Vyombo vya Habari vya Kimataifa vinapata faida gani kuzusha uongo kuihusu Tanzania na Rais Magufuli ?!. Angalia uongo/uzushi wa The Guardian la UK!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Wanabodi, kila nipatapo fursa huwa ninawaletea makala ndefu za Kwa Maslahi ya Taifa, hivyo leo nimepata fursa tena naendelea na zile makala zangu za kuhamasisha uzalendo kwa jina la "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo zinaendeshwa kwa mfumo wa maswali, leo nazungumzia media za kimataifa zinafaidika nini kwa kuzusha uongo kuihusu Tanzania?, na hawa sources wao ambao ni Watanzania wenzetu, wanafaidika na nini kwa kuwa feed info za uongo, uzushi au kubuni?, what do they stand to gain?. Kuzusha uongo dhidi ya taifa lako na viongozi wake kwenye media za mabeberu ni uzalendo?!.

Ni muda mrefu baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa zikiwemo TV, Majarida na Online contents zao kutunga maurongo kuihusu Tanzania kumkashifu au kukashifu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na rais Magufuli, katika maendeleo ya Taifa letu Tanzania, wao watabeza, watakashifu na sometimes hata kumtukana rais wetu, swali la kujiuliza ni vyombo hivi, vinapata faida gani kwa kututungia uongo au kutuzushia na kumzushia rais wetu Magufuli tuhuma za uongo?. What do they get or what do they wish to achieve?.

Katika janga hili la Corona, rais wetu Magufuli anasifiwa duniani kote kwa hatua alizochukua kupambana na Corona, ikiwemo kugomea lockdown, sasa hebu soma makala hii ya gazeti la The Guardian la Uingereza, jinsi ilivyo shehenezwa mauongo na mauzushi kuihusu Tanzania na rais wetu Magufuli!.
Tanzanian president accused of covering up Covid-19 outbreak

Wakati serikali yetu imetoa idadi ya vifo ni kwa huku Tanzania bara ni vifo 16 tuu, na walioambukizwa ni watu 489, hawa jamaa kupitia source wao, wanadai eti Tanzania inaficha idadi ya vifo na maambukizi ya Corona, wandai kuwa wao wameambiwa na source wao kuwa watu waliokufa kwa ugonjwa wa Corona kwa Dar es Salaam tuu pekee ni zaidi ya watu 400!, huku watu zaidi ya 20,000 wameambukizwa nchi nzima!. Huu ni uongo kabisa!, kama serikali yetu imesema waliokufa ni watu 16, then ukweli wa waliokufa ni 16, sasa hiyo idadi ya uongo na uzushi wanaipata wapi na kwa uongo kama huu una malengo gani?, wanapata faida gani kwa kuzusha uongo mkubwa kama huu?!.

Kwa faida ya wale wavivu kufuata links, nakuwekea makala yote, nikiainisha nini ni kweli, nini ni uongo na nini ni uzushi,
Coronavirus outbreak
Tanzanian president accused of covering up Covid-19 outbreak
John Magufuli has repeatedly played down the threat from the pandemic
Jason Burke Africa correspondent
Wed 27 May 2020 17.43 BSTLast modified on Wed 27 May 2020 19.45 BST



My Take
Hawa jamaa wanapata nini kwa kutuzushia uongo?. What do they stand to gain?. Na nyinyi Watanzania wenzetu mmafaidika na nini kwa kuwa vibaraka wa mabeberu na kutunga uongo kuhusu nchi yenu?!.
Uzalendo wenu uko wapi?.

Nawatakia Alhamisi Njema

Paskali.
 
Binafsi haijalishi ni nani au nani kikundi gani au chama gani.

Taifa gani au genge gani maadamu linakashfu Taifa kwa kivuli chao wao wana fikra pana na tuziishi fikra zao.

Basi kwangu mimi binafsi ni wapuuzi kama wapuuzi baadhi ya wapuuzi waliopo ndani ya Taifa.
 
Mkuu UK mbali kote huko? Tz tu kwenyewe kuna watu wazushi vibaya mno. Mwanzoni tuliwaamini ila imefikia hatua sio wa kuamini kabisa maana asilimia kubwa ya mambo wanayosema baadae yanabainika ni uongo. Mbaya zaidi kila kitu wanataka wawe wa kwanza kusema.

Kwa ujumla tunaishi kwenye dunia ambayo kila siku kunazalishwa mamilioni ya taarifa na kusambazwa kila dakika na kati ya hizo nyingi ni uongo au ukweli uliochezewa.
 
Pascal Mayalla,

Kupata ukweli wa nai mwongo kati ya viongozi wetu na hao wanaohita mabeberu, tungepata ushahidi ulio huru toka oande zote mbili bila kuweka vikwazo au vipingamizi.

Kitu kama kipo, kipotu na huwezi kuficha. Sasa wenzetu wako tofauti na huku kwetu. Wao wanasemaga ukweli wa jambo bila kuficha wala kujali madhara ambayo yatatokea kwa viongozi wake. Huku kwetu tunaficha ukweli ili kuwalinda wakuu.
 
awamu yenu ikipita itabidi tuwajengee masanamu.
Worst term ever, mnajaribu kupambana n hao mnaowakopa daily.
Ni kama kutukana wakunga.
Nchi zinazoendekea kiuhalisia kuna mikomo kwenye baadhi ya vitu, hasa kwenye afya za watu, anachokifanya meko ni kucheza na afya ya wananchi wake
 
M Mchungaji fake wa river side ubungo atasoma hii post?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…