Vyombo Vya Rasmi vya Habari vya TZ, Havitimizi wajibu Wake, Njaa, Ukata, Ujinga!. Waandishi, Wamiliki Watakiwa Kujiongeza- Jicho Letu Star TV

hil

kazi yao ni kuimba mapambio tu
Nje ya mada, kutokana na maneno yaliyo kwenye kichwa cha habari: Pascal Mayalla na members wengine. Huu msemo wa mtaani wa ''kujiongeza''. Hivi neno linatakiwa kuwa ''kujiongoza'' au ni ''kujiongeza''? Mimi nadhani msemo huu unatokana na ''kujiongoza'', yaani kutumia akili zako na kujiongoza mwenyewe bila kungojea amri au ushauri wa mtu mwingine. Kwanini iwe ''kujiongeza'' ambayo ina maana ya kuongezeka kimo?
 
nakubaliana na wewe mkuu
 
Nchi hii ni maskini, kila mtu ana njaa. Utatimizaje wajibu wako una njaa? Mmeisaidia ccm kuua upinzani ambao ndiyo ungekuwa chachu ya taasisi mbalimbali kutimiza wajibu wake.
Hii divide & rule iliyotengenezwa haiwezi kutuacha salama.
African dictactorship philosophy..let them be poor to rule.Wafanye kuwa masikini uwatawale.Mtu yeyeto mwenye njaa atamtumikia mwenye shibe,thus wanasiasa,wasomi,wataalamu wanaweka pembeni taaluma zao kuiponya njaa.Chaguzi ni mbili utii maagizo ushibe au usimamie utaalamu badala ya maagizo usife njaa.
 
Kujiongoza linaweza kuwa sahihi na kujiongeza likawa sahihi vile vile.

Kujiongeza sio kujiongeza kimo pekee! Yaweza kuwa kujiongeza kimaarifa kwa kutafuta mbinu mbadala, kujiongeza kimtazamo kwa kubadili mtazamo wa awali, kujiongeza kiubunifu kwa kuwa mbunifu zaidi!

Anyway tuiache mada iliyolengwa zaidi kwenye post hii ijadiliwe tusiweke vitu vingine visivyohusika
 
Pascal Mayalla, binafsi najivunia sana ninapoona mwanafunzi wangu Leonard Mapuli anapongezwa kwa kazi nzuri.
 
Ni kama tunavyodhani akina Mbowe, zito na wachache ndio wapambane Sie tuje tishangilie ushindi tu... Hilo halitowwzekana
Kabisa mkuuu. Ujue hata jeshi lipo kwaajili ya raia. Raia tukionyesha kuwa hatuatak uongozi huu basi wao watasapoti. Lkn kila siku tanataka zitto mbowe lissu maalim seif watusemee. That is nonesense
 
Ni kama tunavyodhani akina Mbowe, zito na wachache ndio wapambane Sie tuje tishangilie ushindi tu... Hilo halitowwzekana
Kabisa mkuuu. Ujue hata jeshi lipo kwaajili ya raia. Raia tukionyesha kuwa hatuatak uongozi huu basi wao watasapoti. Lkn kila siku tanataka zitto mbowe lissu maalim seif watusemee. That is
Hiyo deepdown ndio imempoteza Azory, jf ina kesi mahakamani ambayo iko kwenye hatua ya kusomwa hukumu.
afu bado watu wanalaumu kina paskali. Ikiwa maxence mpaka leo anahudhuria kesi mahakaman kisa jf je ingekuwa wat humu hawana anonymity sijui ingekuwaje. Ni rahisi sana kumsema paskal vby but he knows the pain of the thorn in his foot
Maxence mwenyewe ni kwasabb ya afanyeje but am sure hapendi kupotezewa muda wake kortin kila mwez.
Achilia mbali vitisho pengine anavipata
 
Yaan sasa ndio nimegundua kuwa Pascal Mayalla nyota yako.ni ya musa. Kuwatoa wana wa israel utumwan misri kuwapeleka kanaani. Hebu fanyia kazi hili bhanaa. Huoni comment za watu humu?
 
Tunalaum uhuru wa habari kuminywa ,someeni na nyie huo uandishi wa habari au wapelekeni watoto wenu, Wake zenu, waume zenu wakasomee uandishi wa habari tuone kama watakuja na mbinu mpya ya kuleta uhuru wa vyombo vya habari.
Nani hataki kuishi akiwa na familia yake.
Watu mnamlaum Pascal sijui kafanya nini. Pascal mjanja hataki kuacha familia yake kisa tu awafurahishe ninyi yeye familia ikikosa hata vitumbua vya chai huku mkicheka kuwa alikuwa na kiherehere cha kujifanya anafanya utafiti wa kihabari.
Mtu mwenye akili zake anajua nini cha kufanya wapi, lini , kwa nani na kwa namna gani.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa hali ilivyo vyombo vya habari na wamiliki wake wako kwenye wakati mgumu sana.

Kwa ccm ilikuwa jambo jema sana kwao vyombo vya habari kuishia kusema tu kuwa sumaye ameachana na CDM kwa sababu demokrasia haijatendeka, hili ndiyo lilikuwa lengo kuu.

Kama vyombo vya habari vingeenda mbali zaidi ya hapo maana yake vingeneutralize habari nakuonekana Sumaye ni mlalamishi tu na busy body katika siasa, suala hili lingeua hoja zote za ccm na hivyo lingegeuka kuwa pigo kwao.

Hivi Paschal mmiliki gani wa chombo cha habari yuko tayari kuona chombo chake kimefungiwa kuzipa airtime habari za CHADEMA ?

Ni Mmiliki gani wa chombo cha habari yuko tayari kushitakiwa kesi ya uhujumu uchumi kwa chombo chake kutoa airtime kwa habari zinazoihusu CHADEMA?

Ni mmiliki gani wa chombo cha habari yuko tayari kupelekewa tax assessment kubwa kuliko hata net Value ya asset zake zote zinazoendesha hicho chombo cha habari ?

Je mwandishi gani wa habari yuko tayari kumfuata Azory Gwanda ( disappeared and died) na Daud Mwangosi kwa kuandika habari za CHADEMA ?

HIVI KATIBA ITAKUWA SULUHISHO PEKEE KATIKA JAMII HII INAYOONA HAKI ZAKE NI HISANI YA WATAWALA WAO ?
 
Wewe umesimamia upande upi njaa,ulimbukeni ,[emoji56][emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…