wakaunga mkono maelezo ya Simba kuwa amle tu kondoo, maana alikua na njaa.
Kobe akasema hajaelewa mkasa huo vizuri. Akamuuliza Simba unasema ulifungiwa kwenye kizimba? Simba akajibu ndio. Akamuuliza kipi? Akamwambia kile pale? Akamuuliza mbona kidogo sana? Uliwezaje kukaa humo? Simba akasema nilikuwemo. Kobe akamwambia hebu ingia tuone kama kweli uliweza kuenea humo. Simba akaingia, kobe akafunga komeo kwa nje na kuondoka.
Kobe akawaambia wanyama wenzie. Leo Simba angemla kondoo mngejiona mko salama kwa sababu si nyie mmeliwa. Lakini kesho angepata njaa tena, na hatujui ingekua zamu ya nani.
Ukiogopa kukemea uonevu haimaanishi kwamba upo salama. Inamaanisha umejiweka kwenye hatari zaidi. Leo vyombo vyote vimeungana na mamlaka kuzuia habari za Lissu. Nilipoona Azam wamerusha matangazo nikasema angalau tumempata Kobe wa kuokoa wenzie.
Mara ghafla kobe huyo naye akaungana na wenzie kumtetea Simba amle kondoo. Bila kujua kesho Simba atapata njaa tena na hawajui itakua zamu ya nani.
#Picha kwa hisani ya CHADEMA