Vyombo vya habari vya kimataifa kutoka Africa na nje ya bara la Africa vimeonesha wasiwasi kuwa Tanzania inaweza kurudi nyuma katika masuala ya haki, uhuru wa kujieleza na demokrasia.
Hayo yamesemwa kufuatia hotuba ya rais Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania yaliyofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro mapema wiki hii.
Katika hotuba yake rais Samia alionesha kuchukizwa kwake na jinsi vyama vya siasa, vyama vya kutetea haki za binadamu na balozi za nchi za Ulaya na Marekani zilivyokuza habari za utekaji na mauaji ya baadhi ya watu nchini.
Katika hotuba yake rais alivitaka vyombo vya kimataifa viache Tanzania ijiamulie mambo yake kupitia katiba halali iliyopo.