Vyombo vya Habari vya Tanzania vinaripoti, havichambui. Tatizo lipo kwenye taaluma au ni kukosa wachambuzi?

Vyombo vya Habari vya Tanzania vinaripoti, havichambui. Tatizo lipo kwenye taaluma au ni kukosa wachambuzi?

Mkuu kwenye hivyo kuna wahandisi wa habari kibao... Wapo radhi kufanya uchambuzi au kualika wachambuzi wenye akili ndogo ili muda uishe au habari iruke hewani au gazeti liingie mtaani!!
 
Siku hizi wanaosomea uandishi wa habari ni wale vilaza darasani.......
Utaskia amekosa hata journalism tu[emoji1787][emoji1787]
Sijui kama zamani pia ilikuwa hivi.
Sio kweli kaka....kila Media House inakuwa na Editorial policies zao....kipi kiandikwe na kipi kisiandikwe, mbali na hivyo yapo makosa ya kiubinadamu, lakni pia media nying za bongo kwa sasa hivi zimeacha kuchukua watu ambao ni wataaluma kwenye media na mwishoe wameanza kuwachukua watu maalufu na wenye mashabiki hata nje ya media mfn Baba levo, Swebe, Stv Nyerere na wengine wa mfano wao, so hawa hupelekea media zionekane za hovyo
 
Kwanini matukio yote yanayotoka serikalini yanaripotiwa lakini hayachambuliwi na vyombo vyetu vya habari? Mfano, toka uteuzi ulipofanyika jana hakuna habari mpya kuhusu wateuliwa isipokuwa kile alichoripoti Msigwa. Nini Tatizo?
It's very unfortunately media ya Tanzania hatuna uwezo wa uchambuzi!.
P
 
Nadhani ni yote mawili.
 
Kwanini matukio yote yanayotoka serikalini yanaripotiwa lakini hayachambuliwi na vyombo vyetu vya habari? Mfano, toka uteuzi ulipofanyika jana hakuna habari mpya kuhusu wateuliwa isipokuwa kile alichoripoti Msigwa. Nini Tatizo?
Hakuna uhuru wa habari wala taarifa ya habari, wanapindisha pindisha kuiogopa serikali.
By trueboy Nay wa mitego
 
Ili uchambue hizo habari inabidi kwanza usikilize ushauri wa mwanasheria kwanza,kwa maaana endapo uchambuzi wako utaenda tofauti na mawazo ya wakuu unaweza kuwa hatarini kwa kushawishi umma kupandikiza chuki ama kuhamasisha vurugu
 
Do you look for news or opinion shows/pieces!?kwa wenzetu waMarekani tv na radio hua wametenga muda wao hewani ,Tv nyingi za Habari hua night shows hua ni opinion programs kama za kina Tucker Carlson ,Chris Cuomo na Don Lemon, na mchana hua ni strictly reporting the news unakutana na kina Bret Baier.

Sasa opinion shows kule ndio zimeleta divisiveness kubwa especially kipindi cha Obama na Trump na kwa sasa Bw Joe Biden....swali langu unadhani sisi tumefikia hatua ukomavu wa kisiasa na kifikra kusikia chambuzi ambazo zinaweza kua negative au positive kwa wasikilizaji?

Kwangu mimi ni hapana,sije tukawapa waandishi wa Habari personal vendettas.
 
Mi naweza sema sababu ni hizi hapa
1. Freedom of expression - hii imeminywa sana kipindi hiki mpaka kupelekea watu kufanya analysis ya jambo lolote kuhusu siasa.

2. Taaluma - waandishi wengi wa habar Tanzania hawana ubobezi kwenye fani nyingine, kwa hiyo automatically anakosa uwezo wa kufanya analysis ya aina yoyote, mwisho inakuwa ni news reporting, ambayo naamini haina msaada wowote.

Mwisho wa siku, utashangaa analysis nzuri utaipata kwenye hii mitandao ya kijamii kwa watu ambao sio waandishi wa habar
 
Mi naweza sema sababu ni hizi hapa
1. Freedom of expression - hii imeminywa sana kipindi hiki mpaka kupelekea watu kufanya analysis ya jambo lolote kuhusu siasa....
Point ya kwanza ndo yenye nguvu zaidi mkuu. Yaani siku hizi ukianza kuchambua lazima uangalie hili litakuwa salama kwangu na kwa media house? So bora kureport tu mkuu.
 
It's very unfortunately media ya Tanzania hatuna uwezo wa uchambuzi!.
P
Basi ndio maana mnaitwa Makanjanja. Kwenye Article nisipoona jina la Jenerali Ulimwengu sisomi.
 
Nadhani mijadala mingi ilikufa during JPM regime.......before vilikuwepo vipindi vya mijadala
 
Kwanini matukio yote yanayotoka serikalini yanaripotiwa lakini hayachambuliwi na vyombo vyetu vya habari? Mfano, toka uteuzi ulipofanyika jana hakuna habari mpya kuhusu wateuliwa isipokuwa kile alichoripoti Msigwa. Nini Tatizo?
Kazi ya chombo cha habari na kutoa habari kama zilivyo bila kuzipindisha. Unachoita "kuchambua" ndiko kupindisha habari, ambao ni kazi ya pundits huko spinning room, siyo kazi ya professionals walioko newsroom.
 
Kwanini matukio yote yanayotoka serikalini yanaripotiwa lakini hayachambuliwi na vyombo vyetu vya habari? Mfano, toka uteuzi ulipofanyika jana hakuna habari mpya kuhusu wateuliwa isipokuwa kile alichoripoti Msigwa. Nini Tatizo?

Jamiiforums ndiyo kimbilio la wengi kwa kuchambua taarifa.

Mifano ni mingi, na wa karibu ni habari ya Thobias Mwesiga Richard aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC.

Ni Jamiiforums pekee iliyojiongeza kuchambua taarifa ya msemaji wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Msigwa kwa kina na mapana kama Thobias Mwesiga Richard anatosha ktk nafasi Mpya aliyoteuliwa au la, kwa manufaa mapana ya taifa la Tanzania.

Na kweli tukaona Mamlaka husika ya uteuzi kwa kasi ikaamua kutengua uteuzi wa Thobias Mwesiga Richard.
 
Back
Top Bottom