Kibosho1
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 2,621
- 4,293
Japo ni ngumu kwa nchi za Afrika lakini bado tunaweza.
Tumeona naibu rais tayari ameagiza jeshi la polisi kuanza kutumia mfumo wa kurekodi matukio yao wanapokuwa kazini, jambo jema sana lakini bado kunahitaji mengi zaidi.
Miradi mbalimbali sa serikali inakwama au kuendelea taratibu tofauti na mipango hili likisababishwa na uzembe wa watu waliowekwa kazini.
Ufisadi umekithiri katika miradi hiyo hiyo ambayo kuna uzembe kwenye usimamizi, sio miradi tu, hata katikati ofisi za umma kuna uzembe na hakuna mkemeaji, mashirika ya mengi ya serikali inajiendesha kwa hasara, dawa ni nini?
📸jamiiforums
Umuhimu upo kwa vyombo vyote lakini asilimia kubwa naipa nafasi JamiiForums. Nitaeleza sababu.
UMUHIMU WA WAKE
Lengo ni kuijenga Tanzania kwa ujumla, tuliona kipindi cha nyuma yalikuwepo magazeti fulani lakini changamoto yao yaliegemea upande fulani wa kisiasa.
Mfano mtandao wa Wikileaks au shirika la habari la Uingereza BBC. Shirika hilo limekuwa likitoa ripoti mbalimbali za kiuchunguzi ambazo nyingi zinaibua matukio yaliyo kinyume cha sheria. Hili linafanyika hata inapohusu mambo ya serikali bila kujali ni shirika la serikali bado liko tayari kuweka wazi makosa ya kiongozi wa serikali.
📸BBC
VYOMBO VYA HABARI VYOTE VINAWEZA ILA JF INA NAFASI ZAIDI.
JAMIIFORUMS ni jukwaa ambalo kila mdau anaweza kuandika na kuripoti chochote, na kupitia wasimamizi wa jukwaa wanaweza kutuma kwenye mitandao mingine. (mfano ishu ya uchakachuaji wa mafuta ulivyokuwa)
(Barabara ya mwendokasi Mbagala imekamilika kwanini haizinduliwi, je ni magari hakuna, je ni haijaisha au kuna tatizo lingine?) mfano wa jambo la kuchunguza
USHAURI KWA JAMII FORUMS
Imefika wakati sasa wa kutafuta waandishi na kutoa semina jinsi wanavyoweza kufuatilia matukio kisiri na kwa kujifanya hata ni raia wa kawaida huku wakiwa na vifaa vinavyohitajika kama kamera ndogo, vinasa sauti nk. Wakati fulani wanaweza hata kuhoji wananchi au kujifanya hawajui chochote. Ikiwa mdau ataripoti kero au jambo lolote si vibaya mkaingia kwa ndani zaidi ili kujua ukweli.
FAIDA KWA UMMA NA WANANCHI KWA UJUMLA
Kama kutaibuliwa tuhuma na ushaidi wa picha, sauti au video basi kila mzembe na fisadi lazma waogope kula rushwa au kuwa wazembe kazini na chombo husika kingepata wafuasi na watembeleaji wengi sana.
Kwa hakika Tanzania tukipata vyombo vyenye uthubutu kama mifano niliyotaja hapo juu basi miaka ijayo tutapata viongozi ambao wako makini sana sababu uoga wa kuripotiwa.

Upvote
1