Waandishi wa Habari, ambao wenyewe wanapenda sana waitwe WANATAALUMA, wana mwili wa nyama na damu.
Wanakumbuka fika kuwa Azori Gwanda amepotezwa.
Wanakumbuka fika yaliyomfika Mwandishi Kabendera.
Tuwaonee huruma.
Siyo wao peke yao.
Watanzania tulio wengi tumejazwa hofu, ingawa tofauti yetu ni kwamba, hofu hii haitufanyi tulime mazao vibaya, au tutibu wagonjwa hovyo hovyo.
Kazi zote za kitaaluma zinaendelea, na hapa ndipo Waandishi wa habari inabidi wajiulize kama uandishi wa habari ni taaluma kweli.